NEC yataka wananchi wajitokeze katika uhakiki wa wazi wa kuwezesha kupiga kura.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Wananchi waliojiandikisha katika Daftari la wapiga kura Mwaka 2015 na wale waliojiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari Awamu ya kwanza wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhakiki taarifa zao pindi Daftari litakapowekwa wazi katika maeneo yao na watumie njia nyingine za uhakiki Kama ilivyoelekezwa.
Rai imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Semistocles Kaijage katika ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa kwa ajili kuweka wazi mabadiliko yaliyojitojeza kwenye Daftari la Awamu ya Pili ya Kupigia kura na kukabidhi nakala Kwa wawakilishi wa vyama vya siasa
Jaji Kaijage amesema uboreshaji huo utaanza Aprili 17 na kukamilika Mei 4 mwaka huu kwa nchi nzima ambapo wamegawa katika ruti tatu na kufanyika kwa siku tatu kwa kila mkoa kwa Tanzania bara na Vusiwani.
Hata hivyo amesema kwa jumla ya vituo vitakavyotumika awamu hii ni 4006 badala ya 8031 vilivyokuwa vimekubaliwa hapo awali ambapo kwa sass vituo 3956 vitakuwa Tanzania bara na 50 Zanzibar.
Aidha amesema uboreshaji huu utafanyika katika kila Kata ambapo kutakuwa na Mwandishi Msaidizi na BVR kit Operator ambao watakuwa na orodha ya vituo vyote katika Kata husika na watendaji hao watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa za mpiga kura yeyote.
Aidha amesema wananchi hususani wenye sifa ya kujiandikisha kama wapiga kura wapya wasisubiri kujitokeza siku ya mwisho ya zoezi na hivyo kusababisha msongamano bali wafike vituoni mara tu zoezi litakapowafikia na watuze kadi zao.
Sambamba na hayo Jaji Kaijage amesema NEC haina wataalamu wa Afya ila imenunua vifaa vya kujikinga kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 unaisababishwa na virusi vya corona na tayari wametoa maelekezo kwa watendaji wake kuzingatia miongozo ya wataalamu wa Afya.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Uboreshaji wa Daftari la Mipiga Kura awamu ya pili.
Mkurugenzi wa Uchazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dkt.Wilson Mahera akitoa akizungumza wakati wa kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume hiyo wakati wa Mkutano vyama vya siasa wa Uboreshaji wa Daftari la Mipiga Kura awamu pili utaoanza hivi karibuni.
Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mstaafu Francis Mutungi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya siasa nchini John Shibuda wakati Mkutano wa vyama vya Siasa na NEC.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama CHAUMA Eugene Kabendera akitoa akiuliza swali kuhusiana na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mipiga Kura awamu ya pili katika Mkutano wa Vyama vya Siasa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Oparesheni na Mafunzo wa Chadema Benson Kigaila akichangia katika katika Mkutano vya Siasa na NEC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Semitocles Kaijage akijibu maswali ya viongozi wa vyama vya Siasa katika Mkutano wa Vyama hivyo na NEC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea kati ya vyama vya Siasa na NEC
Leave Comments
Post a Comment