KMC KAMILI GADO KUIVAA MWADUI FC LEO
Kikosi cha Timu ya ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimejiandaa vilivyo katika kukabiliana na mchezo wake wa leo dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Mwadui Complex Mkoani humo.
Kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Mkoani humo jana kimefanya mazoezi katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga ikiwa ni katika hatua za mwisho kabla ya kuelekea kwa mchezo huo ambao KMC FC itakuwa mgeni dhidi ya Mwadui FC.
Katika kikosi hicho hali ya wachezaji ni nzuri na kwamba hakuna majeruhi ambaye anaweza kukosa mchezo huo ambao KMC imejipanga kuhakikisha kwamba inapata ushindi wa alama tatu kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi kuu inayoendelea hapa Nchini.
Imetolewa leo Septemba 20 na
Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC.
Leave Comments
Post a Comment