Ads Right Header

Buy template blogger

MAVUNDE AAHIDI KUMALIZA CHANGAMOTO YA AFYA KATA YA HOMBOLO, 'TUTAJENGA SHULE NYINGINE YA SEKONDARI'

MAVUNDE AAHIDI KUMALIZA CHANGAMOTO YA AFYA KATA YA HOMBOLO, 'TUTAJENGA SHULE NYINGINE YA SEKONDARI'

 MAVUNDE AAHIDI KUMALIZA CHANGAMOTO YA AFYA KATA YA HOMBOLO, 'TUTAJENGA SHULE NYINGINE YA SEKONDARI'


Charles James, Michuzi TV

NIKO tayari kuwatumikia! Ndio kauli aliyosema Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Anthony Mavunde wakati alipokua akiomba kura katika kata ya Hombolo ambapo ameahidi kumaliza changamoto yao ya Maji.

Akizungumza katika mkutano wake na wananchi wa kata hiyo, Mavunde amemuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, yeye mwenyewe pamoja na mgombea wa Udiwani wa kata hiyo ili wapate kura nyingi Oktoba 28 waweze kuwaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo na Jiji la Dodoma kwa ujumla.

Mavunde amesema kwa kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Dk Magufuli ameiweka Tanzania kwenye ramani kwa kurudisha nidhamu serikalini, kumaliza kero ya maji, umeme, kuleta elimu bure pamoja na kulinda rasilimali za watanzania.

Amesema Jiji la Dodoma peke yake limenufaika kwa kiasi kikubwa na Dk Magufuli kwa kupata miradi mbalimbali mikubwa ambayo imekua chachu ya kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kuongeza ajira kwenye Jiji hilo.

" Dk Magufuli ametuletea stendi ya mabasi kubwa kuliko zote Afrika Mashariki yenye uwezo wa kuingiza magari 600 kwa wakati mmoja, soko kubwa la kisasa la Job Ndugai, tutajengewa uwanja wa mpira mkubwa kuliko wote Afrika Mashariki utakaobeba watu 80,000 tunataka nini tena?

Siyo hivyo anatuletea treni ya ndani itakayokua ikibeba abiria kama hiyo haitoshi anatuletea treni ya mwendokasi hadi Dar es Salaam kwa masaa matatu tu yaani hata ukiwa na mgonjwa Muhimbili unaweza kumpelekea uji kutokea Dodoma," Amesema Mavunde.

Amesema kata ya Hombolo peke yake ndani ya miaka yake mitano chini ya Dk Magufuli wamepatiwa mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya Sh Milioni 900 pamoja na kituo cha afya na kuomba wananchi hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 kutoa kura za heshima kwa Magufuli.

Mavunde ameahidi kumaliza changamoto ya watoa huduma za afya kwenye kituo cha afya cha Hombolo pamoja na kufanya maboresho kwenye majengo na kuleta vifaa mbalimbali vinavyohitajika kituoni hapo ili kumaliza adha inayowakabili wananchi wa Hombolo kwenye afya.

" Kwenye elimu nafahamu changamoto inayowakabili watoto wetu wanaotoka Mkoyo kuja Hombolo Sekondari umbali ni mrefu na unaleta vishawishi kwao kiasi cha wengine kupata mimba, niwaahidi mkinichagua tutashirikiana kujenga shule ya sekondari Mkoyo ili watoto wetu wasitembee umbali mrefu.

Hombolo tuna bwawa kubwa na lenye maji mengi kuliko yote Dodoma ni lazima tulifanye kuwa fursa kwetu ya kitalii, tutashirikiana katika kulitengeneza na kuweka mazingira mazuri ya watu kuja kupumzika huku na kutalii, hii itachochea maendeleo ya kata yetu na kukuza uchumi wa wananchi mmoja mmoja pia," Amesema Mavunde

 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kata ya Hombolo Bwawani waliojitokeza kusikiliza Sera zake kwenye muendelezo wa kampeni zake Jimboni kwake.

 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Meja Mstaafu Risasi (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na Diwani wa Kata ya Hombolo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde akiomba kura za mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, za kwake mwenyewe na za mgombea Udiwani wa Kata ya Hombolo. 

Wananchi mbalimbali ambao  walijitokeza kwenye kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde katika kata ya Hombolo Bwawani.

Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile ameshiriki kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na kuomba kura za Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo hilo, Anthony Mavunde na Diwani wa Kata ya Hombolo.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4