SPOTI XTRA LAGAWA TIKETI ZA KUTOSHA KWA MASHABIKI WA YANGA LEO KWA MKAPA
MAPEMA leo Agosti 30, 2020 Mkuu wa kitengo cha Masoko Global Publishers, Adam Antony ameongoza zoezi la kuwakabidhi tiketi za kuingilia uwanjani kushuhudia sherehe za Kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuiona mechi ya Yanga dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi.
Walikabidhi mashabiki ambao walikutwa wakilisoma gazeti hilo katika viunga vya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mkuu huyo amewataka mashabiki na wasomaji waendelee kujipatia nakala ya gazeti la Spoti Xtra kwa bei ya shilingi 500 pekee na ndani yake kuna habari na uchambuzi wa kitaifa na kimataifa.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment