HAYA HAPA MAJEMBE SABA YA KAZI AMBAYO YAMEMALIZANA NA YANGA
Hii hapa orodha kamili ya wachezaji wazawa ambao wameshamalizana na Yanga watakipiga msimu wa 2020/21 na tayari timu inaendelea na mazoezi pale Uwanja wa Chuo cha Sheria,:-
Farid Musa yeye ni kiungo mshambuliaji alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya CD Tennerife ya Hispania na mkataba wake ulikuwa umekwisha.
Yasin Mustafa yeye ni beki wa kushoto alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Polisi Tanzania.Zawadi Mauya anacheza nafasi ya kiungo mkabaji alikuwa anakipiga ndani ya Kagera Sugar.
Bakari Nondo Mwamnyeto yeye ni beki wa kati alikuwa anakipiga ndani ya Coastal Union.
Abdalah Shaibu yeye ni beki wa kati alikuwa anakipiga ndani ya MFK Czech ya Serbia.
Kibwana Shomari yeye ni beki wa kulia alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mtibwa Sugar.
Waziri Junior yeye ni mshambuliaji alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Mbao FC.
Nyota hao wote wamesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment