Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 01 & 02 (Return Of Olivia Hitler)


Furaha na amani, vinazidi kuendelea kutawala familia ya bwana Eddy pamoja na mke wake Rahma. Uzuri wa watoto wao ambao kwa sasa wametimia miaka kumi na nane tangu watoke tumboni mwa mama yao mzazi, unaendelea kuchukua twasira mpya kwenye jamii. Kwani mara kadhaa wazamini wa mashindano ya urembo mkoani Tanga, wanapeleka maombi yao mara kwa mara kwa wazazi wa Xaviela na Xaviena, ili waweze kushiriki mashindano ya ulimbwende kumtafuta mrembo wa jiji la Tanga atakaye wakilisha mkoa katika kuwania taji la urembo wa Tanzania na taji la dunia.
"Baba Xaviena hivi unauhakika kweli na hao watu, wanao wataka kina Xaviena wakashiriki huo udubwasha wao?"
Ni sauti ya Rahma akizungumza humu macho yake akimtazama mumewe anaye jikuna kichwa akifikiria jibu la kuwapa wazee saba wanao husika katika maswala ya kuandaa mashindano ya urembo, wanao wasubiria sebleni.
"Hivi hao wanao wewe unawaonaje onaje?"
"Sijakuelewa swali lako mume wangu?"
"Namaanisha wataweza kushiriki hayo mashindano?"
"Sasa Eddy mume wangu, Xaviena kidogo ninaona ndio anavutiwa na hayo mambo ya urembo. Ila Xavila mmmmm sidhani kama ana hata mpango wa kuwa miss."
"Wenyewe wapo wapi?"
"Ndani kwao"
"Wapigie simu waje"
Kutokana na ukubwa wa jumba wanalo ishi Eddy na mke wake, ilimlazimu Rahma kumpigia simu Xaviena, akawaomba waingie kwenye chumba cha kusomea ambapo wapo wazazi wao
Haukupita muda sana Xaviela na Xaviena wakaingia kwenye chumba cha kusomea na kuwakuta wazazi wao wakiwasubiri kwa hamo.
"Wale wazee wamekuja tena?"
Xaviela aliuliza huku akiwatazama wazazi wake.
"Ndio kwani vipi?"
Eddy alijibu huku akirudisha swali kwa mwanaye huyo.
"Lakini dady, hao wazee si uliwakataza wasije?"
"Ndio niliwakataza wasije, kipindi kile mulikuwa mupo shule sasa kipindi hichi munacho subiria matokeo yenu ya mtihani, nimeona niwashirilishe hili jambo"
"Jambo gani baba?"
Xaviena aliuliza kwa upole huku akimtazama baba yake usoni. Eddy akawaelezea watoto wake dhamira ya wazee hao kufika hapo nyumbani kwao mara kwa mara, hadi anamaliza kuzungumza sura ya Xaviena ikawa imechanua kwa tabasamu pana, akifurahia ombi la wazee hao, kwani ni moja ya ndoto zake kuwa mrembo japo hata kwa mtaa anao ishi yeye. Hali ni tofauti kwa Xaviela asiye penda hata kusikia neno urembo, muda wake mwingi anautumia katika kufanya mazoezi ya viungo na kutazama filamu za mapigano.
"Baba na mama, mimi sina muda huo wa kwenda kwenye mashindano hayo ya kipuuzi"
Xaviela alizungumza, akafungua mlango na kuondoka, jambo lililo mfanya Rahma kufungua mlango na kwenda anapo kwenda mtoto wake huyo wa kike, anaye mpenda kupita maelezo.
"Eheee na wewe vipi, jibu ni kama la huyo mwenzio?"
"Hapana baba, mimi nipo tayari kwa hilo"
"Kweli?"
"Kweli Dady"
"Haya usije ukenda kutuaibisha kama unavyo fahamu baba yako ninagombania ubunge uchaguzi unao kuja, itakuwa jambo la kushangaza mtoto wa mbunge akishindwa"
"Mmm jamani dady ngoja nikuonyeshe wanavyo tembea mamiss"
Xaviena akaanza kutembea mbele ya baba yake, huku mara kadhaa akigeuka kwa mapozi kama wanavyo fanya warembo wanao gombabia mataji mbali mbali duniani.
"Amekufundisha nani hivyo?"
"Mimi mwenyewe huwa napenda kutazana mashindano ya urembo"
"Kwahiyo nikawajibu upo tayari"
"Ndio baba"
"Haya"
Eddy akatoka katika chumba alichokuwa na Xaviena na kwenda katika sebule alipo waacha wazee hao
"Jamani samahini kwa kuwaweka sana"
"Hakuna shida ni jukumu letu hilo"
"Bwana nimezungumza na mabinti wangu. Mmoja amekubali ila mmoja amekataa"
"Sawa, hata buyo mmoja anatutosha kwa maana tunatana kusimamisha mrembo ambaye ataliletea sifa jiji letu la Tanga na mkoa mzima"
"Sawa na hao wengine mulio wapitisha mashindano vipi nao?" Eddy sliuliza
"Ahaass hao gelesha tuu, kwani mshindi halisi sisi tunaye ambaye atakuwa ni mwanao"
"Ahaaaa sawa, ila jamani hala hala na mwanangu, kwenye hayo mashindano yenu ninasikia kuna mambo ya kifuska, sinto jisikia vizuri siku mwanangu atakapo fanyiwa upuuzi bado ni mwanafunzi huyo"
"Hilo mkuu wala usiwe na shaka nalo nwanao yupo katika mikono salama kabisa"
"Nyinyi semeni hivyo siku nije kusikia ujinga nitawachinja"
Eddy alizungumza kwa kujiamini, huku akiwatazama machoni wazee hao, walio anza kutazanana wenyewe kwa wenyewe kwani wanamfahamu Eddy ni miongoni mwa matajiri wakubwa mkoani Tanga pamoja na nchini Tanzania.
"Mimi kama mkurugenzi wa mashindano hayo wala sinto kuangusha muheshimiwa mbunge mtarajiwa"
Hawakuwa na lakuzungumza zaidi ya kuaga na kuondoka zao.
***
Kuingia kwa Xaviena siku ya kwanza katika kambi ya warembo, iliyopo katika hoteli ya kitalii Tanga beach reasort, ikaanza kuzuka woga kwa baadhi ya warembo wengine walio ingia katika kambi hiyo siku mbili za nyuma. Uzuri wa Xaviena, umechangiwa na urefu wake, wa futi sita na nchi kadha. Rangi ya chocolate isiyo kolea sana, inazidi kuufanya uzuri wake kuzidi kuongezeka mara dufu.
Sifa zake za uzuri wake ukizilinganisha na warembo wengine waliopo katika kambi hii, ni sawa sawa kulilinganisha ardhi na mbingu, kwani hakuna mrembo anaye mfikia hata kwa asilimia kumi.
"Habari zenu?"
Xaviena akawasalimia warembo wezake wapatao ishirini na tatu, baadhi walimuitilia salamu yake ila wengine wakabaki wakiibenua midomo yao kwa dharau iliyo jaa wivu ndani yake
"Jamani huyu ni mwenzenu atajumuika nasi katika kipindi chote cha kukaa hapa kambini"
Mlezi wao(matroni) alizungumza, akimtambulisha Xaviena mbele yao
"Kwa jina anaitwa Xaviena Eddy, ninaomba tumpe ushirikiano wetu"
"Sawa matroni"
Kutokana ni jioni, warembo wote ukawa ni muda wa wao kuzunguka maeneo mbali mbali ya Hoteli, kuzipumzisha akili zao kwa ajili ya siku inayo fwata.
"Jamani mimi kuna kitu kinaniumiza kichwa"
Msichana mmoja alizungumza akiwa amesimama katilati ya kundi la wezake wapatao wanne
"Jambo gani hilo?"
"Hivi huyu demu aliye kuja ametokea wapi kwa maana hapa sisi kila mmoja ameingia akitokea kwenye kitongoji chake ila huyu mwenzetu hatujui jatoka wapi?"
"Shosti nilidhani ni mimi peke yangu niliye dhani hilo"
"Hawa ndio wale wanao chochomekwa, sasa huyu dawa yake nimesha ijua"
"Unata kumfanya nini?"
"Ngoja usiku ufike nitawaonyesha cha kumfanya. Atajuta kuja hapa atanitambua kwamba ni Asha binti Adalah kutoka Pangani"
Muda wa kulala ukawadia warembo wote akiwemo Xaviena wakaingia katika vyumba vyao vya kupumzikia, na kila chumba kina vitanda viwili vinavyo laliwana na warembo wawili wawili. Kutokana Xaviena amechelewa kuingi kambini ikamlazimu kulala chumba cha kwake peke yake. Mipango ya Asha na wezake katika kutafuta chokocho dhidi ya Xaviena ikakwama kwa usiku huu wa leo, wani hawakutambua ni wapi alipi lala Xaviena.
***
Siku ziku zidi kwenda, warembo wakiendelea kupewa mafunzo mbalimbali kwenye kambi yao, huku kila mmoja akizidi kujijengea matumaini moyoni mwake kwamba anaweza kunyakua taji hilo la urembo wa mkoa wa Tanga. Kitu kilicho washangaza baadhi ya wa rembo akiwemo Asha, ni jinsi ya Xaviena alivyo jaliwa kutambua mambo mengi juu ya urembo. Uwezo wake wa kuyatambua mambo mengi mara kadhaa, ilimzimu mwalimu wao kumuachia darasa Xaviena ili awafundishe wezake. Ukweli ni kwamba baadhi ya washiriki wakaanza kumpatia ushindi Xaviena hata kabla ya mashindano. Ila ipo tofauti kwa Asha na kundi lake la watu watano, ambao wamejipa jina la Team KISHKWAMBI, wakionyesha kuzipeleka nguvu zao zote kwa Asha, ambaye kwa upande wake anajivunia kuwa na asili ya bara la Asia japo amezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania.
"Asha, unakosea kitu kimoja unapo takiwa kutembea usiiachie mikono kama imevunjika, kidogo unatakiwa kuikaza ili...."
Asha hakumpa nafasi Xaviena kuimalizia sentensi yake, akaachia msunyo mkali ulio wafanya wezake wote kukaa kimya wakimtaza kusubiria atazungumza kitu gani.
"Kwanza unanifundisha wewe kama nani?"
"No, mwalimi si ameniachia darasa ni jukumu langu kukuelekeza kama mshiriki mwenzangu"
"Heeee makubwa, wewe ni wakunielekaza mimi?"
Asha alizungum huku akimpandisha kwa macho makali Xaviena kuanzia juu hadi chini.
"Hembu jifananishe wewe mwenyewe. Hunahadhi ya kunifundisha mimi."
Asha aliendelea kumtolea maneno ya dharau Xaviena ambaye muda wote macho yake makubwa kiasi yana kazi ya kumtazama Asha jinsi anavyo jichetua mbele yake.
"Basi nisamehe mimi, ninakuomba ukakae kwenye kiti"
"Siendi kukaa"
Asha alizungumza huku mikono yake ikiwa imeshika kiuno chake chembaba kiasi.
"Asma mbona unakuwa mjeuri wewe, mwenzako si anakuambia uje huku kukaa"
Mrembo mmona alizungumza kwa sauti ya upole akimuomba Asha kurudi kukaa kwenhe viti walivyo kalia wao
"Babueee hayakuhusu na wewe, si uwaache wenyewe wamalizane"
Mmoja wa wapambe kwenye kundi la kishkwambi alizungumza kwa sauti ya ukali, iliyo mfanya mrembo aliye jaribu kufungua kinywa chake kukaa kimya asizungumze kitu cha aina yoyote.
"Wewe kunguni uiliye kosa kunyonya damu ya mbwa umekuja kunyonya damu ya binadamu leo utanitambua."
Asha alizungumza huku akimsukuma Xaviena aliye pepesuka kidogo, na kuanguka chini. Bila ya kupoteza muda, Asha akamrukia Xaviena. Akamkalia tumboni na kuanza kumtandika vibao mfululizo vya mashavuni. Warembo walio upande wa Xaviena hawakusita kunyanyuka kwenye viti vyao na kuwatenganisha Xaviena na Asha. Machozi ya uchungu yakaanza kumtiririka Xaviena usoni mwake, kwani hadi sasa hivi hatambui ni sababu gani inayo mfanya Asha pamoja na kundi lake kumchukia sana.
Xaviena hakuona haja ya kuendelea kukaa katika fukwe ya bahari wanapo fanyia mazoezi kila asubuhi na jiono. Kwa mwendo wa haraka huku akijiziba sura yake inayo endelea kutiririkwa na machozi akondoka eneo hilo.
Gafla akastukia mkono wake ukishikwa kwa pembeni, akamtazama mtu aliye mshika mkono
"Unalia nini wewe?"
Sauti ya Xaviela ilizungumza, huku akimtazama mdogo wake Xaviena
"Hapana"
"Hapana nini wakati unalia?"
Xaviela alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo, akiendelea kumtazama Xaviena aliye chafuka mwili mzima kwa micha aliyo mwagiwa na Asha. Siku zote za maisha yao Xaviela hapend kumuona pacha wake huyu akionewa na mtu wa aina yoyote, na endapo itatokea hivyo nilazima afanye kitu chochote dhidi ya kuumupa furaha mdogo wake.
"Sema nani kakupiga?"
Xaviela alizungumza huku akiyageuza geuza mashavu ya Xaviena, yaliyo jichora alama za vidole
"Ni yule dada aliye vaa kibukta cheupe na sidiria nyekundu"
"Ahaaa twende"
Xaviela akamshika mkono Xaviena, wakelekea katika eneo walipo warembo wengine, kila aliye muona Xaviela na Xaviena akabaki akiwa amejawa na mshangao mkubwa sana. Kwani wana fanana sana na wote ni warembo kuliko hata wao.
"Wewe nguruwe ndio uliye mpiga mdogo wangu?"
Xaviela alizungumza huku akifyatua teke kali lililo ichota kiguu yote ya Asha na kumuangusha chini kama gunia. Xaviela akamshika Asha nywele zake, akamnyanyua juu, hadi akasimama wima kama mlingoti.
"Wewe unamjua huyo ni nani?"
Xàviela alizungumza hukua akiendelea kuzishikilia nywele za Asha. Rafiki mmoja wa Asha akajaribu kumshika Xaviela mkono wake wa kulia ili asiendelee kumshika mkuu wao. Ngumi nzito ikatua kwenye pua ya msichana huyo na kumfanya mrembo huyo kutoa ukelele mkali wa maumivu ulio ambatana na matone ya damu yaliyo anza kumchuruzika puani mwake. Xaviela akamtandika kichwa kizito Asha, akimsindikiza na kofi zito lililo muangusha Asha chini kwa mara ya pili.
"Sikiliza wewe mpumbavu, usirudie ziku nyingune kumgusa mdogo wangu, hii ni mboni ya jicho langu akilia yeye ni sawa sawa nimeli mimi, siku ukirudia kufanya ulicho mfanyia, nitakuua."
Xaviela alizungumza huku akiwa amemuinamia Asma, anaye ona mawenge mawenge kwenye macho yake kwani kichwa hicho kimekata network zote za kujitambua kichwani mwake.
"Kama kuna mtu kati yenu alikuwà anajidanganya kumdhururu mdogu wangu, atambue atadili na mimi kwa marefu, twende zetu Xaviena."
Xaviela akaanza kuondoka na Xaviena akifwatia kwa nyuma. Wakawaacha warembo wakinong'onezana kwani hawakutamba kwamba Xaviena ana pacha mwenzake ambaye ni mkorofi kupita maelezo. Wapambe wa Asha walio salia wakawa na kazi ya kuwainua wezao walio jeruhiwa kwa kipigo hicho.
"Matroni akija lazima niseme"
Asha alizungumza huku akiendelea kulia, jambo lililo wafanya warembo wengine kuanza kumcheka kwa dharua.
"Heeee hee leo timu Kishkwambi, kwisha habari yake, chezea pacha wewe"
Mrembo mmoja alizungumza huku akicheka kicheko kilicho wakasirisha Asha na timu yake nzima.


TANGA RAHA 02

Xaviena akamaliza kuoga, na kuvaa nguo nyingine, na kuelekea katika sehemu ya mapumzikio anapo subiriwa na Xaviela.
"Hivi haya ndio maisha unayo ishi humu na hao wezako?"
"Hapana ni leo tu ndio yule dada, aliamua kunifanyia hivyo"
"Na wewe ukakubali kupigwa kirahisi rahisi tu?"
Xaviena akakaa kimya kutokana yeye si mgomvi, na hapendelei kugombana na mtu, hii nikutoka na upole wake.
"Ok, tuachane na hayo. Baba na mama wemenituma nije kukutembelea nijue unaishije humu"
"Mimi nipo sawa, ila ninaomba usiende kumuambia mama hili swala la mimi kupigwa"
"Sinto muambia ila kuwa makini, kama mambo yenyewe ndio hayo wala hamna haja ya wewe kuendelea kushiriki huo ujinga"
"Xaviela huu si ujinga, kwani ni kitu ninacho kipenda kutoma moyoni mwangu. Ni sawa sawa na wewe unavyo penda kucheza michezo ya kareti, kwani mwanzoni si ulikua na wewe unapigwa"
"Nimekuelewa, kwanza yule demu anaitwa nini?"
"Yupi?"
"Humjui, yule aliye kupiga?"
"Anaitwa Asha"
"Powa nitamfwatilia, ila endapo itatokea amekuanza tena, nipigie simu nije kumshikisha adabu"
"Sawa nimekuelewa"
Xaviela na Xaviena wakaeleka kwenye maegesho ya magari, wakaagana kisha Xaviela akaingia kwenye gari lake aina ya 'Landrover discove' na kuondoka zake na Xaviena akabaki katika eneo hili la hoteli.
Haikuwa ni siku ya furaha kwa Xaviena ambaye emethihiririshiwa na Asha kwamba anamchukia kutoka rohoni, akaamua kutafuta sehemu iliyo tulia kwenye moja ya kibanda chenye nguzo moja iliyonezekwa juu kwa kutumia makuti.
"Kwa nini jamani wananichukia mimi, kosa langu lipo wapi?"
Alijisemea kwa sauti ya chini huku akimwagikwa na machozi
"Binti usilie"
Sauti ya mwanamke ilisikia kutoka nyum ya kiti alicho kaa Xaviena, ikamlazimu kugeuka na kumtazama mwanamke anaye msemesha, nisura ngeni kwake kwani hakuwahi kumuona mwanamke huyu, mrefu aliye valia gauni refu jekundu pamoja na miwani kubwa iliyo yaziba macho yake.
"Ninaweza kukaa?"
"Mmmmmm yaa unaweza kukaa”
Xaviena alijibu hukuba akijipangusa machozi yake kwa viganja vyake vilaini, mwanadada huyo akavuta kiti kilichopo mbele ya Xaviena na kukaa, taratibu akaivua miwani yake nyeusi na kuziweka nywele zake ndefu vizuri na kumtazama Xaviena kwa umakini, akaachia tabasamu pana na kumpa mkono Xaviena
"Mimi ninaitwa Olivia Hitler wewe je unaitwa nani?"
Macho ya Xaviena yakamtazama Olvia aliye jitambulisha mbele yake huku akiwa amemuelekezea mkono wake, akiashiria waikutanishe mikono yao pamoja kwa ajili ya kusalimiana. Xaviena akaunyanyua mkono wake taratibu na kumkabidhi Olvia ambaye muda wote amemtumbulia macho malegevu yaliyo jaa upendo ndani yake, huku sura ya Olivia ikipambwa na tabasamu pana.
“Mimi ninaitwa Xaviena”
“Waoo jina lako ni zuri sana”
“Asante”
“Baba yako na mama yako wanaendeleaje?”
Swali la Olvia Hitler likamfanya Xaviena kustuka kwani hakutegemea kusikia swali kama hilo kutoka kwa Olvia Hitler. Mstuko wa Xaviena ukamfanya Olvia Hitler kuto kushangaa sana kwani ni moja ya jibu ambalo alikuwa akilitegemea kutoka kwa Xaviena, ambaye bado anaoenekana kumshangaa.
“Nahisi utakuwa umestuka kidogo, kusikia nikimuulizia baba yako pamoja na mama yako, ila maana yangu si mbaya kutokana nimesikia kwamba baba yako anahitaji kugombania Ubunge si ndio?”
Macho ya Xaviena yakamtazama Olvia vizuri machoni mwake, kisha akaachia tabasamu taratibu na kuilazimisha furaha kuwa ndani ya moyo wake, japo usoni mwake bado anamshaka mengi na Olvia Hitler.
“Hawajambo”
“Ahaaaaa, mimi nilipenda kuilijua hilo, ila tuachane na mambo ya wazazi wako. Yule niliye kuona naye kwenye maegesho ya magari, ukimsindikiza ni nani yako?”
“Ahaaa Yule ni pacha wangu anaitwa Xaviela”
“Aiseee munafanana sana, kweli wazazi wenu nina imani wana jivunia kwa kuwa na watoto kama nyinyi”
“Asante”
Olivia Hitler akatoa kikadi kidogo kwenye pochi yake kilicho andikwa namba za simu kisha akamakabidhi Xaviena.
“Ukiwa na tatizo nijulishe kupitia hiyo namba”
“Sawa, ila kwa nini umenipa namba zako, tukiwa hatufamamiani, na nimara ya kwanza kuonana leo?”
Xaviena aliuliza swali huku akimtazama Olvia Hitler aliye anza kusimama kwenye kiti alicho kikalia, akitaka kuondoka katika eneo hilo.
“Ahaa kupeana namba ni jambo la kawaida, isitoshe nina kampuni yangu ya urembo, nimekuona unaweza kunifaaa kwenye baadhi ya matangazo ndio maana nimekupa hiyo namba nikiwa na maana kwamba siku mukimaliza mashindano yanu nikutafute tufanye biashara pamoja”
“Nashukuru kwa ofa yako Olvia”
“Usijali ukikubaliana na mimi, kufanya biashara nitahakikisha utajulikana dunia nzima”
Maneno ya Olvia Hitler yakazidi kumfurahisha Xaviena, aliye na malengo makubwa sana katika maisha yake kupitia swala la urembo, na siku zote malengo yake anahitaji kuwa kama mwanadada, Nansi Sumari, aliye tingisha katika maswala ya urembo miaka kadhaa ya nyuma hapa nchini Tanzania.
“Usijali kila kitu kitakuwa sawa, ila kabla sijasahau ninakuomba usimueleze kitu chochote baba yako kuhusiana na mimi”
“Kwa nini?”
“Nisinge penda wafahamu kuwa sisi ni marafiki, na ninataka niwafanyie kama zawadi ambayo hawajaitegemea kwa miaka mingi iliyo pita kutoka kwangu”
“Sawa ila wewe na baba munafahamiana vipi?”
“Ahaaaa hayo tutazungumza siku tukipata muda mzuri, wa kukaa mimi na wewe”
“Sawa”
Olvia Hitler akasimama na kumpa mkono Xaviena, kisha akaivaa miwani yake na kuondoka taratibu kwa mwendo ulio tawaliwa na mapozi ndani yake. Jambo lililo zidi kuzua maswali mengi ndani ya kichwa cha Xaviena, ni kumuhusisha baba yake kuwa katika mahusiano ya kimapenzi Olvia aliye toka kuzungumza naye muda mchache ulio pita, kwani hatambui ni sababu gani inapelekea Olvia kukataa wazazi wake wasitambue juu ya urafiki wao ambao ndani yake unamaswala ya kibiashara.
“Labda utakuwa ni mchepukoi wake huu kwa maana baba mmmmmmm…..!!!”
Xaviena alizungumza huku akiachia tabasamu usoni mwake, akaondoka katika eneo la kupumzikia na kuelekea katika vyumba vyao vya kulala, huku moyoni mwake akitawaliwa na amani kubwa.
***
Timu Kishkwambi na kiongozi wao Asha, wote wametawaliwa na hofu juu ya Xaviena ambaye siku hadi siku anazidi kutingisha ndani ya kambi hiyo. Uwepo wa Xaviena katika kambi hiyo ikawafanya wakurugenzi wa makampuni mbalimbali, kutia timu katika kampuni inayo aandaa mashindano hayo ya urembo. Baadhi ya wakurugenzi, lengo lao ni kuhakikisha wana daka sihihi ya Xaviena kkatika matangazo ya kampuni zao. Huku wengine wakihitaji kumnasa binti huyo.
Vituo kadhaa vya habari ndani na nje ya jiji la Tanga, wakatia kambi kuhakikisha kwamba wana rekodi juu ya matukio yanayo endelea kwa mabinti hao.
“Xaviena”
Matron alimuita Xaviena mara baada ya kuingia kwenye chumba chake cha kupumzikia.
“Bee”
“Jindae kuna waandishi wa habari ambao wamekuja kukujoji maswali mawwili matatu hivyo jiandae”
“Kwa nini wamekuja usiku?”
“Ndio muda ambao mkurugenzi aliwapangia. Ila hii ni bahati ya kipekee hembu jiandea bwana”
Xaviena akaanza kujiandaa kwa haraka haraka kisha wakaongozanana Matron hadi katika ukumbi wa mikutano katika hoteli hii. Akawakuta waandishi wa habari pamoja na jopo la waandaaji wa shindano hili pamoja na wadhamini walio jitoa kuhakikisha wana dhamini tukio zima la miss Tanga. Xaviena akahojiwa kisha akaonyeshwa sehemu ya kukaa.
Mahojiano yakaanza kwa waandaaji wa shindano kisha wakafwatia wadhamini na baada ya hapo wakahamia kwa Xaviena.
“Je umejiandaaje na mchuano huu?”
“Nimejiandaa vizuri. Hakika ni jambo la kupendeza na la kumshukuru Mungu”
“Je unajipa asilimia ngapi katika swala zima la ushindi?”
“Mmmm hayo nina muachia Mungu pamoja na majaji”
Maswali la Xaviena hayakuwa mengi sana na baada ya hapo mahojiano yakaisha kisha Xaviena akarudi chumbani kwake huku akisubiri kesho siku ya mashindano.
***
“Jamani jindaeni haraka haraka tuwahi ukumbini, hadi saa hizi saa mbili bado hamjamaliza kujipamba humo ndani mwenu?”
Eddy alizungumza huku akigonga mlango wa chumba alichopo Xaviela pamoja na mke wake Rahma, ambao wanajianda kwa kwenda kutazama kinyang’anyiro cha taji miss Tanga, ambapo mtoto wao naye ni miongoni mwa washindani.
“Tunatoka jamani”
Rahma alizungumza huku akimalizia kumpaka wannja Xaviela ambaye amependeza sana. Wakamaliza kujipamba na kutoka katika chumba walichopo. Eddy akajikuta akiwa amewatumbulia mimacho akiwatazama akionekana kuwashangaa
“Nini, mbona unashangaa kama leo ndio mara yako ya kwanza kutuona?”
“Kumbe na nyinyi mukiamua kujipara munapendeza kiasi hicho?”
“Dady kwani sisi tunakasoro gani hadi tusipendeze”
“Hapana maana yangu sio hiyo”
“Ila?”
“Haya mumependeza sana, tuwahini jamani mwenzenu amepiga simu muda si mrefu anadaia simu zao zitachukuliwa kwani muda wa mashindano unakwenda kuanza”
Wakatoka kwa paomoja na wote wakaingia kwenye gari lao, aina ya RangeRover Sport na kuondoka nyumbani hapo na kuwaacha walinzi wakiimaisha ulinzi kila eneo.
***
Upweke ukazidi kumuumiza Xaviena, ambaye kila dakima macho yake yanatazama kwenye mlamgo wa kuingilia wageni waalikwa. Kila mara anajaribu kutazama kama wazazi wake na dada yake wameingia ndani ya ukumbi huu wa hoteli ya Mkonge. Ukumbi huo ume jaa watu wenye hadhi kubwa, pamoja na watu wenye kipato cha kawaida walio kuja kushuhudia mtanange huu wa warembo. Usiku wa leo atatangazwa mshindi atakaye vishwa taji na kuwa mrembo wa mkoa wa Tanga huku, akizawadiwa na gari ya Audi Q7 pamoja na kitita cha shilingi milioni hamsini.
Jinsi muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi mapigo ya moyo ya Xaviena yalivyo zidi kwenda kasi, mbaya zaidi simu aliyo kuwa akiitumia kuwasiliana na baba yake, tayari imesha chukuliwa na mlezi wao wa kike(matron).
Mawazo mabaya kakaanza kumtawala Xaviena, kichwani mwake, huku akiwaza kwamba huenda wazazi wake pamoja na dada yake watakuwa wamepata ajali kwani ni muda mwingi umepita tangu alipo wapigia simu na kuwaambia kwamba wawahi kufika, kutokana mashindano yanaanza saa nne kamilili usiku na hadi sasa hivi zimebaki dakika kumi na tano tangu kuanza kwa mashindano hayo
“Ohhh Mungu wangu, watakua wamepatwa na nini?”
Xaviena alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, na mwili mzima ukianza kumtetemeka mithili ya mtu aliye mwagiwa maji ya baridi.
“Mbona unalia?”
Olvia Hitler alizungumza huku akiwa amesimama nyuma ya Xaviena aliye simama pembezoni mwa jukwaa, huku akitazama mlango wa kuinguilia ndani ya ukumbi huu kupitia uwazi mdogo wa pazia lilizo ziba upande wote wa nyuma ya jukwaa.
“Familia yangu hadi sasa hivi haijafika?”
Xaviena alizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi kana kwamba ni mtu aliye fiwa
“Ohhh usilie my dear, watakuja tu, ninaimani watakuwa wapo njiani”
“Tangu saa mbili, kwani kuna umbali gani kutoka Sahare hadi hapa Raskazoni jamanii?”
“Sawa usijali watakuja, kwani hata mimi pia nipo, hakuna kitakacho haribika, wewe kuwa na amani”
Olvia Hitler akamkumbatia Xaviena,
ITAENDELEA

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4