BWALYA WAHUSISHWA KUIBUKIA YANGA NA SIMBA
Larry Bwalya mwenye miaka 25 yeye ni kiungo mshambuliaji anakipigandani ya Ligi Kuu ya Zambia kwenye Klabu ya Power Dynamos anahusishwa kujiunga na Yanga na inaelezwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaendelea vizuri.
👉Walter Bwalya mwenye miaka 25 huyu ni mshambuliaji wa zamani wa Nkana FC (The Red Devils) kwa sasa anakipiga Ligi Kuu ya Misri kwenye Klabu ya El Gouna FC yeye anahusishwa kujiunga na Simba.
Kwa muda mrefu Bwalya amekuwa akitajwa kuibukia Simba ila kikazwo awali ilikuwa inatajwa kuwa ilikuwa ni dau kubwa ila kwa sasa mambo yanaelezwa kuwa safi kwa pande zote mbili kuelewana.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wapo vizuri katika masuala ya usajili wana imani ya kuwa na kikosi bora cha ushindani.
Leave Comments
Post a Comment