Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

ISHU YA SIMBA KUACHANA NA SVEN, UONGOZI WAWEKA KILA KITU BAYANA

ISHU YA SIMBA KUACHANA NA SVEN, UONGOZI WAWEKA KILA KITU BAYANA

UONGOZI wa Simba umesema kuwa hauna mpango wa kuachana na Kocha Mkuu, Sven Vandenbrocek kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

Hivi karibuni taarifa zilieleza kuwa Sven ndani ya Simba alikuwa amepewa mechi tatu ambazo mbili zilikuwa za ligi na moja ya Kombe la Shirikisho.

Za ligi ilikuwa ni mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania huku ile ya Shirikisho ikiwa ni ya fainali dhidi ya Namungo FC ambao umechezwa jana, Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela na Simba ilishinda kwa mabao 2-1.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa suala la kocha kuachwa ndani ya Simba halipo kwa kuwa hakuan aliyesema jambo hilo la kuachana na kocha.

"Hili jambo sitaki kabisa kuliskia kabisa hakuna ambaye ametangaza kuhusu kuachana na kocha, kocha gani ambaye anaweza kuachana na kikosi cha Simba, hatutaki majungumajungu, suala la kocha hili hakuna kiongozi aliyesema," amesema Manara.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4