Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

DC NKASI AMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA KUWAKAMATA WANAFUNZI KISHA KUWAFUNGIA CHUMBA KIMOJA NA NGURUWE

DC NKASI AMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI KWA TUHUMA ZA KUWAKAMATA WANAFUNZI KISHA KUWAFUNGIA CHUMBA KIMOJA NA NGURUWE

 

Mkuu wa Wilaya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Said Mtanda ameagiza kusimamishwa kazi mara moja Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Matala Ndg. Revocatus Tinga  kwa tuhuma za kuwakamata Wanafunzi ambao imeelezwa walikuwa watoro shuleni kisha kuwafungia chumba kimoja na Nguruwe.

Akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Swahila Mkuu huyo wa Wilaya amedai kuwa yeye baada ya kupata taarifa hizo alimuagiza Mkurungenzi Mtendaji wa Wilaya kumsimamisha kazi Mtendaji huyo na kumpeleka Mtendaji mwingine katika Kijiji hicho huku akidai kitendo alichokifanya Afisa Mtendaji huyo hakikubaliki hivyo kwanza asimamishwe kazi na baada ya hapo akabidhiwe kwenye vyombo vya serikali kwa ajili ya uchunguzi.

Mkuu huyo wa wilaya alidai kuwa baada ya uchunguzi huo kukamilika na ikibainika kweli afisa mtendaji huyo amefanya kitendo hicho ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria na mamlaka yake ya nidhamu.

“Ni jambo lisilolokubalika kwa Mtendaji wa Kijiji ambaye ni mlinzi wa amani  katika Kijiji na anafanya kitendo hicho sisi kama serikali ni lazima tuchukue hatua stahiki”-Mh. Mtanda.

Sambamba na hilo aliwataka Wananchi wa eneo hilo kugawa muda wa kufanya kazi zao za kuandaa Mashamba kuelekea msimu mwingine wa Kilimo badala ya kuendekeza masuala ya kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni,kwani wasipoutumia muda huo vizuri msimu wa kilimo utafika na kupita mwisho wa siku ni kukumbwa na balaa la njaa.

Aidha,aliwataka Wananchi kuendelea kulinda amani katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu ili ukifika wakati Watu wenyewe watumie Demokrasia kuwachagua viongozi bora wanaowataka.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4