Ads Right Header

Buy template blogger

MANCHESTER CITY YAIBAMIZA WOLVES NA KUSEPA NA POINTI TATU

MANCHESTER CITY YAIBAMIZA WOLVES NA KUSEPA NA POINTI TATU

 KELVIN De Bruyne nyota wa Manchester City aligungua pazia la ushindi wakati timu yake ikishinda mabao 3-1 mbele ya Wolves kwenye mchezo wa Ligi Kuu England England uliochezwa usiku wa kuamkia leo dakika ya 20 kwa mkwaju wa penalti.

Mabao mengine yalifungwa na Phili Foden dakika ya 32 kisha Wolves walipata bao la kufutia machozi dakika ya 78 kupitia kwa Raul Jimenez na msumari wa mwisho wa Manchester City ukipachikwa kimiani na Gabriel Jesus dakika ya 90.

Manchester City inayonolewa na Kocha Mkuu, Pep Guardiola ilionekana kuwa bora kwenye mchezo huo licha ya kuwa ugenini Uwanja wa Molineux kwa kuwa ilimiliki mpira asilimia 66 huku wapinzani wao wakimiliki asilimia 34.

Guardiola amesema kuwa timu ilikuwa tayari na ilianza vizuri kipindi cha kwanza jambo lilowapa matokeo mazuri kwenye mchezo wao.


Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4