Ads Right Header

Buy template blogger

SANE SASA KUIBUKIA BAYERN MUNICH

SANE SASA KUIBUKIA BAYERN MUNICH

LEROY Sane, kiungo wa Manchester City inaelezwa kuwa amemalizana na Klabu ya Bayern Munich ili aitumikie timu hiyo msimu ujao.

Kiungo huyo amemaliza mkataba wake ndani ya Manchester City iliyo chini ya Kocha Mkuu, Pep Guardiola na inaelezwa kuwa amegoma kuongeza dili jingine.

Taarifa zinasema kuwa Bayern Munich wamekubali kuvunja benki na kuweka mezani kitita cha pauni milioni 54.8 kwa ajili ya kupata saini yake.

Licha ya kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha City alishindwa kuonyesha makeke yake jambo ambalo linamfanya afikirie kupata changamoto mpya.

Jana Sane alionekana akiwa kwenye jiji la Munich jambo linaloongeza nafasi ya kuibukia ndani ya klabu hiyo.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4