HIVI NDIVYO OKWI ALIYOKUWA ANAWAPA TABU YANGA
JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Klabu ya Yanga amesema kuwa ilikuwa ni shughuli pevu kupambana na mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi ndani ya uwanja.
Kwa sasa Okwi hayupo ndani ya Simba anakipiga nchini Misri ambapo habari zinadai kwamba huenda akarejea msimu ujao makao makuu ya Simba pale Msimbazi, Kariakoo kumwaga wino na kuendelea kukipiga.
Abdul amesema kuwa ni aina ya wachezaji ambao wanatumia nguvu na akili uwanjani jambo ambalo lilikuwa linampa tabu.
"Ni miongoni mwa washambuliaji wazuri wakiwa uwanjani wakati wowote anaweza kukusababishia matatizo ndani ya uwanja kwa kukupita na kufunga.
"Labda unaweza kufananisha usumbufu wake na kiungo mshambuliaji wetu Bernard Morrison kwa namna anavyofanya akiwa uwanjani," amesema.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment