RC KILIMANJARO AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA WANAWAKE WAJASILIAMALI JIJINI ARUSHA LEO
Woinde Shizza,Michuzi TV Arusha
Mkuu wa Mkoa WA Kilimanjaro Mama Anna Mghwira amefungua Kongamano kubwa la kimataifa la Wanawake ambao ni wajasiria Mali na wamiliki wa Biashara mbali mbali kutoka nchi za barani ulaya na Africa mashariki
Akizungumza na Wanawake hao waliojitokeza katika Kongamano hilo Mghwira amewaomba Wanawake kujiongezea mitaji mikubwa pamoja na kupambania fursa za uwekezaji katika Biashara zao kwani Wanawake wamekuwa na mchango Mkubwa katika kuimarisha uchumi wa familia na nchi Kwa ujumla
Alisema Wanawake wanapaswa kuendelea kupambana katika kujimarisha katika Masoko ya Nje Kwa lengo la kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa Nje kwani Kazi nyingi zinazo zalishwa nchini zina ubora wa kiwango cha kuuza Nje
Kwa upande wake Bi Gladiness Katega ambaye ni Mratibu wa Kongamano hilo alisema kwamba lengo la kuwakutanisha Wanawake hao ni kujijengea uwezo pamoja na kutambua fursa za kufanya biasha Ndani na Nje ya nchi kwani Biashara za Wanawake ziliyumbishwa na ugonjwa wa corona
Alisema Kongamano hilo limelenga kuwapasha Wanawake namna ya kupambana na Biashara kimataifa na kitaifa na kufikia malengo ya kukuza uchumi Kwa bidhaa wanazo zalisha na kuleta Maendeleo katika familia zao
Baadhi wa washiriki wakiongelea Kongamano hilo na namna watakavyo nufaika wameleza kufuraishwa sana na wanategemea kupata mafunzo yatakayo wasaidia kusonga mbele katika Biashara zao na kufikia Masoko makubwa ya Nje hasa kutumia mitandao
Mkuu wa mkoa.wa Kilimanjaro akiangalia baadhi ya bidhaa zilizoletwa kuonyeshwa na wanawake katika kongamano hilo
Mkuu wa Mkoa WA Kilimanjaro Mama Anna Mghwira akifungua Kongamano kubwa la kimataifa la wanawake lililoanza Leo katika hotel ya Mount Meru
Baadhi ya wanawake kutoka nchi za barani ulaya na Africa mashariki wakiwa katika picha ya Pamoja na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mara baada ya kufungua kongamano la Wafanya biashara wanawake
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment