WATIA NIA ZA UBUNGE 15 NA UDIWANI 190 WAOMBA RIDHAA MKURANGA
Janeth Raphael, Michuzi Tv.
Na Janeth Raphael, Michuzi TV
JUMLA Ya watia nia wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa katika nafasi za ubunge 15 na udiwani 190 wamerudisha fomu za kuwania nafasi hizo katika Mkoa wa Pwani Wilayani Mkuranga, ikiwa ni sehemu ya mchakato unaoendelea nchi nzima kwa sasa kwa hatua ya awali ya kusaka wawakilishi wabunge na Madiwani.
Akizungumza na Michuzi Tv leo Wilayani humo Katibu wa CCM Wilaya ya Mkuranga Rukia Mbasha amesema kuwa Wilaya ya Mkuranga ina kata 25 na zoezi limekamilika salama na waliotia nia ya kugombea nafasi za Ubunge wamefikia 15 na nafasi za udiwani 190.
Aidha Katibu huyo Amesema kuwa;
"kwa ujumla zoezi la uchukuaji fomu na kurudisha lilienda vizuri hapakuwa na changamoto yeyote na kumekuwa na mwamko mkubwa sana ukilinganisha na mwaka 2015." ameeleza.
Pia Mbasha amewapongeza wote waliojitokeza na amewaombea kwa Mungu kwa kila aliye sahihi Mungu ampe nafasi ya kuongoza wananchi na kutatua changamoto zao kwa weledi na kusukuma maendeleo ya nchi mbele katika kumsaidia Rais Magufuli na kusimamia ilani za chama hicho.
Mwisho.
Previous article
Leave Comments
Post a Comment