Mahusiano
UPENDO HUWA HIVI.
Mara ya kwanza ulipopendana na mpenzi wako au mke wako au mchumba wako, kuwaza kuhusu yeye kulikuja kwenyewe automatically.
Ulitumia masaa mengi sana kumuwaza namna anavyoonekana, ukijiuliza atakuwa anafanya nini katika muda fulani, ulikuwa unarudiarudia kuwaza na kujiuliza vitu vizuri ambavyo ungemwambia au kuongea naye wakati mkiwa wote, ulimtumia picha nzuri zenye maneno matamu, ulimtumia sms mara kwa mara kuonesha ulikuwa unamuwaza, uliandika hata barua nzuri kuonesha hisia zako na kwamba ulikuwa unamuwaza, ulihangaika kutafuta maneno matamu ambayo akiyasikia anafahamu kwamba zaidi ya kumpenda ulikuwa unamuwaza.
Na hata usiku ulimuota (ndiyo maana ulikuwa unamwambia usiku hukulala) yeye kwa sababu ulikuwa unamuwaza kuliko kitu chochote.
Ikafika Mahali ukakiri kwamba;
“Siwezi kuacha kukuwaza wewe!”
Hata hivyo kwa baadhi ya wapendanao (inawezekana hata wewe unayesoma hapa ndicho kinachoendelea katika penzi lako) baada ya kuwa wapenzi au kuoana mambo huanza kubadilika kwani mwanamke sasa amempata mwanaume aliyekuwa anamuhitaji; na mume ameshapata tamu ambayo alikuwa anaiwinda miaka yote, sasa kazi ya kuwinda amemaliza, mission complete, job done, malengo yametimia.
Miali ya ukaribu wa kimapenzi inaanza kuwaka kwa udhaifu mkubwa na kilichokuwa kinasukuma kumuwaza sasa kinapoa, sasa unaweka malengo katika kazi na taaluma yako au marafiki, au mambo unayoyapenda wewe binafsi na baada ya muda unaanza kuacha kutimiza mahitaji ya mke wako au mume wako.
Hata hivyo bado ukweli unabaki palepale kwamba ndoa imemuongeza mtu maalumu katika maisha yako na hii haitabadilika na kama uwezo wako wa kufikiri unashindwa kumweka mtu aliyeongezeka katika mawazo yako ili kumpa nafasi basi unakoelekea ni hatari.
Kama hujifunzi kumfikiria/kumuwaza Mpenzi wako basi unaweza kuishia pabaya, inaweza kufika birthday yake usijue, inaweza kufika siku ambayo mlianza mapenzi yenu na usikumbuke na ukalaumiwa kwamba humfikirii yeye bali wewe mwenyewe.
Utakosa nafasi nzuri za kuweza kuonesha upendo wako kwake.
Kuonekana huna wazo lolote kuhusu Mpenzi wako ni adui mkubwa wa kudumisha moto wa ukaribu wa kimapenzi katika penzi.
Mwanamke siku zote ana hamu ya kufahamu namna mpenzi wake anavyomuwaza na hii humfanya kujisikia anapendwa.
Je, ni mara ngapi au ni muda kiasi gani umekuwa kuitumia kuwaza namna unaelewa na zaidi unavyoweza kuonesha upendo kwa mpenzi wako?
Je, ni tukio gani ambalo sasa unaandaa ili kuonesha unamuwaza na unamkumbuka?
“Ndoa Nzuri huja baada ya mawazo Mazuri”

Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment