Mahusiano

WRITER………………………………………………………………..EDDAZARIA G.MSULWA(Next Level Author)
ILIPOISHIA
“Jinga sana wewe fanya jana watu pata ajali jili yako”
Sikujua bosi anacho kizungumzia ni nini kwani sikujua hiyo ajali niliyo isababisha mimi ni ajali gani
“Ajali gani bosi?”
“Wewe jana kuja teja hapa taka wewe tengeneza gari breki na jenga jenga vibaya na kwenda wao pata ajali”
Kumbu kumbu zangu zikanipeleka kwenye gari la jana lililo letwa na waarabu walio niomba niwatengenezee breki na kutokana na mawazo sikujua nilicho kiteneneza ni nini kwani nilifunga funga ili mradi kazi imalizike.
“Bosi ninaomba unisamehe”
“Kuna mimi samehe wewe kuanzi now(sasa) taka wewe ondoka ofini kwangu”
“Basi samahani sana nakuomba unisamehe kwani sikujua kama itakuwa hivi”
“Sema toka na no pay(na hakuna malipo)......fanya mkwe wangu kufa jili jinga yako wewe toka kabla sijapiga simu polisi”
ENDELEA
Bosi alizungumza kwa hasira na kunifanya nitoke ofisini kwake huku machozi yakinilenga lenga na sikutaka watu kujua kitu kilicho jitokeza ofisini kwa bosi na moja kwa moja nikaelekea nyumbani kwetu na kuikuta gari uliyo nikosa kosa kunigonga ikiwa imesimama nje kwetu na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa kwani nikaanza kuhisi kwamba yake maneno aliyo niambia kuwa ataita polisi kuja kunikama mtu mzembe kama mimi yakanijia kichwani na nikataka kugeuza ila nikajipa moja kuwa atakuwa sio yeye.Nikapiga hatua mbili mbele nikielekea mlango wa kuingilia nyumani na kumkuta mama akitoka na yule mama aliye nikosa kosa kunigonga na gari huku wakizungumza na kucheka
Mama alipo niona akaniita na nikapiga hatau za taratibu hadi sehemu walipo na kumfanya mama aliye nikosa kosa kuniogonga kunitazama kwa umakini huku akisikilizia mama anachohitaji kuzungumza
“Mama Caro huyu ndio Eddy mwanangu niliye kuwa nikikumbia”
“Ahaa Eddy habari yako?”
“Salama shikamoo”
“Marahaba hujambo baba?”
“Sijambo......Mama nipo ndani”
“Sawa vipi mbona leo mapema unaumwa”
“Kidogo ninajisikia sikia maumivu ya kichwa”
“Sawa pumzika”
“Asije akawa anaumwa na malaria?”
“Eddy hembo njoo”
Nikatoka nje na mama akaniweke mkono kwenye shingo na akaguna akionekana kulishangaa joto langu la mwilini lilivyo panda kwa kiasi kikubwa hii ni kutokana na kulia kwangu wakati bosi alipokuwa akinifukuza kazi na sikuhitaji kumuambia juu ya swala hilo
“Ngoja basi tumpeleke hospitalini”
“Hapana jamani mimi nipo powa wala nisiwasumbue sana.....Ila mama kopo la dawa umeliweka wapi?”
“Chumbani kwangu kwenye meza”
Nikaingia ndani kutokana siumwi nikaingia chumbani kwangu na kula hadi mida ya jioni mama akaniamsha kwa ajili ya kupata chakula cha jioni.Nikaamka na kuelekea bafuni na kumuacha mama akiwa anaendelea na biashara ya kuuza pombe kwa wateja wake.Nikamaliza kuoga na nikiwa ninatoka bafuni nikamkuta mama akiwa anasukumwa na kijana mmoja aliye kunywa pombe na anakataa kulipa pesa aliyo ambiwa kulipa.Kwa haraka nikamfwata jamaa kwa haraka na kumshika shati na kumtandika ngumi mbili za uso zilizo myumbisha na kumuangusha chini na wezake wakaanza kuamu ugovi na kutokana wamelewa tayari nikawazidi nguvu na kumfwata mwezao aliye msukuma mama na kumkalia tumboni mwake na kuendelea kumshushia mangimi ya uso hadi mama akanishika mkono na kuninyanyua
“Eddy basi mwanangu”
“Mama hawezi kukudhalilisha huyu”
“Ndio mwanangu msamehe......Jamani baa imefungwa hadi kesho naombeni muondoke sasa”
Walevi wakaanza kuondoka mmoja baada ya mwengine na kutuacha mimi na mama na nikaendelea na kazi ya kutoa vitu vilivyo tumika.
“Mama hii biashara ni vyema ukaiacha kwa maana sioni maendeleo ya aina yoyote zaidi ya hawa wau kukuvunjia heshima”
“Lakini mwanangu Eddy tambua hii biashara imeyasogeza sogeza maisha yetu”
“Hata kama mama ila inabidi ifikie kipindi uelewe kuwa unatakiwa na wewe uheshimike na sio hizi shida ndio zikufanye uwe unadharaulika kisi hichi”
“Sawa mwangu nimekuelewa”
“Mama sasa hivi nimekuwa nitajua nifanye nini mama yangu uishi maisha mazuri”
“Sasa mwanangu”
Maisha yakazidi kwenda mbele huku kila siku nikiwa ninatoka asubuhi na kwenda kufanya vibarua vya kulima mbali kidogo na nyumbani na sikuhitaji kumueleza mama kwamba nimefukuzwa kazi isitoshe na yeye ameifunga biashara yake ya uuzaji wa pombe.Urafiki wa mama na mama Caro ukazidi kuongezeka hadi ikafikia hatua mama akawa ananiagiza baadhi ya vitu vyeke nikavichukue kwa mama Caro jambo lililo mp asana furaha mama Caro kipindi akiniona nimeagiziwa nyumbani kwake.
Kadri ya siku zinavyo katika ndivyo nikapoteza matumaini ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Christina kwani sikuweza kupata mawasiliano naye.Maisha yangu yakazidi kupata simanzi baada ya kutoka kwenye mihangaiko yangu na kumkuta mama akiwa hajitambui na sikujua ni ugonjwa gani ulio mpata kwani hata kuzungumza kwake ni kwashida,Nikatoka nje na kukimbilia sehemu zinapo simama bodaboda na kuja nayo nyumbani na tukasaidia na dereva boda boda na tukamuwahisha mama hospitali kwa matibabu zaidi
***
Tukafika nyumbani kwa mama Caro na kushuka ndani ya gari lake na sikumsemesha kitu cha aina yoyote na moja kwa moja nikaenda chumba ambacho mama Caro amenipatia na sikuwa na kitu kingine cha kufanya zaidi ya kulala.Mida ya jioni mama Caro akaniamsha kwa ajili ya chakula cha usiku,Nikaingia bafuni kuoga ili niweke mwili swa na kwende mezani kupata chakula
“Baby nimepata wazo”
“Wazo gani?”
“Uaonaje ukaanza kufanya kazi kwenye gereji yangu kama msimamizi”
“Ni kweli ila ninaomba kidogo akili yangu itulie kidogo ila hata nikaanza kufanya kazi ninajituma kwa nguvu zangu zote”
“Sawa ukiwa sawa utanijulisha”
Baada ya wiki moja nikaanza kazi katia gereji ya mama Caro huku nikifanya kazi kwa juhudi zangu zote japo nimepewa mamlaka ya kuwasimamia wengine ila na mimi ninafanya kazi kama kawaida na kitu kingine ambacho kinanisaidia zaidi ni kwamba nilisha wahi kuifanya hii kazi ya gereji kipindi cha nyuma.Kutokana na ucheshi wangu watu wakatokea kunizoea kupita kawaida japo ni mgeni na kila mtu kwangu nilimchukulia kama ndugu yangu na hata kasi ya uwajibikaji ikaongezeka kwa wafanyakazi wengine na hawakusubiria kuamrishwa na mimi
"Samahani wewe kaka"
Dada mmoja aliniita akiwa ndani ya gari yake aina ya Verosa na nikapiga hatua hadi sehemu aliyo simama
"Bila samahani dada yangu"
"Gari yangu inatoa kimkwaruzo ambacho sikipendi ninapo endesha gari"
Dada akashuka ndani ya gari huku akiwa amevalia kasketi kafupi na shati lenye mistari mistari ya rangi ya chungwa huku tai ndogo aliyo ivaa shingoni ikifanana na mistari ya shati lake nikatambua ni mfanya kazi wa benk moja mjini.Nikaliwasha gari lake na kweli linatoa la kutoa mlio wa mkwaruzo,nikafungua bonet ya gari nikarekebisha sehemu yenye tatizo
"Hembu washa gari"
Akawasha na gari ikarudi kwenye hali yake ya kawaida na mkwaruzo wake haukusikika tena
"Asante sana kaka yangu"
“Hakuna shaka jisikie furaha sasa na gari lako”
Nilizungumza huku nikitabasamu na dada akatoa noti kumi za elfu kumi kumi na kunikabidhi na mimi nikasita kuzipokea
"Za nini hizi?"
"Za matengenezo ya gari"
"Hapana ilikuwa si kazi kubwa ambayo unaweza kunilipa kiasi hicho cha pesa"
"Sawa ila chukua tuu kama asante yangu au unaogopa kuwa bosi wako atakuzingua?"
"Hapana dada yangu wewe kaa nayo tuu na isitoshe hapa mimi ndio msimamizi mkuu"
Dada akanitazama kwa macho ya mshangao kwani kwa mjini hususani hapa Dar es Salaam ni mara chache kukutana na mtu ukampata pesa kama ujira wa kazi aliyo ifanya alafu akaikataa
"Naomba basi namba yako ya simu hata likiharibika nikuite ili uweze kunitengenezea"
Nikamtajia akanipigia nikaipata namba yake kisha akaondoka na baadhi ya wezanga walio lishuhudia tukio langu wakanisogelea huku sura zao zikiwa na matabasamu
“Nini?”
“Ahaa tunakuona toto la ukweli limekuzimikia?”
“Ahaa wapi mbona kawaida tuu jamani?”
“Kawaida wapi kaka Eddy mtoto kamaind hicho kifua mpaka kaomba namba yeye mwenyewe”
“Jamani kwani demu akiomba namba ya simu ni ajabu?”
“Kwa Town hapa ni ajabu sanaa kwa watoto wakali kama wale wanao miliki mandinga(magari) makali kama yale kuomba namba tena kwa mafundi gereji kama sisi masaa yote tumechafuka”
Tukajikuta tukicheka na wezangu na kila mmoja akaendelea na kazi zake,Usiku nikiwa ninarudi nyumbani nikaona gari likiwa limesimama njiani huku linafuka moshi mwingi sehemu ya mbele na taratibu nikapiga hatua za haraka kwenda kulitazama lina tatizo gani,kwa bahati nzuri nikamkuta yule dada wa asubuhi akiwa amejilaza kwenye siti ya derava huku akiwa hajitambui.Nikamgonge kwenye kioo chake akastuka na kufungu kioo huku macho yake dhahiri yakiashiria kuwa amelewa kupita maelezo na pembeni yake kuna mzinga mmoja wa pombe kali
"Ahaaa fundii……umekuja kuchukua hela yalo huku?"
Alizungumza kwa sauti ya ulevi huku akishuka ndani ya gari akiwa anayumba yumba kiasi kwamba akataka kudondoka na nikamuwahi kabla hajaanguka chini.
"Unajua wewe kaka una roho nzuri yaani unamsaidia mtu yoyote yulee ambaye wala humjuiii…..!!"
"Samahani dada labda unielekeze unaishi wapi ili nikupeleke kwa maana hapa ni usiku na isitoshe hapa ni barabarani unaweza ukapata tatizo la kuvamiwa na vibaka?"
"Mimi naishi humu ndani ya gari nalala naoga humo humo ndani ya gari"
Nikashusha pumzi kisha nikamshika kiuno japo amenipita urefu kutokana na viatu vyake virefu ila nikaweza kummudu na kumuingiza ndani ya gari yake na kumkalisha kwenye siti ya pembeni ya dereva
"Ohoo ukinishika kiuno najisikia raha wee kaka nishike tena"
Nikampotezea kutokana ninatambua si akili zake kwani pombe aliyo kunywa ndio zinamfanya kujiropokea maneno ya ajabu ajabu,Nikaingia kwenye gari na kukaa siti ya dereva na kumtazama
"Eti unakaa wapi?"
"Mimi nimekuambi nakaa humu humu kwenye gari huelewi auuu…..wewe ni fundi gani usiye muelewa?"
Nikawasha gari yake ila halikuwaka nikatoka na kufungua bonet na kutengeneza tatizo.Nikaliwasha tena na likawaka na tukaondoka huku nikiwaza ni wapi nimpeleke huyu dada wakati mfukoni sina hata mia kutokana pesa zote za matengenezo anakaa nazo muhasibu ambaye yeye anasuhulika na kuzipeleka benki kila mwisho wa wiki.Nikapata wazo la kwenda kwenye fukwe za bahari zilizopo nje ya jiji ambapo nikalisimamisha gari sehemu ambayo si rahisi kwa mtu kuliona kwani ni chini ya jiwe kubwa lenye uwazi mkubwa,nikamtazama dada akiwa amepitiwa na usingizi nikashusha siti kidogo kisha na mimi nikajipumzisha huku nikitafakari ni nini nifanye na nikakosa jibu.Nikastushwa na mlio wa risasi ambao sikujua ni wapi umetokea na tukajikuta sote tukistuka na dada akataka kupiga kelele ila nikawahi kumziba mdomo
"Shiii..."
“Wee nani?”
Dada aliniuliza huka akijitahidi kuutoa mkono wangu mdomoni mwake
"Tulia mimi ni yule fundi wa gari lako katika ile gereji uliyo kuja asubuhi"
Akanitazama huku akiwa anahema juu juu mithili ya mbwa aliyekimbia umbali mrefu huku jasho likimwagika.Mlio mwengine wa risasi ukasikika na wote tukajikuta tukikaa kimnya huku tunatizamana na hakuna hata mmoja aliye msemesha mwenzake
"Tupo wapi kaka yangu?"
"Tupo mbembezoni mwa fukwe za bahari"
"Tumefikaje?"
"Nitakuadisia kukipambazuka"
Nikafungua mlango kwa tahadhari huku giza jingi likiwa limetawala ila ni nyoto angani ndizo zinaonekana vizuri,nikachungulia eneo zima la bahari sikuona dalili ya kuona mtu au watu na nikapiga hatua chache na nikasimama sehemu ambayo ninaweza kuiona barabara kwa juu na nikaona watu watano wakiwa na bunduki kasoro mmoja ambaye ni mwanamama ila sikuweza kuziona sura zao kutokana na giza kubwa.Nikawashuhudia wakiibeba miili miwili ya watu ambao wanaoneka wamewaua kutokana na milio ya risasi niliyo isikia muda mchache ulio pita.Jamaa wanne wakaibeba miili ile na kushuka nayo eneo la bahari ila sio upande tulio kuwepo sisi na kunifanya nichuchumae chini ili niweze kuona kitu wanacho kwenda kukifanya kwenye miili hiyo
Wakaitupa miili ndani ya bahari kisha wakarudi eneo la barabarani wakaingia kwenye magari yao mawili na kuondoka kwa kasi.Nikarudi ndani ya gari kwa haraka huku nikihema na nikiwa na woga wa hali ya juu ulio upelekea mwili wangu kunitetemeka
“Kuna nini huko nje?"
Dada alizungumza huku mwili ukimtetemeka kwa kiasi kikubwa na nikatulia kwa muda huku nikifikiria kitu cha kumjibu kwani nakahisi nikizungumza kwa wakati huu labda majambazi wanaweza kusikia na kutuua na sisi
"Kuna majambazi wametupa miili ya watu baharini"
"Mungu wangu tuondoke tusije tukapewa sisi hiyo kesi"
Nikawasha gari na kuondoka eneo hili kwa kasi ya ajabu na nikajikuta nikifunga breki za gafla katikati ya barabara na kumuuliza
"Sasa tuelekee wapi?"
Akanielekeza kwake na nikawasha gari na kuondoka kwa kasi na kutokana hakuna foleni hatukuchukua muda kufika anapo ishi na nikasimamisha gari getini na dada akaupitisha mkono wake juu ya mikono yangu na kuminya batani ya honi na ndani ya dakika geti likafunguliwa na mlinzi
"Simamisha gari kwanza"
Dada akaniambia na nikalisimamisha gari kati kati ya geti na akaanza kuzungumza na mlinzi
"Lile gari pale ni la nani?"
"Ni la shem Frenk amekuja na yupo ndani?"
"Kwanini umemruhusu mtu kuingia ndani kwangu pasipo mimi kuwepo?"
"Bosi si nimesha zoea kuwaona pamoja na siku nyingine sian……"
"Wee koma umechoka kazi ehee?"
Alizungumza kwa hasira huku akiwa anamnyooshea mlizi wake kidole
"Hapana bosi sijaichoka ninakuomba unisamehe"
"Twende mwaya"
Nikawasha gari akanionyesha sehemu ya kulisimamisha gari tukashuka huku yeye akitangulia mbele kwa mwendo wa haraka na kabla hajafika mlangoni kwake nikamuongelesha
"Acha mimi niondoke dada yangu"
"Haa unakwenda wapi usiku wote huu?"
"Hapana nawahi nyumbani"
"Hembu acha ujinga wewe usiku huu unadhani utaweza kutembea peke yako barabarani?"
Akanishika mkono na tukaingia ndani huku akiwa amenishika mkono na gafla taa za sebleni kwake zikawashwa na macho yangu yakakutana na jamaa mwenye misuli mingi akiwa amejifunga taulo huku akiwa amesimama kwenye moja ya kuta huku akitutizama kwa macho makali
"Huu ndio muda wa kurudi nyumbani?"
"Unaniuliza wewe kama nani?"
Akaniachia mkono na kusima huku akiwa amejishika kiuno
"Mimi kama mumeo mtarajiwa na huyo ni nani?"
Frank alizungumza huku akisogea eneo tulilo simama mimi na dada ambaye hadi sasa sikuweza kulijua jina lake.Frank akataka kunishika mkono ila dada akaupiga mkono wa Frank usinishike
"Huyu hakuhusu pili huna hadhi ya kuwa na mwanamke kama mimi labda yule malaya niliyekukuta muna tomb**a ofisini kwako ndio ana hadhi yako wewe sawa"
"Clara nitakupasua"
"Nipasue kama wewe ni mwanaume kweli"
Frank akamshika Clara mkono na kumvutia kwake kisha akamsukuma kwenye sofa na akaanguka kama mzigo wa kuni ulio tuliwa kutoka kichwani
"Wewe mpumbavu changanya mbaliga zako kabla sijakuvunja vunja"
Frank alininyooshea kidole nikapiga hatua za kurudi kinyuma nyuma huku mwili mzima ukiingiwa na hofu kubwa
"Fundi wala usiondoke baki hii ni nyumba yangu na huyo mwehu ana mamlaka ya kukufukuza"
"Wewe malaya hembu nyamaza kabla sijakuvunja hicho kichwa chako sizungumzi na wewe ninazungumza na huyu mwehu wako uliye kuja naye kwanza mtu mwenyewe mchafu sijui umemtoa wapi?"
Frank akanirukia na kunishika shingo na kunikandamiza ukutani na nikawa na kazi ya kuanza kuushika mkono wake ili usiendelee kuniminya sana shingo yangu.Frank akanipiga kichwa kilicho nichanganya hadi macho nikaanza kuyafumba fumba,Clara akanyanyuka kwa hasira na kumshika Frank kwa nyuma na kuanza kuminyana naye ili aniachine.Nikamshuhudia Clara akianguka kwenye meza ya kioo hadi ikapasuka na kumfanya kutoa ukulele wa maumivu. Sikujua hata nguvu zimetokea wapi nikaikaza mikono yangu na kuutoa mkono wa Frank ulio nikaba kuoni na nikampiga kigodi cha tumboni na kumfaya ajikunje kidogo na kupata nafasi ya kumpiga kisukusuku cha mgongoni na akaanguka chini. Frank akaninipaga mtama ulioniangusha mzima mzima na akaniwahi kunikalia tumboni na kunikamata shingo yangu kwa mikono yake miwili huku macho yake yakiwa ameyakaza na nikaanza kuhisi malaika mtoa roho anaikaribia roho yangu kuitoa jambo ambalo sikuhitaji linitokee kwa sasa
Nikaanza kuutoa sauti ya kukoroma huku nikianza kupoteza pumzi kwani kila nilipo jaribu kuotoa mikono ya Frank ila nikashindwa na taratibu nguvu za mwili zikaanza kuniishia. Gafla kastukia damu nyingi zikinimwagikia usoni huku huku taratibu Frank akiangukia pembeni yangu na kunifanya nianze kuvuta pumzi kwa haraka ili kuyapa uhai tena mapafu yangu ambayo tayari yalisha anza kupoteza pumzi nyingi.Nikamshuhudia Clara akiwa ameshika bastola yake huku akiwa anatetemeka mwili mzima ikiashiria kwamba yeye ndio amepiga risasi Frank.
ITAENDELEA
STORY ... MY MOM'S FRIEND 03

Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment