SIMBA INA HESABU ZA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA WAARABU
SIMBA INA HESABU ZA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA WAARABU
UONGOZI wa Simba umesema kuwa una mpango wa kucheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Al Ahly ya nchini Misri kwa siku za hivi karibuni ili kuongeza mahusiano mazuri zaidi kwenye masuala ya michezo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alitembelea makao makuu ya Klabu ya Al Ahly ya Misi na kufanya ziara kwa ajili ya kujifunza zaidi.
Akiwa huko aliongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi waliweza kutembelea makao makuu ya Klabu ya Al Ahly yaliyopo jijini Cairo, Misri na kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo ya biashara, ufundi na uendelezaji wa wachezaji kwa kujenga kituo cha kukuza vipaji kwa ushirikiano na timu ya Al Ahly ikiwa ni kituo cha kwanza nje ya Misri (barani ya Afrika) ambacho kitaendeshwa na Simba na klabu hiyo.
Pia wamekubaliana hapo baadaye timu hiyo kuja nchini kucheza mchezo wa kirafiki na Simba SC.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment