Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 6


Sad Black Girl - Free image on Pixabay


Hakumpenda Linda lakini hakutaka kumwambia ukweli kwa kuwa hakupenda kumuona msichana huyo akilia mbele yake. Alitoa mimba yake kitu kilichomfanya kuamini kwamba kama angediriki kumwambia ukweli kuwa hakutaka kuwa naye basi ingekuwa balaa.
Wakati ambao Linda alikuwa akilazimisha penzi kutoka kwa Dickson ndicho kipindi ambacho kijana huyo alikuwa beneti na Nandy.
Bado maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Nandy na Dickson walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi lakini kipindi chote hicho hawakuwa wamefanya mapenzi.
Hilo halikumfanya Dickson kuumia, kwake, aliamini kwamba kuna siku Nandy angekuwa mke wake wa ndoa. Waliendelea kuwasiliana, kila mmoja alimwambia mwenzake kwamba angekuwa mwaminifu mpaka pale ambapo wangekuja kufunga ndoa kanisani.
Hakuacha kwenda nyumbani kwa binti huyo na kuzungumza naye, aliendelea kumsisitizia upendo wa dhati uliokuwa moyoni mwake.
Baada ya Nandy kuingia kidato cha sita, Dickson akamwambia jinsi alivyokuwa akijisikia mwilini mwake. Hakutaka kufanya mapenzi na msichana yeyote yule, mtu pekee ambaye alitamani sana maishani mwake kufanya naye mapenzi alikuwa Nandy tu.
Akamwambia, msichana huyo alianza kukataakataa lakini mwisho wa siku walikuwa chumbani, kitandani huku wakiwa watupu kabisa na kuanza kufanya mapenzi.
Yalikuwa ni maumivu makali kwa Nandy, hakuwahi kukutana na mwanaume kimwili, siku hiyo hakusikia raha yoyote zaidi ya maumivu tu.
Dickson akampoza na kumwambia kwamba angezoea, na walipoendelea kufanya, Nandy akazoea, akachanganyikiwa mno kiasi kwamba hakuona kama duniani kulikuwa na wanaume wengine zaidi ya Dickson.
Siku zikaendelea kukatika mpaka Nandy alipokuja kumaliza masomo yake ya kidato cha sita na hatimaye kusubiri matokeo na kuona kama alistahili kujiunga na chuo au la.
Hapo, Dickson akamfuata tena mzee Gwamaka na kumuomba ruhusa ya kumnunulia simu Nandy, kwa kipindi hicho mzee huyo hakutaka kukataa, akakubaliana naye na hivyo kumnunulia simu msichana huyo.
Hilo likawarahisishia mawasiliano, wakaanza kuwasiliana kwa karibu, kutumiana picha na mambo mengine. Mapenzi yalikuwa na raha tele, hakukuwa na mtu ambaye aliamini kama watu hao wangeweza kuachana siku moja.
Dickson hakutaka kuvumilia, alichokifanya ni kumtambulisha Nandy kwa wazazi wake, alitaka wamfahamu kuwa huyo ndiye alikuwa msichana wa maisha yake ambaye alitegemea kutengeneza familia pamoja naye.
Hilo halikuwa tatizo, wazazi wakamkubali kwa mikono miwili na kuahidi kugharamia kila kitu katika siku ambayo wao wangeamua kufuanga ndoa.
Maisha yalikuwa ya raha na furaha, kila mmoja alikuwa akimpenda mwenzake na mbele yao waliyaona maisha ya ndoa yakiwa yamewasogelea kwa karibu.
Wanawake wengi wakamuonea wivu Nandy kwa kuwa alikuwa na mpenzi aliyekuwa na uzuri wa sura, wengi wakatamani kumpiku na kumchukua kijana huyo lakini kwa Dickson hakukuwa na nafasi tena, moyo wake haukugawa mapenzi, yote hayo yalibaki kwa msichana mmoja tu, huyo alikuwa Nandy.
Wakati hayo yote yakiendelea, nchini Uingereza bado Linda alichanganyikiwa kupita kawaida. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea nchini Tanzania kwani kwa jinsi Dickson alivyokuwa akimpotezea, muda mwingine alihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
Alichokifanya ni kuwasiliana na rafiki yake, Dotnata aliyekuwa Tanzania na kumwambia aende akampeleleze Dickson ili kuona kama alikuwa na mwanamke mwingine au la.
Hiyo haikuwa kazi kubwa kwa Dotnata, akaanza kazi hiyo ambapo baada ya wiki tu akampigia simu Linda na kumwambia kile alichokuwa amebaini.
“Shoga nakutumia wimbo,” alisema Dotnata, kwa kile alichokuwa amegundua, ilikuwa ni lazima kutumiwa wimbo hata kabla ya kuambiwa.
Akafungua WhatsApp na kukuta ametumiwa wimbo wa Unaibiwa ulioimbwa na Rayvanny, hilo lilimchanganya, hayo yalikuwa majibu ya kile alichokuwa amemtuma Dotnata.
“Unamaanisha kuna mtu anamega penzi langu?” aliuliza Linda huku akionekana kuvimba kwa hasira.
“Ndiyo hivyo! Ila hako kadada kazuri!” alisema Dotnata kwani hata naye alipomuona Nandy, alichanganyikiwa.
“Unanichanganya! Hivi kweli Dicky anaweza kunifanyia hivi? Sikubali,” alisema Linda.
Moyo wake uliuma kupita kawaida, alitamani kurudi nchini Tanzania na kufanya maamuzi magumu. Kwa kipindi hiko ilishindikikana kwani ndiyo ulikuwa mwaka wa mwisho kumalizia masomo yake chuoni hapo.
Alisoma huku akiwa na maumivu makali moyoni mwake, alikumbuka maisha aliyoishi na Dickson, walipendana sasa ilikuwaje leo hii awe na mwanamke mwingine?
Baada ya mwaka kumalizika, akaamua kurudi nchini Tanzania, hakujua angefanyaje, hakujua ni kwa namna gani angeweza kumfuata na kumwambia yale yote aliyosikia na wakati mwanaume huyo hakuwa akimtaka.
Kwake, ilimuwia vigumu sana, ili kumpata Dickson basi alitakiwa kufanya kitu fulani hatari sana ambacho kingemfanya mwanaume huyo kukubaliana naye na hatimaye kuoana kanisani.
Mtu ambaye alimtegemea alikuwa msichana mwingine aliyekuwa akiishi Manzese, msichana huyu aliitwa Amina. Alikuwa binti wa uswahilini, mwenye makalio makubwa, kila wakati alipokuwa akitembea uswahili, makalio yake yalikuwa yakicheza kwenda huku na kule.
Alijua kuwatega wanaume, mtaani alikuwa mtu hatari, wanawake wenye ndoa zao hawakumpenda kwa kuwa alikuwa mwiba mkali kwenye maisha yao kiasi cha kuzitetemesha ndoa hizo.
Aliyatumia makalio hayohayo kuwachukulia waume zao kitu ambacho kiliwafanya wanawake wengi kumchukia na kumuona kuwa ni adui namba moja.
Kumpata Amina wala halikuwa tatizo, alimfuata mpaka kwao Manzese na kuanza kuongea naye. Alimpa kazi hiyo, kwa Amina, hilo wala halikuwa tatizo, kwanza akainuka na kuanza kumuonyeshea Linda jinsi alivyokuwa amejaaliwa.
Akayatingisha makalio yake, yalikuwa laini sana na mbaya zaidi kwa ndani hakuwa amevaa nguo yoyote ile hivyo kuifanya dela kuingia kwa ndani. Alitamanisha kiasi kwamba hata Linda mwenyewe alitamani kuwa mwanaume ili amfaidi mtoto mzuri kama Amina.
“Kwa hiyo kazi yenyewe ni ipi?’ aliuliza Amina huku akimwangalia Linda.
“Nataka umtege, yaani umtege mpaka ategeke. Naujua udhaifu wake, anapenda sana wanawake,” alisema Linda.
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Na makalio anayapenda?”
“Sidhani lakini hakuna mwanaume anayechukia makalio. Hata kule Uingereza tu ukiwa na makalio makubwa, wewe utavuma mji mzima,” alisema Linda.
“Sawa. Kwa hiyo inakuwaje sasa kwenye kufanya hiyo kazi?” aliuliza Amina.
Akaanza kumwambia namna ambavyo kazi hiyo ilitakiwa kufanyika. Kwa Amina, ilikuwa nyepesi sana, ni kama kumsukuma mlevi kwenye mteremko wa mlima.
Akamwambia Linda kwamba alikuwa tayari, alimhakikishia kwamba kwa kutumia makalio yake basi kazi ile ingefanikiwa kwa urahisi sana, hivyo alichokifanya ni kumpa namba ya Dickson kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
“Ukifanikiwa nakupa shilingi milioni tatu,” aliahidi Linda.
“Basi ziandae kabisa manake kwenye kazi hii hakuna kushindwa,” alisema msichana huyo aliyekuwa akiyaamini makalio yake kumpata mwanaume zaidi ya kumwamini Mungu wake aliyemuumba.

Dickson alikuwa amekaa ndani ya chumba chake, hosteli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kichwa chake kilikuwa na mawazo tele juu ya mpenzi wake aliyekuwa akimpenda kwa moyo wote. Kwa kipindi hicho, hakukuwa na kitu chochote alichokuwa na hamu nacho kama kuona akimuoa Nandy ambaye kwake alikuwa amekufa na kuoza.
Aliwaambia wazazi wake kuhusu msichana huyo, walimzoea na kumpenda na hata wakati mwingine kumpigia simu na kumsalimia. Walikuwa karibu kitu ambacho kwa Dickson kilimfurahisha kwani kuungwa mkono na wazazi katika jambo kama hilo halikuwa la kupuuzia.
Wakati kichwa chake kikiwa na mawazo tele, mara simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia kioo cha simu ile, mtu aliyekuwa akipiga hakuwa akimfahamu kwani namba ilikuwa ngeni kabisa kwenye simu yake. Akaanza kujiuliza kama ilikuwa sahihi kuipokea au la, akaamua kuipokea.
“Halo,” ilisikika sauti nyororo ya msichana kutoka upande wa pili.
Kwa jinsi sauti ile ilivyosikika, moyo wake ukapiga paaa. Ilikuwa sauti nyororo kupita kawaida, ilipita sikioni mwake, ikatetemesha misuli yote na kwenda kuuchanganya moyo wake vilivyo. Pale kitandani, akajiweka vizuri.
Hakukuwa na kujiuliza zaidi, alijua kwamba kwa jinsi sauti ile ilivyokuwa nzuri ilikuwa ni lazima msichana huyo naye awe mzuri kama sauti ile ilivyokuwa.
Akaanza kumuumba msichana wake kichwani kutokana na ile sauti aliyokuwa akiisikia kwenye simu yake, msichana aliyemuumba muda huo alikuwa bonge moja la msichana ambaye hata ukizunguka Tanzania nzima, hutoweza kumpata.
“Halooo!” naye aliita.
Msichana huyo hakuwa mwingine, alikuwa Amina. Akaanza kuongea naye, alimwambia kwamba alikuwa akimtafuta rafiki yake aliyeitwa Ashura. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea, alivyoiremba sauti yake bado iliendelea kumvuruga Dickson na kumchanganya zaidi.



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4