NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI SEHEMU YA 7

“Utakuwa umekosea namba dada.”
“Jomoniiiii! Kweli nimekosea namba kaka’ngu?” aliuliza Amina, hako kasuati kake bado kalikuwa na msisimko moyoni mwa Dickson.
“Yeah! Umekosea!”
“Sawa. Basi nashukuru baby boy!” alisema Amina, alivyosema Baby Boy, mapigo ya moyo wa Dickson yakaongeza kasi.
Huo ndiyo ulikuwa udhaifu wake mkubwa, alipenda sana wanawake japokuwa moyo wake ulikuwa umezama na kuoza kwa Nandy. Kila alipokuwa akiongea na msichana huyo ndivyo alivyozidi kuchanganyikiwa naye.
Mwisho wa siku wakaanza kupiga stori za kawaida na kuzoeana huku Amina akimwambia Dickson kwamba katika maisha yake alikuwa amekutana na mwanaume kimwili mara moja tu, tena maumivu aliyoyasikia siku hiyo, hakutaka kurudia tena.
“Huwa inauma kwa siku moja tu, baada ya pale, mambo yanakuwa mukide,” alisema Dickson kwani alijua kuwa aliyekuwa akiongea naye alikuwa msichana wa uswahilini hivyo naye akaanza kuingiza mikato ya kiswahili.
“Basi sawa.”
“Nimefurahi sana. Hebu nitumie picha zako!”
“Upo WhatsApp bebi?”
“Nipo!”
“Sawa nakutumia!”
Kwa kipindi cha dakika chache tu tayari alikuwa amemsahau Nandy, msichana mpya akamuingia moyoni mwake na hakutaka kusikia la mtu yeyote yule.
Akaingia WhatsApp huku tayari akiwa amesave namba ile kama Cute Ammy. Baada ya dakika chache, picha zaidi ya kumi na tano zikaingia kwenye simu yake, alipozipakua na kuziangalia, Dickson bado nusu azimie kwa mshtuko.
Hakuamini kama angekutana na mwanamke aliyekuwa na kalio kama lile alilokuwa akiliona, alichanganyikiwa, aliliangalia mara mbilimbili, lilikuwa kama pembe la ng’ombe, hata lilipokuwa likifunikwa khanga bado lilionekana tu.
Macho yakamtoka, ashki ya kufanya mapenzi na Amina ikamkamata kwa kiwango cha juu kabisa. Wakati akiwa amepigwa butwaa, akatumiwa video ilioyomuonyesha msichana huyo akikatika kitandani huku akiwa amevaa taiti na cheni kiunoni.
“Mamaaaaaaaaa..” alijikuta akisema kwa sauti, akainuka kabisa kitandani ili aone vizuri kwani alihisi kama anapitwa.
Udenda ukamtoka, alikuwa kama fisi aliyeona mzoga. Hakutaka kuchelewa, hapohapo akampigia simu.
“Amina. Naomba nikuone!” alisema Dickson huku akionekana kuchachawa.
“Jomoniiiiiii!”
“Please naomba nikuone! Siwezi kuvumilia, nitakulaje kwa macho na wakati nina mikono!”
“Utaweza?”
“Nijaribu!”
“Basi sawa. Kwa sasa nipo Dodoma, nitakuja kesho, nitapanda basi la asubuhi, nahisi saa kumi nitakuwa huko,” alisema msichana huyo, hakuwa Dodoma, alikuwa chumbani kwake huko Manzese.
“Hapana! Nakutumia nauli ya ndege uwahi. Ngoja nikutumie,” alisema Dickson.
Hakutaka kuchelewa, haraka sana akaingia kwenye huduma za kibenki kwenye simu yake na kumtumia msichana huyo kiasi cha shilingi laki tano. Hakutaka kuona akichelewa kufika Dar, alitaka kumuona haraka sana.
Amina alipoipokea pesa hiyo, akasimama, akanyoosha mikono yake kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa makalio makubwa aliyompa kwani ndiyo yalikuwa yakimfanya kuwachuna wanaume vilivyo.
“Mungu ahsante kwa haya makalio, hakika ulijua kuyaumba,” alisema Amina.
Upande wa pili Dickson alikuwa amechanganyikiwa, akili yake iliruka, muda wote alikuwa akiziangalia picha za msichana huyo, zilimchanganya kupita kawaida.
Hakuacha kuchati naye, muda mwingi alikuwa akichati naye na kumwambia jinsi alivyokuwa na hamu ya kukutana naye. Siku hiyo hakutaka hata kuwasiliana na Nandy, mtu wa kwanza aliyekuwa kichwani mwake alikuwa huyo Amina.
Usiku, mawazo yote yalikuwa kwa msichana huyo, hakuacha kuwasiliana naye na kurudia kuziangalia picha zile mara kwa mara.
“Ila naomba nikuulize kitu bebi!” alisema Amina.
“Uliza tu!”
“Una mpenzi?”
“Hapana! Sina! Nimekuwa peke yangu kwa kipindi kirefu sana mpenzi,” alijibu Dickson.
“Kweli?”
“Haki ya Mungu tena.”
“Basi kwanza nitumie picha zako na wewe.”
“Haina shida.”
Dickson hakutaka kuchelewa, muda huo alikuwa radhi kufanya kitu chochote kile lakini si kumkosa Amina aliyekuwa na makalio makubwa. Akamtumia picha zaidi ya tano hukohuko WhatsApp.
Amina alipozipata picha za kijana huyo na kuziangalia, hakuamini kama mtu huyo ndiye aliyekuwa akichati naye. Dickson alionekana kuwa kijana mwenye sura nzuri kupita kawaida.
Tabasamu lake lilimpagawisha Amina, alichanganyikiwa, katika maisha yake japokuwa alitembea na wanaume wengi lakini hakuwahi kutembea na mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama alivyokuwa Dickson.
Aliambiwa kuucheza mchezo mbaya sana na Linda lakini kwa jinsi Dickson alivyokuwa na sura nzuri, akajiuliza kwa nini asitulie naye na kufikiria kujenga maisha?
“Hivi kweli niucheze mchezo ule jamani kwa mwanaume mwenye sura nzuri kama huyu? Mh! Mbona Linda ananipa wakati mgumu!” alijisemea.
Baada ya kumaliza kuwasiliana na Dickson, akaamua kuwasiliana na Linda na kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kwamba alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kazi ile aliyokuwa amempa.
Kwa msichana huyo ilikuwa ni furaha tele kwani miongoni mwa vitu ambavyo hakuwa akitamani kuviona ni Dickson akimuoa Nandy ambaye kwake alionekana kama adui mpya katika maisha yake.
“Sasa onana naye kwa siku ya kwanza, muonyeshee mambo mazito, kitandani tawala sana mchezo mpaka achanganyikiwe,” alisema Linda kwenye simu.
“Haina shida, nitafanya kama nacheza baikoko au segele,” alisema Amina huku akiwa na uhakika wa kufanikiwa kwa kie ambacho angekwenda kukicheza kwa mwanaume huyo.
Siku iliyofuata akawasiliana na Dickson na kumwambia apange sehemu ambayo walitakiwa kuonana. Hilo halikuwa tatizo, Dickson akamwambia sehemu ambayo walitakiwa kukaa na kuzungumza.
Ilikuwa ni kwenye hoteli ya Mmarekani Royal iliyokuwa Sinza jijini Dar es Salaam. Wakati Dickson akiingia mahali hapo, kila mtu alibaki akiliangalia gari alilokuja nalo, lilikuwa la kifahari mno, kila mtu aliliangalia huku wakiwashtua wenzao ambao hawakuwa wameliona.
Baada ya sekunde chache, Dickson akateremka, kila mtu alibaki akimshangaa, wasichana waliokuwa mahali hapo wakabaki wakimwangalia. Dickson alikuwa na sura ya ajabu, alikuwa mwanaume ambaye alibarikiwa sura, iliwezekana kuwa zaidi ya wanaume wote nchini Tanzania kipindi hicho.
Hotelini hapo,wakaonana, uzuri wa Dickson ulikuwa umeongezeka machoni mwa Amina, alibaki akimwangalia mwanaume huyo, hakuamini kama mtoto wa Manzese kama yeye ambaye alizoea kupata wanaume wababaishaji sasa alikuwa njiani kulala na mwanaume aliyekuwa na sura nzuri kama Dickson.
Wakabaki wakiongea tu kwenye mgahawa wa hotelini hapo. Amina alijua kuongea na mwanaume alijua jinsi ya kumfanya mwanaume kumdatisha. Wakiwa hapohapo kwenye viti, akaupeleka mkono wake katika miguu ya Dickson na kuanza kumminyaminya kwa kutumia kucha zake ndefu.
Hilo lilimpagawisha mno Dickson, alichanganyikiwa, hakuamini kama msichana huyo alimfanyia michezo hiyo ambayo alizoea kuiona katika filamu za kikubwa tu.
Hakuwa amewahi kutembea na mwanamke wa uswahilini, alizoea kutembea na wanawake wa ushuani ambao hawakuwa wakijua lolote lile, hawakujua jinsi ya kumpagawisha mwanaume faragha, hawakujua kufanya chochote zaidi ya kuwa gogo tu kitandani.
Amina alilijua hilo, alimfanyia utundu hapo kwenye kiti mpaka Dickson akachanganyikiwa, akili ikamruka na kuhisi kama alikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa.
“Nakupenda mpenzi!” alisema Amina, tena alimwambia hilo sikioni kabisa huku akimpulizia na pumzi yake katikati ya sikio.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment