Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

ISHU YA KUANZA KIKOSI CHA KWANZA KWA NYOTA WA SIMBA IPO HIVI

ISHU YA KUANZA KIKOSI CHA KWANZA KWA NYOTA WA SIMBA IPO HIVI

 


SVEN Vandenbroeck raia wa Ubelgiji ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba, amewapa mchongo wachezaji wake wapya, Bernard Morrison na Larry Bwalya kwa kusema wana nafasi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza.

 

Kocha huyo ameweka wazi kwamba kila mchezaji ambaye yupo kikosini hapo anaweza kuanza katika kikosi cha kwanza endapo tu atapambania nafasi.

 

Mbelgiji huyo ameongeza kwamba, hakuna mchezaji ambaye ana nafasi ya moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kwa sababu huu ni msimu mpya ambapo wamekuja wachezaji wengine wanaohitaji kuwatizama.


Kwa hapa licha ya kwamba kuna wachezaji wengi, kila mmoja ana nafasi ya kucheza na kuanza ndani ya kikosi cha kwanza.


“Hiyo inakuja kwa sababu huu ni msimu mpya na kuna wachezaji wengine tofauti na msimu ulioisha ambao ninahitaji kuwatazama, hivyo kwa yule ambaye atakuwa anapambania nafasi anaweza kucheza.

 

“Kitu kimoja ni kuwa nafurahia namna timu ambayo inaenda kwa sasa na naamini kama tutakuwa hivihivi hadi mwishoni mwa msimu tutakuwa tumefikia mafanikio makubwa,” alimaliza Sven.

 

Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wametua Simba katika msimu huu ni pamoja na Bernard Morrison, Larry Bwalya, Chris Mugalu, Joash Onyango, Ibrahim Ame, Charles Ilanfya na David Kameta ‘Duchu.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4