Tamasha la muziki la Marafiki kukutanisha wadau wa Muziki
Vikundi 13 vya wananumiziki wa Tanzania na mmoja wa Kenya vitatumbuiza kwenye tamasha la kwanza la muziki liitwalo Marafiki litakalofanyika kwa siku tatu sehemu mbili tofauti ikiwemo Dar Es Salaam na Bagamoyo.
Mkurugenzi wa Tamasha hilo Isack Abeneko amesema tamasha hilo lifanyika kuanzaio tarehe 8-10 mwezi huu.
Tamasha hilo lenye kauli mbiu Utamaduni ni ngao ya Taifa litafanyika Slow Leopord Masaki kwa tarehe 8 na 9 na kwa tarehe 10 tamasha litakua Bagamoyo Firefly kwa viingilio vya Sh10,000 tu. Tamasha litaanza saa 1 jioni mpaka saa sita usiku kila siku.
“Huu ni msimu wa kwanza wa Tamasha linalongenga kuleta fursa zaidi kwenye shughuli za kimaendeleo ya jamii kupitia jukwaa la muziki mubashara.Wazo la tamasha hili liluizaliwa kutoka kwa tukio la Marafiki Night Live ambalo hifanyika mara moja kwa mwezi kuazia mwezi October 2018.
Tukio hili huleta marafiki na wadau wa muziki kufurahia muziki kwa pamoja. Kupitia jukwaa la Marafiki Night Live tukaona kuna umuhimu wa kuanzisha tamasha hili ambalo litatoa fursa zaidi kwa wadau wa muziki kupata nafasi ya kuonyesha kazi zao na engine kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wenzao,”amesema Abeneko.
Abeneko amewataja wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Wamwiduka Band , Ze Spirits Band, DDC Mlimani Park – Sikinde, Abeneko & Positive mind, Rich Lumambo, Malfred, Siti & The band (Zanzibar), Afro Simba Band (Kenya), Upendo Manase, Shabo Makota, Msafiri Zawose, Baba Kash na Tamimu.
“Utofauti wa tamasha la Marafiki na matamasha mengine ni namna tamasha lilivyoanza kwa kuunganishwa na urafiki ndani ya tasnia yua muziki na sasa tamasha linaanza kwa kuleta pamoja marafiki wa muziki na wanamuziki pamoja waungane kwa kupitia muziki na kupata fursa ya kushiriki tamaduni mbalimbali kupitia muziki,” amesema Abeneko.
Shaban Mugado Meneja wa Tamasha amesema, ASEDEVA kwa kushirikiana na Weka Music Records wameandaa tamasha hilo ambalo mbali na burudani ya muziki tamasha litaambatana na warsha zitakazosaidia wadau wa muziki kukuza uelewa wao kupitia mada zitakazotolewa wakati wa tamasha hilo la siku tatu.
“Tamasha litakua na mada mbalimbali kwenye warsha ambazo zitawasaidia wasanii kuongeza thamani kwenye kazi zao za kimuziki ili kukuza sanaa ya muziki pamoja na kuwajengea uwezo. Tutajadili biashara ya muziki, usimamizi binafsi wa mwanamuziki na hata baada ya kupata meneja, namna ya kupata nafasi za maoneysho ya Kimataifa na Uhandisi wa sauti. Tarehe 8 na 9 mwezi huu kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 730 mchana warsha zitafanyika Nafasi Art Space Mikocheni,” amesema Mugado.
Mugado amewashukuru wadhamini wa Tamasha ambao ni Goethe-Institut Tanzania, Firefly Bagamoyo, The Slow Leopard Bar & Restaurant, Jameson, Busara promotion, Boresha Radio, Acto Light, Nafasi Art Space, EM media, Ruka Company, Basata na Eyecue Media Solution.
Leave Comments
Post a Comment