Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA FEI TOTO

HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA FEI TOTO

FEISAL Salum nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa kwa sasa anachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na kufanya mazoezi binafsi ili kuwa bora.

Tayari Fei Toto alikuwa ameingia kwenye mfumo wa Kocha Mkuu Luc Eymael raia wa Ubelgiji ambapo alikuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Fei amesema:"Nipo vizuri kwa sasa ninachukua tahadhari na kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona, ni ombi langu pia kwa mashabiki na watanzania kiujumla kuendelea kuchukua tahadhari kwani Virusi vipo," .

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4