Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MBUNGE MTEULE LUDEWA AENDELEA NA HARAKATI ZA KUSAKA KURA ZA MGOMBEA URAIS MAGUFULI

MBUNGE MTEULE LUDEWA AENDELEA NA HARAKATI ZA KUSAKA KURA ZA MGOMBEA URAIS MAGUFULI

 Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga ameendelea na harakati zake za kupita vijijini kwa ajili ya kumuombea kura rais in John Pombe Magufuli.

Sambamba na kumuombea kura rais Magufuli pia amekuwa akisikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi na kujua vipaumbele vyao katika maendeleo.

Akizungumza katika Kijiji cha Madope kilichopo katika kata ya Madope mbunge huyo amesema anataka kujua vipaumbele vya wananchi ili aweze kutimiza malengo yao.

"Kiongozi bora ni yule anayesikiliza zaidi kuliko anayeongea, siwezi kuja na mipango yangu ya maendeleo yenu inaweza isiwe msaada kwenu kwa wakati huo hivyo napenda nisikie kutoka kwenu", Alisema Kamonga.

Alisema kuwa ni vyema kusikia kutoka kwao maana wao ndio wanaojua uzito wa changamoto zao.

Aidha kwa upande wa wanakijiji hao wamezungumzia changamoto za bara bara zinazounganisha kata hadi kata, ulanguzi wa bei katika mazao mbalimbali pamoja na changamoto ya maji.

Baada ya kuambiwa changamoto hizo aliwaahidi kuzishughulikia Pindi atakapoanza kazi rasmi.

Mbunge huyo akiwa na ratiba ya kutembelea vijiji vitatu kwa siku ambapo mpaka Sasa tayari kashatembelea vijiji 24.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akijumuika kupata chakula na vibarua wa ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege walichokiandaa kwa mlo wa mchana.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akisaidiana na diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu kusawazisha zege lililomwagwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akisalimiana na baadhi ya wananchi wakifika kwenye mkutano huo
Madiwani wa kata mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.  Kutoka kushoto ni diwani mteule viti maalum Leah Mbilinyi, Leodgar Mpambalioto diwani mteule kata ya Mawengi, Edga mtitu diwani mteule kata ya Lubonde na Patrick Mgaya diwani wa kata ya Madope.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiwa na diwani mteule wa kata ya Lubonde wakiangalia usukwaji wa nondo zilizotandazwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege.
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga (mwenye kofia nyeusi kushoto) akiwa sambamba na Diwani mteule wa kata ya Lubonde Edga mtitu wakisaidia kusambaza zege katikati barabara ya kiwango cha zege inayojengwa kwa km. 50 kutoka Lusitu hadi Mawengi
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiwa kwenye picha ya pamoja na mabalozi wa kijiji cha kivuyo
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga(aliyeshika bendera) akiwa akiselebuka huku akiwa amezungukwa na wananchi
 Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa Joseph Kamonga akiwavalisha vitambulisho mabalozi wa kijiji cha kivuyo

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4