HESHIMA YA MWANAUME NI?
Tusiogope kuzungumza sisi kwa sisi ili tupone!
Jamani kabla ya kuwalaumu wake zetu kuwa wanatudharau tujiulize kama ni kweli tunakidhi haja zao kimwili?
Unajua mwanamke hakufuata vyakula,mavazi na pesa tu kwako ndugu yangu,wengine wanavyo makwao na hata wameacha kila kitu wakatufuata sisi wanaume.
Je umewahi kujiuliza walichofuata ni nini na unamtimizia kama awali au speed gavana imeingia kutu?
Kisaikolojia mwanamke ambaye hafiki mnarani sawa sawa huwa na msongo wa mawazo,hasira,kiburi,dharau,hupauka,hukosa amani na kuchakaa.
Humuona mwanaume wake dhaifu kuwa adui na kiumbe kisicho na thamani mbele yake japo wanawake wengi nao mmekuwa washenzi wa tabia,mumeo kapatwa na hitilafu kidogo badala ya kumsitiri kwa kumpa ushauri nasaha juu ya kutafuta ufumbuzi wa kina mnaanza kuwanyanyapaa,kuwadharau,kuwatukana au kuwasifia wanaume wengine mliowahi kukutana nao.
Jambo hilo huwaharibu wanaume kisaikolojia,huondoa kujiamini na kusababisha migogoro ndani ya nyumba na hata wengine kukatisha maisha yao kumbe jambo lilikuwa ni la kisaikolojia tu.
Yako mambo mengi yanayochangia upungufu wa nguvu za kiume;-
(1)Kujichua kwa muda mrefu,
(2)Kuwaza juu ya ugumu wa maisha,
(3)Kuwaza juu ya mwenendo wa biashara na kazi zako, (4)Migogoro isiyokwisha baina ya wanandoa,
(5)Kubweteka baada ya kuoana/yaani hakuna tena ubunifu na mahaba ya dhati,
(6)Magonjwa ya kinamama yanayopelekea harufu mbaya sehemu za siri pia huondoa ladha na utulivu wa tendo lenyewe,namaanisha fistula,UTI sugu na fangas kwa wanaume nao unapelekea kutengeneza ukurutu unaosababisha wanawake kutojiachia wakati wa faragha.
Kutofanya usafi wa kinywa sawa sawa,jambo hili huondoa mvuto,kujiamini na hupelekea kutotuliza akili sehemu moja.
Kumbuka ili uendelee kusimamisha ni lazima mzunguko wa damu na kisaikolojia uwe sawa lakini ukiacha kuzingatia kitu hicho ukahama kiakili na kuwaza kitu kingine lazima utafeli tu na kuhisi una upungufu wa nguvu za kiume au kike.
Tumuombe sana Mwenyezi Mungu atupe afya njema,uwezo na busara ya kushughulikia tatizo hili kwa amani na upendo ili tuzinusuru ndoa na mahusiano yetu.
Tatizo hili si kubwa sana kama tunavyoaminishwa na wafanyabiashara wa madawa na vyakula vinavyoitwa virutubisho.
Mengine ni elimu ya saikolojia tu unakaa sawa na hutoadhirika tena.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment