KAGERA SUGAR V YANGA NI BALAA TUPU, REKODI ZAIGOMEA SARE
LEO Kagera Sugar inawakaribisha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 jioni.
Ni mchezo wa kwanza kwa Yanga nje ya Dar huku kwa Kagera Sugar ukiwa ni wa pili kucheza Uwanja wa Kaitaba.
Rekodi zinaonyesha kuwa ndani ya misimu mitatu ya hivi karibuni, Kagera Sugar na Yanga zikiwa zimekutana mara sita, Kagera Sugar imeshinda mara moja huku wakiwa hawajaambulia sare na Yanga imeshinda mara tano.
Jumla Yanga imefunga mabao 11 huku Kagera Sugar ikifunga mabao sita kati ya mabao 17 ambayo yamefungwa kwa wababe hawa.
Hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa rekodi zinaonyesha kwamba kupatikana sare kwa timu hizi mbili kwa misimu ya hivi karibuni imekuwa ni ngumu.
Misimu mitatu nyuma matokeo ya Kagera Sugar v Yanga matoke yapo namna hii:-
2019/20
Kagera Sugar 0-1 Yanga
Yanga 0-3 Kagera Sugar
2018/19
Yanga 3-0 Kagera Sugar
Kagera Sugar 1-2 Yanga
2017/17
Yanga 3-0 Kagera Sugar
Kagera Sugar 1-2 Yanga.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment