YANGA KUIBUKA NA MAJEMBE MAWILI YA KAZI DHIDI YA SIMBA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa ana uhakika wa kuwatumia wachezaji wake wawili kwenye mchezo wake wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba wa Kombe la Shirikisho.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 12, Uwanja wa Taifa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu imedhamiria kutinga hatua ya fainali ili kutwaa taji la FA.
Wachezaji hao wawili ni nahodha wa kikosi hicho, Papy Tshishimbi ambaye yupo nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha pamoja na Bernard Morrison ambaye alikuwa na mvutano na timu kuhusu suala la mkataba.
Eymael amesema:"Tshishimbi tayari ameanza mazoezi mepesi hivyo ananiongezea upana wa kikosi kwa ajili ya mechi yetu dhidi ya Simba ambayo kwetu ni muhimu.
"Morrison yeye amerejea tayari na ameanza mazoezi na wenzake akiwa na furaha na ameniambia kwamba yupo tayari kucheza kwenye mchezo dhidi ya Simba."
Yanga ipo safarini leo kuelekea Mara, ambapo itakuwa na mchezo wa ligi Julai 5 dhidi ya Biashara United.

Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment