Sunday, 16 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 09 & 10 (Return Of Olivia Hitler)



ILIPOISHIA
“Hahaaa. Unataka kujua kwamba mimi ni malaya eheee”
Olvia akamsimamisha wima Eddy, akamvua nguo zake zote na akabaki kama alivyo zaliwa. Akamtazama kwa sekunde kadha na kumshika Eddy sehemu zake sari.
“Nahitaji nikuonyeshe umalaya wangu upo vipi Eddy na miaka yote hiyo kumi na tisa, nime jawa na nyeg** ambazo leo nina hitaji uzishushe zote la sivyo nitamuua mwanao mmoja baada ya mwengine ukishuhudia kwa macho yako haya mawili”
Olvia Hitler alizungumza kwa sauti iliyo jaa mikwaruzo ya kutisha huku mkono wake wa kulia ukiendelea kumchua jogoo wa Eddy taratibu.
ENDELEA
Taratibu Olvia Hitler akaanza kuzinyonya lipsi za Eddy huku akimpulizia pumzi iliyo anza kuyapoteza maumivu ya Eddy mwilini mwake. Hisia za mapenzi zikaanza kumtawala Eddy ambaye sio mara yake ya kwanza kukutana kimwili na Olvia Hitler. Eddy akaanza kuyatomasa makalio ya Olvia Hitler aliye anza kutoa miguno ya kimahaba. Eddy akamvua Olvia gauni lake, akazidi kwenda mbali na zaidi, akacha bikini ya Olvia na kumgeuza, akamuinamisha na kunza kumla kitumbua chake kwa kasi huku akihakikisha ana mkomesha Olvia ambaye siku zote kwenye upande huo wa kitandani huwa Eddy ana ibuka kuwa mshindi.
***
Kuondoka kwa watu wote nyumbani, kukampa nafasi Xaviela kukushanya nguo zake. Akaziweka kwenye begi lake kubwa. Akaingia chumbani kwa wazazi wake, akafungua shelf iliyo jengwa ukutani kwa kuingiza namba za siri ambazo wao wanne katika nyumba hiyo ndio wana ifahamu namba hiyo ya siri. Akatazama vibunda vya pesa za kimarekani vilivyo pangwa vizuri. Xaviela akachukua vibunda vinne vya dola elfu tano tano. Akatoka navyo na kurudi chumbani kwake. Akaviingiza kwenye begi lake la mgongoni aina ya GUCCI. Akataka kutoka ndani humu ila akaona sio busara kuondoka bila ya kumuachia ujumbe pacha wake. Akatafuta karatasi nyeupe pamoja na kalamu, akaandika ujumbe mfupi wa maandishi kisha akauweka juu ya kitanda, eneo ambalo ni rahisi kabisa kwa Xaviena kuuona. Akababe begi lake la nguo na kuliingiaza kwenye gari lake, kisha akaondoka nyumbani hapo huku akiwaacha walinzi kwenye jumba hilo la kifahari.
“Upo wapi?”
Xaviela alimuuliza Frank rafiki yake wa kipindi kirefu.
“Nipo nyumbani”
“Ninakuja”
“Kwema lakini?”
“Nina kuja usitake kujua kama ni kwema ama si kwema.”
Xaviela akakata simu na kuizima simu yale. Akafika nyumbani kwa Frank, akafunguliwa geti Frank akaingiza gari lake hilo na kushuka.
“Vipi umenifanyia suprize?”
“Nishushie begi langu kwenye gari”
Xaviela alizungumza huku akitangulia ndani huku begi lake lenye pesa likiwa mgongoni. Frank akashusha begi hilo la nguo.
“Nitakaa hapa kwako kwa siku mbili kisha nitaondoka”
“Kwema lakini nyumbani?”
“Mbona umekazania kuuliza nyumbani kwetu. Kwani kuna kuhusu nini?”
Xaviela alizungumza kwa hasira huku akimtazama Frank mwanaume ambaye siku zote amekuwa akimfwatilia Xaviela pasipo mafanikio ya aina yoyote.
“Samahani mama, nina imani kwamba ombi langu umenikubalia?”
“Sikiliza Frank sijakuja hapa nyumbani kwako kwa ajili ya kunitomb**. Kumbuka kwamba wewe ni mwalimu wangu wa mazoezi na siku zote siwezi kutembea na mwalimu wangu. Heshima kati ya mwanafunzi na mwalimu ita shuka na sasa hivi sihitaji kumuingiza kinyago chochote moyoni mwangu. Kama unaweza kunisaidia nisaidie kukaa hapa kwako siku mbili kisha nitaondoka. Ila kama haiwezekani, basi nitaondoka muda huu”
Xaviela alizungumza kwa hasira na kumfanya Frank kuwa mpole sana kwani ana mtambua binti hyo ni mtu mwenye hasira za karibu na ni mtu ambaye siku zote huwa ana maamuzi magumu ili mradi kuuridhisha moyo wake.
***
Rahma na mwanaye wakashauriana kurudi nyumbani mara baada ya kushindwa kumpata Eddy katika simu yake ya mkononi.
“Xaviela hayupo nini?”
Xaviena alizungumza mara baada ya kukuta gari la dada yake likiwa halipo katika eneola maegesho.
“Hembu mpigie simu”
Xavien akampigia simu Xaviela, kwa habati mbaya akakuta simu ya Xaviela haipo hewani.
“Hapatikani”
“Atakuwa amekwenda wapi naye huyu jamani?”
Rahma alilalama huku akionekana kushoshwa na matatizo yanayo endelea kwenye familia yake.
“Ngoja nikawaulize walinzi”
Xaviena akashuka kwenye gari hilo na kuwafwata walinzi wawili getini.
“Jamani Xaviela ametoka hapa?”
“Ndio ameondoka akiwa na begi lake la nguo”
Taarifa hiyo ya mlinzi ikamfanya Xaviena kushikwa na butwaa kwa sekunde kadhaa.
“Aha…a….ameondoka na begi la nguo?”
“Ndio tulimuona akilipakiza kwenye gari lake. Kwani hajawaaga?”
“Ahaa basi”
Xaviena akaelekea ndani na kumkuta mama yake akiwa amekaa sebleni.
“Mama Xaviela ameondoka na begi lake la nguo”
“Nini?”
“Ndio walinzi walimuona akilipakiza kwenye gari”
“Ohoo Mungu wangu, jamani amekwenda wapi huyu mtoto?”
Xaviena akakimbilia chumbani kwake ili kudhibitisha hayo yaliyo semwa na walinzi. Akakuta barua kitandani kwake. Akaichukua na kuisoma.
‘Xaviena mdogo wangu. Usiwe na shaka juu ya usalama wangu, nipo sehemu salama, nimeondoka kwa ajili ya kutafuta maisha yangu. Hakikisha una simama kwenye ndoto zako na huendi mbali na mama. Mlinde sana mama. Ninakupenda sana Xaviena na niombee msamaha kwa mama’
Barua hiyo ya Xaviela ikaanza kumtoa machozi Xaviena. Taratibu akarudi sebleni na kumkabidhi mama yake barua hiyo. Rahma mara baada ya kumaliza kuisoma barua hiyo, machozi yakaanza kumbubujika usoni mwake. Akakosa hata cha kuzungumza kwa maana barua hiyo ina jieleza kabisa. Xaviena akaendelea kumtafuta dada yake kwenye simu yake ya mkononii ila hakuweza kufanikiwa.
“Haki ya Mungu hawa watu wawili wata niua mimi mwaka huu”
Rahma alizungumza huku akilia kwa uchungu sana. Familia yake ambayo ilitawaliwa na upendo na furaha leo hii imekuwa ni familia iliyo jaa maumivu na machungu mengi sana.
“Mama usisema hivyo, ukifa mimi nitabaki na nani?”
Xaviena alizungumza huku akimtazama mama yake usoni. Siku hii haikuwa nzuri kabisa kwao, hadi inafika saa sita usiku ndio Eddy ana rudi nyumbani.
“Mume wangu vipi ume fanikiwa kumuona Olvia?”
Rahma aliuliza kwa shahuku kubwa huku akimtazama Eddy usoni mwake. Eddy hakujibu kitu cha ina yoyote zaidi ya kupitiliza hadi chumbani kwake. Rahma akamfwata Eddy chumbani kwao.
“Mume wangu mbona nimekuuliza hujanijibu chochote? Muda wote nikekaa nikiwa na wasiwasi”
“Rahma naomba nilale tafadhali tutazungumza asubuhi”
“Sawa nime kuandalia chakula naomba tukale”
“Nitakula kesho, sasa hivi sina hamu ya kuweka chochote kinywani mwangu”
Eddy alizungumza huku akivua nguo zake. Alama za lipstiki za mabusu, zilizo baki mgongoni mwa Eddy zikamstua sana Rahma. Wivu na maumivu ya moyo wake vikaanza kumtawala taratibu.
“Eddy umetoka wapi?”
Rahma alizungumza kwa hasira huku akimshika mkono Eddy aliye mpa mgongo.
“Rahma si nimekuambia kwamba nahitaji kupumzika.”
“Kupumzika eheee? Nimekaa nyumbani nikikusubiria tuje tule pamoja mume wangu. Kumbe umetoka kufanya umalaya wako na Mungu ameamua kukuumbua mbele yangu, mabusu ya lipstiki yamebaki mgongoni mwako. Kwa nini unanifanya hivyo Eddy, kwani nini hutambui thamani yangu. NImekuwa nikijitunza kwa miaka yote hiyo kwa ajili ya kuheshimu penzi langu kwako. Kwa nini umekuwa una uumiza moyo wangu kwenye kipindi kama hicho ambacho mwanangu mmoja ameondoka nyumbani eheee?”
Karibia maneno yote hayakumstua Eddy, ila neno la mtoto mmoja kuondoka nyumbani likamfanya amtazama mke wake.
“Nani ameondoka nyumbani?”
“Xaviela ameondoka nyumbani. Amebeba kila kilicho chake na kuondoka”
Eddy akatupia macho kwenye shelf yake ya kuhifadhia pesa na nyaraka muhimu. Akaifungua na kukuta kiwango cha pesa kikiwa kimepungua.
“Shenzi huyu mtoto nitamuua”
“Utamua wa nini ikiwa wewe hasira zako ndio zimemfanya mtoto kuondoka nyumbani”
“Nyamaza wewe mwanamke”
“Siwezi kunyamaza na nitakuambia ukweli. Mimi ndio nina jua uchungu wa mtoto. Mimi ndio nilipanua miguu yangu kule lebour na kuwazaa hawa watoto. Ninajua maumivu yake. Wewe hilo wala hulijui ndio maana kwenye kipindi kama hichi ume amua kwenda kujiburudisha kwa malaya zako”
Rahma alizungumza kwa ukali hadi sauti yake ikafika chumbani kwa Xaviena ambaye muda wote amekuwa ni mtu wa kumlilia pacha wake. Xaviena akashuka kitandani kwake na kuelekea katika chumba cha wazazi wake, akausukuma mlango na kukuta ume fungwa kwa ndani.
“Rahma tafadhali usinipigie kelele”
“Maneno yangu sio kelele, ninaongea ukweli na ukweli utabaki kuwa hivyo. Eddy kwa nini umetoka kunisaliti kwa wanawake wengine hadi wamekuachia alama za midomo mgongoni huku?”
Maneno ya Rahma anaye zungumza huku akilia kwa uchungu sana yakamfanya Xaviena kushika kinywa chake huku akiwa amejawa na mshangao.
“Eddy usininyanyase hivi, ikiwa nimeamua kuishi maisha ya kujishusha. Kumbuka ni wapi wewe nimekutoa. Kumbuka ni usaliti gani niliufanya kwa wazazi wangu, ili mradi niwe na wewe. Hivi leo hii ndio una nipa haya malipo yake eheee?”
“Kaaa kimya Rahma”
Eddy alizungumza huku akimziba Rahma mdomo wake kwa nguvu na kumfanya Rahma anze kuminyana ili kuutoa mkono huo. Miguno ya mama yake anaye onekana kuomba msaada ikafanya Xaviana kugonga mlango kwa nguvu.
“Baba muachie mama”
Xaviena alizungumza huku akiendelea kugonga mlango huo kwa nguvu. Rahma akampiga Eddy teke la sehemu zake za siri na kumfanya Eddy amuachie huku akitoa yowe la maumivu makali sana. Rahma akakimbilia mlangoni, akaufungua na kumpita mwanaye spidi na kuingia katika chumba cha wanae. Xaviena akamshuhudia baba yake akiwa ameanguka chini akigugumia kwa maumivu makali sana.
“Rahma nitakuua wewe mwanamke”
Kauli hiyo ya Eddy ikamfanya Xaviena kutimka mbio hadi chumbani kwao. Akaufunga mlango wao kwa ndani na kumtazama mama yake aliye kaa kwenye kona ya kitanda huku amejikunyata kwa woga. Weupe wa mama yake ukamfanya Xaviena kushuhudia jinsi alama za vidole vya baba yake, zilivyo baki mashavuni mwa mama yake. Xaviena akamuonea huruma mama yake na akamkumbatia huku wote wakilia kwa uchungu sana.
***
“Haaaa, haki ya nani huyu mwanaume ni mtamu sana, sijapata ona”
Olvia Hitler alizungumza kwa furaha huku akiwa amejilaza kitandani mwake. Mizunguko sita ya nguvu aliyo kwenda na Eddy wakiwa ofisi kwake imemfanya achoke sana na hata hamu yake ya tendo la ndoa ikiwa imeisha kwa asilimia zaidi ya themanini.
“Sinto mua tena ila kwa sasa niamfanya awe wangu kabisa. Rahma ame faidi vya kutosha”
Olvia Hilter alizungumza huku akiendelea kujigeuza geuza kitandani hapo.
“Eddy mbona umekuwa mtamu jamani? Tofauti na kipindi kile. Naamini yale mabusu mgongoni, ni lazima mke wake atayaona na akiyaona basi uaminifu wa mke wake utaishia hapo na Eddy ataendelea kuwa wangu”
Mlio wa simu yake, ukamtoa Olvia Hitler kwenye dimbwi zito la mawazo ya kimapenzi juu ya Eddy. Akaitazama simu hiyo na kukuna ni namba ya Xaviela.
“Ohoo kimenuka huko”
Olvia alizungumza huku akiipokea simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Habari yako Olvia”
“Safi sana Xaviela, mbona usiku usiku umenipigia kuna tatizo?”
“Hapana, ila nina ombi kwako”
“Ombi gani mwanangu?”
“Nahitaji kupata chuo cha ujasusi, nahitaji nikapate mafunzo hayo ya ujasusi na nikifanikiwa kuhitimu masomo yangu basi mtu wa kwanza kumu hukumu ni baba yangu. Nita hakikisha kwamba ana lipa madhambi yote ya kumuua babu yangu mzaa mama, pamoja na watu wengine ulio nieleza.”
Kauli hiyo ya Xaviela ikamfanya Olvia Hitler kukaa kitako kitandani huku akiwa amejawa na mshangao saa, kwani moyo wake umesha badilisha maamuzi juu ya kumdhuru Eddy, mwanaume anaye mpenda na kumridhisha kitandani.

TANGA RAHA   10

Taratibu Olvia Hitler akashusha pumzi huku akitafuta ni jibu gani sahihi ambalo ana weza kumpatia Xaviela.
“Haloo, una nisikia”
“Ndio nina kusikia Xaviela. Acha nijaribu kufwatilia na kuona ni wapi ambapo nina weza kupata hicho kitengo kisha nitakufanyia mpango”
“Nitashukuru sana Olivia”
“Haya nikutakie usiku mwema. Au kuna jambo lolote una taka kuniambia?”
“Hapana”
“Usiku mwema”
“Nawe pia”
Olvia Hitler akakata simu na kujifunika shuka lake huku akili yake ikirejea kwenye mawazo juu ya mpenzi wake Eddy.
***
Xaviela akatabasamu huku akimtazama Frank usoni mwake.
“Yaani una taka kusomea hiyo kazi kwa ajili ya kumkabili baba yako?”
“Ndio”
“Kwa nini lakini, kumbuka wewe ni damu yake?”
“Alafu hako kamsemo sikapendi mimi. Eti mimi ni damu yake. Sasa kama mtu amefanya makosa unahitaji nisimshuhulikie?”
“Kwa kupania huko wala huto weza kufanikisha hicho unacho kiwaza na nina kuambia ukweli ipo siku uta tambua umuhimu wa baba yako”
“Hembu niachie ujinga wako na wewe”
“Haki ya Mungu vile ipo siku uta jua umuhimu wake. Sisi wengine hadi tunafikisha miaka hii hatuwajua baba zetu kutokana na kifo kuwachukua. Leo hii una ringa kwa sababu una muona ona baba yako.”
Frank alizungumza kwa unyonge huku akiwa amejiinamia. Xaviela akahama kwenye sofa lake na kukaa pembeni ya Frank.
“Frank mbona hukuwahi kuniambia kwamba baba yako ame fariki?”
“Si baba tu, pia mama amesha fariki. Wale ambao una waona wanaishi kule Sahare, wale ni wazazi wangu wa hiyari”
“Hiyari kivipi?”
“Waliniokota nikiwa mchanga kabisa sijitambui”
Xaviela akakaa vizuri huku akimtazama Frank usoni mwake.
“Walikuokota?”
“Ndio, ni historia ndefu sana kwenye maisha yangu. Sikuhiyaji siku hata moja uweze kufahamu kama mimi ni mtoto yatima. Wazazi wale walio nilea, kwa jinsi walivyo nielezea hii historia. Kuna siku waliku wanatoka Dar es Salaam. Walipo fika maeneo ya Mkanyageni wakashuhudia gari ndogo ikiwa imegongwa na roli na ilikuwa ni majira ya usiku sana. Ndipo hapo walipo weza kukutana na mimi, wakaniokoa na kunilea”
“Masiikini pole sana kwa hiyo hawakuweza kukutanisha na ndugu wa upande wa baba yako wala mama yako?”
“Walijitahidi sana kuwatafuta ndugu zangu ila kwa hahati mbaya hawakuweza kufanikiwa kuwapata na hawakuwa na budi ikawabidi wanilee na kunijali kama mtoto wao na siri hiyo nimekuja kuifahamu ukubwa huu”
“Pole sana Frank, kumbe una pitia mambo makubwa na magumu kiasi hicho?”
“Ndio ila nashukuru sana. Ila tafadhali nina kuomba usiweze kumueleza mtu yoyote juu ya siri hii.”
“Siwezi kufanya hivyo Frank. Naamini wewe una nifahamu sana, sina mdomo mdomo wa kuzungumza”
“Ni kweli, ila Xaviela natamani sana siku moja uje kuwa mke wangu. Mwanamke ambaye utanizalia watoto. Na mimi natamani niwe na familia yangu, endapo nitakufa mimi bila ya kuwa na mtoto basi ukoo wangu hauto kuwepo kabisa kwa maana nitakuwa nimekufa na kila kitu kitakuwa kimepotea kwenye maisha yangu”
“Frank nakuomba unisikilize. Nakuheshimu tena sana. Sihitaji kucheza na hisiza zako wala kuuchezea moyo wako. Sijapanga kuzaa kwa sasa wala kuolewa. Sina mshipa wa kuitwa mama, japo nina umbo la kike, sura ya kike ila nina roho ya kiume. Tafadhali hembu badilisha hisia zako na ujaribu kumpatia mwanamke ambaye atakuwa ni sahihi kwenye maisha yako”
Xaviela alizungumza kwa msisitizo huku akimkazia macho Frank.
“Xaviela”
“Samahani Frank nakuomba sana uniache nikalale”
Xaviela akasimama na kuondoka sebleni hapo, ili kupoteza hisia za kimapenzi za Frank. Akaingia kwenye chumba alicho pewa na Frank na kujifungia.
***
Hadi asubuhi Rahma na Xaviena hawakuweza kupata amani kabisa katika chumba chao. Hapakuwa na hata mmoja wao ambaye aliweza kupata hata lepe la usingizi.
“Sijui baba yako atakuwa amesha amka?”
Rahma alizungumza huku akishuka kitandani.
“Acha mimi nikamu……”
Kabla hata Xaviena hajamalizia sentensi yake, wakastukia kusikia mlango wao ukigongwa kwa nguvu. Kila mmoja akastuka huku Rahma akirudi kitandani na wakajikunyata kitandani hapo.
“Fungueni mlango”
Sauti ya Eddy ilisikika kwa ukali sana. Woga ukazidi kuwatawala Xaviena na mama yake. Xaviena akashuka kitandani huku akitembea kwa woga.
“Xaviena usifungue”
Rahma alizungumza huku akizidi kutetemeka kwa woga. Xaviena akafungua mlango na kukutana na baba yake aliye vimba kwa hasira.
“Mama yako yupo wapi?”
“Yuu….”
Eddy akampiga kikumbo Xaviena na kumfanya apepesuke. Eddy akaingia chumbani humo na kumuangalia Rahma aliye kaa kitandani huku akili kwa woga kwani katika kipindi chote cha maisha yake na Eddy hakuwahi kumshuhudia akiwa katika ukatili wa siku mbili hizi.
“Mwanamke muuaji sana wewe. Umenipiga na umeamua kunitelekeza mule ndani peke yangu je ningekufa ingekuwaje?”
Eddy alifoka. Akapanda kitandani hapo na kumshika Rahma mkono na kuanza kumvuta.
“Baba muache mama”
Xaviena aliingilia ugomvi huo na kumshika Eddy mkono ulio mshika mama yake.
“Kaa pembeni na wewe”
“Muachie mama. Mama hajafanya jambo lolote baya, tafadhali”
Eddy akamsukumiza Xaviena kitandani na kumburuta Rahma kitandani hapo na kwa bahati mbaya akaanguka chini huku kichwa chake kikigonga katika pembe ya kitanda, ikapelekea kupoteza fahamu hapo hapo.
“Nyanyuka nimekuambia”
Eddy alizidi kufoka huku akihisi mke wake ana muigizia hali hiyo. Xaviena akamchungulia mama yake huki akiwa juu ya kitanda na kuona utofauti. Akashuka kitandani kwa haraka na kumgusa shingoni na kukuta mama yake akianza kuwa wa baridi, ikiwa ni ishara mbaya sana.
“Wewe Rahma!!”
Eddy alizungumza huku akijaribu kuinama. Ila akajikuta akisukumwa na Xaviena aliye simama huku macho yake yakitawaliwa na hasira kali sana.
“USIMGUSE MAMA YANGUUUUUUUUU…………..!!!”
Kwa mara ya kwanza leo Xaviena ana ionyesha hasira yake halisi mbele ya baba yake. Siku zote Xaviena amekuwa ni mpole na mkimya na Eddy hakuwahi kumshuhudia mwanaye huyo akiwa na hasira.
“Toka ndani kwangu”
“Ngoja niwapigie watu wa gari la wagonjwa”
“Sitaki, nitamshuhulikia mama yangu mimi mwenywe”
Xaviena alizungumza huku akichukua simu yake kitandani. Akapiga namba za msaada katika hospitali ya Bombo na akaahidiwa gari la wagonjwa litafika hapo ndani ya dakika tano.
“Xaviena mwanangu sikukusudia kumfanyia hivyo mama yako”
Xaviena hakumjibu kitu chochote Eddy zaidi ya kuachia msunyo mkali sana. Akaanza kumpepea mama yake huku kwa mara kadhaa akimpima mapigo ya moyo wake.
King’ora cha gari la wagonjwa kikamfanya Eddy kutoka nje na kuwaomba walinzi waweze kuruhusu gari hilo kuweza kuingia. Madaktari walio fika na gari hilo kwa haraka wakaingia ndani na kuongozana na Eddy hadi chumbani kwa wanae.
“Amekumbwa na nini muheshimiwa?”
Daktari mmoja alimuuliza Eddy, aliye jikuta akimtazama Xaviena ambaye ana endelea kutokwa na machozi ya uchungu sana.
“Aha…ameanguka kwa habati mbaya hapo kitandani”
Madaktari hawa wakaanza kushirikiana kumpa Rahma huduma ya kwanza. Wakamuweka juu ya machela walio kuja nayo na kutoka naye ndani.
“Ukithubutu kuleta pua yako hospitalini, nitauadithia ulimwengu kila kitu ulicho kifanya kwa mama yangu”
Xaviena alimnong’oneza Eddy, kisha akaingia kwenye gari hilo la wagonjwa na kuondoka nyumbani hapo. Rahma akafikishwa hospitalini na moja kwa moja akakimbizwa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuanza kupatiwa matibabu. Uwepo wa Xaviena katika hospitali hiyo, kukaanza kuwafanya waandishi wa habari kuanza kuweka kambi huku kila mmoja akitamani kuweza kusikia ni kitu gania ambacho kimemfanya awepo hospitalini hapo.
“Ahaa samahani Xaviena, kuna waandishi wa habari hapo nje wana hitaji kukuhoji”
Nesi mmoja alimuambia Xaviena aliye jiinamia chini huku akimuombea mama yake aweze kupata japo nafuu na kuepuka kwa hali hiyo iliyo mpata.
“Sihitaji kuzungumza na mtu. Tafadhali musiwaruhusu kuingia hapa ndani”
“Je tuwaambie nini kwa maana wamesha anza kuzua zogo hapa na watu wengine wana hitaji kujua ni kitu gani ambacho kina endelea. Ukitazamia hapa ni hospitalini”
“Sasa kama ni hospitalini mimi nifanye nini? Si muna walinzi, watoeni nje kama vipi?”
Xaviena alizungumza kwa hasira sana na kumfanya nesi huyu kuishiwa pozi.
“Nimekuelewa”
Nesi huyu akaelekee eneo walipo waandishi wa habari ambao kwa haraka wakamzunguka ili kuweza kusikia kile ambacho Xaviena amekizungumza.
“Jamani miss Tanga hayupo sawa. Ninacho waomba muweze kumpa muda, akiwa vizuri basi atazungumza nanyi, ila ninacho waomba sana musipige kelele wala musilete fujo kwa maana kama munavyo jua hapa ni hospitali na kuna wagonjwa ambao hawahitaji kabisa kusikia kelele. Asanteni.”
Nesi huyo mara baada ya kuzungumza maneno hayo akarudi ndani.
***
Taarifa ya uwepo wa miss Tanga katika hospitali ya Bombo, ikamfikia Frank kwa kupitia kituo cha tv cha Tanga Tv. Frank akaacha kufanya mazoezi hayo ya asubuhi na kuelekea katika chumba cha Xaviela. Akagonga mlango na baada ya muda kidogo mlango ukafunguliwa.
“Za asubuhi Frank”
“Salama, tafadhali njoo uweze kuona”
“Kuna nini kwani?”
“Njoo uone tu huku kwenye tv.”
Xaviela akaongozana na Frank hadi sebleni. Taarifa ya mdogo wake kuwepo katika hospitali ya Bombo kidogo ikamstua. Hakutaka hata kusikiliza nini kina zungumziwa, akarudi ndani na kuichukua simu yake, akaiwasha na kitu cha kwanza kukifanya ni kumpigia Xavien. Simu ya Xaviena ikaanza kuita, kisha ikapokelewa.
“Dogo vipi, kuna nini kinacho endelea?”
Xaviela wala hakuanza kwa salamu.
“Ni baba”
Xaviena alizungumza huku akilia.
“Baba amekufa au?”
Xaviela alizungumza huku wasiwasi ukimuisha moyoni mwake kwani kama ni mkataba wake wa upendo na baba yake alisha ufuta toka jana.
“Hapana baba amempiga mama hadi amepoteza fahamu”
“NINI…………!!!???”
Xaviela aliuliza kwa mshangao huku akivuta ya taswira ya baba yake, huku moyo wake mmoja una mshauri kwenda kumuua baba yake huku nafsi yake nyingine ikimshawishi awahi kwenda hospitalini kwenda kumuona mama yake.
ITAENDELEA

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4