MASHABIKI YANGA WAOMBWA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA
MASHABIKI YANGA WAOMBWA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa wana imani na mashabiki na wadau wa timu hiyo hasa katika masuala ya kujitolea kwa ajili ya timu yao hivyo wanaamini watafanikisha bila matatizo.
"Tunawachezaji wa kimataifa wawili ambao tayari tumeshazungumza nao kila kitu, ila tunaomba hawa gharama za usajili zifanywe na mashabiki na wadau ambao wamekuwa nasi kila wakati.
"Uwezo ninajua upo kwa sababu msimu uliopita walisajili wachezaji 10 mashabiki wenyewe ila msimu huu tunaomba waweze kusajili wachezaji wawili tu na utaratibu utatolewa hivi karibuni," amesema.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment