Ads Right Header

Buy template blogger

YANGA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU MORRISON

YANGA YAFANYA MAAMUZI MAGUMU KUHUSU MORRISON

LUC Eymael,raia wa Ubelgiji, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hataki kusikia kabisa jina la kiungo wa Yanga, Bernard Morrison.

Maamuzi hayo magumu yametokana na Eymael kutofurahishwa na matendo ya nyota huyo ambaye inaelezwa kuwa anawindwa na watani zao Simba.

Morrison amekuwa kwenye mvutano na viongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba, yeye anadai mkataba wake ulikuwa ni wa miezi sita na umemeguka huku Yanga wakieleza kuwa ni kandarasi ya miaka miwili.

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa ikiwa Morrison hana mkataba na Yanga basi anapewa ruhusa ya kusaini anakohitaji.

"Kama yeye ni mchezaji huru basi aende kusaini anakohitaji maana tumechoka sasa kuzungumzia suala lake, aende tena nasema aende akasaini haraka," alisema.

Eymael amesema kuwa kwa sasa hataki kuskia jina la mchezaji huyo na hataweza kuzungumzia masuala yake.

"Kuhusu Morrison kwa sasa siwezi kuzungumzia masuala yake na wala sitaki kuskia jina lake atamalizana na uongozi," amesema.

Bado Morrison hajajiunga na Yanga kwa sasa tangu atolewe Uwanja wa Taifa dakika ya 64 ambapo alisepa uwanjani na bodaboda.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4