Sunday, 16 March

Ads Right Header

Buy template blogger

HAMU YA TENDO LA NDOA HUTOFAUTIANA.

Katika mahusiano mengi mmoja kati ya wanandoa huwa na hamu ya Kufanya Mapenzi na kutaka Tendo la  ndoa mara nyingi zaidi kuliko mwenzake kwa sababu binadamu tunatofautiana levo za kuendesha hamu ya Kufanya Tendo.
     


Kama wewe na mwenzi wako mna kiwango kinachofanana cha kuhitaji Tendo la Ndoa basi ninyi mmebarikiwa.


Ukweli ni kwamba suala la Tendo la Ndoa ni moja ya eneo ambalo ni tete sana katika ndoa, ndiyo maana kukataliwa Kufanya na mwenzi wako huwa ni jambo linaloumiza sana (hasa wanaume) ingawa wapo wanawake wana hamu kubwa ya Kufanya kuliko mwanaume ambaye siku zote anaonekana anahitaji Kufanya Mapenzi  24/7.



Hata hivyo kuna sababu za msingi za kibaolojia zinazopelekea mmoja wa wanandoa kuhitaji Tendo zaidi ya mwenzake.

*Nini husababisha hamu ya Tendo la Ndoa?
Hamu ya kutaka Kufanya Mapenzi husababishwa na homoni ambayo kitaalamu huitwa testosterone.
Wote wanaume na wanawake wanayo hii homoni kwenye miili yao.
Wanaume wanayo nyingi zaidi kuliko wanawake kwa sababu wanawake wanayo homoni nyingine inayojulikana kama estrogen.



Msingi ni kwamba kiwango cha testosterone ulichonacho mwilini huweza kuelezea ni kiasi gani au hamu ya Tendo la Ndoa itakuwaje.
Ukiwa na kiwango kikubwa unakuwa na hamu kubwa na ukiwa na kiwango kidogo unakuwa na hamu ndogo.

Mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanaume wana kiwango kikubwa sana cha testosterone na hii husababisha wao kuwa na hitaji kubwa la Tendo la Ndoa.
Moja ya tatu ya wanaume wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na uhitaji mdogo wa tendo.


Kwa upande mwingine mbili ya tatu (theluthi mbili) ya wanawake wote wana kiwango kidogo cha testosterone na husababisha wao kuwa na kiwango cha kawaida cha hamu na moja ya tatu (theluthi moja) tu ndiyo wenye kiwango kikubwa cha testosterone na hawa huwa na hamu kubwa.


Hii ina maana kwamba mbili ya tatu ya wanaume wenye hamu kubwa huishia kuishi (kuoana) na wanawake ambao wana hamu kidogo na wapo wanawake hujikuta wapo ndani ya nyumba na wanaume (theluthi moja) ambayo hamu ya kufanya ni ndogo sana.


*Je, ni homoni peke yake husababisha kutokuwa na hamu ya Kufanya Tendo la Ndoa?

Siyo homoni peke yake ndiyo inayosababisha mwanaume au mwanamke kuwa na hamu ndogo kuna vitu vingine vingi huweza kufanya hamu kuwa ndogo kama vile kuchoka na kazi, kulea mtoto, migogoro katika ndoa, nk.

Pia ni jambo la msingi kutambua kwamba kwa mwanamke suala la maisha huchukuliwa kwa pamoja kwa maana kwamba yupo connected na kila eneo la maisha yake kama vile familia, kazi, tendo la ndoa nk.

Kama mwanamke amekuwa na siku mbaya kazini au amekuwa na wakati mgumu na watoto wake ni ngumu sana kujisikia ana hamu na Kufanya Mapenzi.



Wanawake huhitaji muda wa kuondoa masumbufu au kusafisha mawazo yao kabla ya kujihusisha na Tendo la Ndoa na hii hufanywa na mwanaume ambaye kwake ni mtu wa karibu.
Mwanamke huhitaji kuwa Karibu na mume kabla hajawa tayari kujiingiza kwenye masuala ya kuwa mwili mmoja.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4