Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

JINSI WANAWAKE WANAVYOWAKOSEA WAUME ZAO



 WANAWAKE wanajali zaidi kuliko wanaume. Tafiti zinaonesha hivyo. Kiasili wanawake wana hisia za juu zaidi kuliko wanaume. Kitendo cha kuwa na hisia za juu zaidi kinawafanya wanawake wawe wanaguswa zaidi na matendo wanayofanya wanaume tofauti na wanaume.
 Ukiangalia sababu hizo na sababu zingine za kimazingira na tamaduni, zimewafanya wanaume kutegemea zaidi huruma, upendo na unyenyekevu kutoka kwa wanawake huku wanawake wakitegemea zaidi matumizi na zawadi kutoka kwa wanaume.
Sasa tatizo lipo pale mwanaume anaposhindwa kupata anachotaraji kutoka kwa mke wake. Mfano, mwanaume kachelewa kutoka kazini, anarudi kachokwa mno. Kazini kavurugwa na boss na kuchoshwa na majukumu ya kila siku. Fikra na hisia zake ni kwamba anapofika nyumbani atapata faraja na utulivu ila badala yake anakumbana na kisirani, mtu kasusa na hata wakati mwingine maneno ya karaha.
 Mwanaume yoyote anapokutana na hali kama hii, mbali na kuumia sana kihisia ila hujikuta akianza kuwa na hisia za chuki kwa mke wake.
 Anafikiria kaamka asubuhi sana kw aajili ya kwenda kutafuta kwa ajili ya familia yake. kagombana na watu, kabezwa na wengi na hata kuumizwa na maneno ya boss. Akili na hisia zake ni kwamba mara atakapofika nyumbani, atasahau yote hayo kwa faraja na amani atakayosababishiwa na mke wake. Sasa anapokumbana na hali ya namna hii. Ya kuonekana kususiwa ama kupewa maneno ya karaha na mke wake huumia na wakati mwingne hutamani asingerudi nyumbani.
 Nimefanya tafiti nyingi sana kuhusu sababu za wanaume kuwa na michepuko. Zipo sababu kadhaa. zipo za kimaumbile, za kijinga na zipo za namna hii.
 Wanaume wengine huamua kuwa na michepuko nje sio kwa sababu nyingine ila kwa sababu ya kutafuta faraja na raha wanayoikosa nyumbani.
 Fikra za wanaume wengi baada ya kutoka kazini, baada ya kukaripiwa na boss, baada ya kuchoshwa na majukumu, baada ya kupambana na wateja anataka akifika nyumbani ajihisi sehemu tulivu. Ajihisi yupo katika dunia nyingine inayompa hadhi, heshima na raha.
 Mwanamke anapokuwa na tabia ya kugombana hovyo na mume wake. Tabia ya kupenda kuleta mada zinazochochea uhasama na matatizo badala ya kuleta maneno ya furaha, mwanamke huyu ana haribu hisia za mumewe taratibu.
 Mwanaume hata awe na upendo vipi ila kama kila siku anapata karaha na kero kutoka kwa mwanamke wake, taratibu hisia za upendo huanza kupotea na hisia za chuki huibuka. Nani atapenda kuw ana mtu ambaye anamfanya aumie kihisia na achoke zaidi baada ya majukumu ya kila siku.
 Wapo baadhi ya wanawake hutafuta kwa lazima makosa ya wanaume zao ili waweze kuleta tafrani. Mwanamke utakuta yupo busy kwenye ukurasa wa mitandao ya kijamii  ya mumewe kutafuta meseji hata za miaka mitatu iliyopita ili aanze kumuuliza maswali makali mumewe.
 Ngoja niseme neno moja. Kama kila siku mwanamke anatafuta sababu za kumfanya mume wake aonekane mkosaji, jambo hilo sio tu linaharibu amani na utulivu katika familia ila pia linasababisha kiasi cha upendo kilichopo kiyeyuke.
 Wale ambao wako katika ndoa na upendo hakuna, jambo hilo halikutokea bahati mbaya. Wengine walikuwa wakipendana sana ila gomvi na kero za kila siku zimesababisha hali ya upendo baina yao kupotea kabisa. Kuwa makini.
 Mwanamke ana uwezo mkubwa sana kutuliza akili ya mume na kumfanya awe katika hali bora zaidi. Ila kama kila siku ni kero basi hata mwanamke huyo anapoteza maana katika maisha ya mwanaume husika.


  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4