Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMBA YAPIGA 4G JKT TANZANIA, JAMHURI

SIMBA YAPIGA 4G JKT TANZANIA, JAMHURI

 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, leo Oktoba 4 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mabao ya Simba yalifungwa na  Meddie Kagere aliyefunga mabao mawili dakika ya 4  na dakika ya 40 na mabao mengine yalifungwa na Chris Mugalu dakika ya 6 na Luis Miquissone  naye alitupia bao dakika ya 51. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 13 ikiwa nafasi ya kwanza na ina mabao 14 kibindoni huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Yanga yenye pointi 13 tofauti kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. 

Yanga imefunga jumla ya mabao 7 kibindoni na ushindi wa jana, Oktoba 3 ulikuwa ni wa kwanza kwa Yanga kushinda mabao zaidi ya mabao 3 uwanjani.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4