somo la leo linataka utulivu kidogo unielewe na likikukaa kichwani, basi ndoa yako/penzi lako Litakuwa salama miaka 100.
Shoga yangu somo la leo linataka utulivu kidogo unielewe na likikukaa kichwani, basi ndoa yako itakuwa salama miaka 100.
Hutakiwi kujisahau mama, mwanaume wako atakwenda nje, shauri yako! ❤❤❤ Mwanaume aliyekamilika lazima aamshwe asubuhi. Tena siyo kwa kurukaruka, la hasha! Mwamshe kwa utulivu, umfanye aamke akiwa mwepesi.
Mwanaume anapoamshwa asubuhi, inamwondolea uchovu, hata akili inachangamka, hapo anakuwa kamili bin tayari kwa ajili ya ujenzi wa taifa. Shoga, mpaka sasa hujaelewa mwanaume anaamshwaje? ❤❤❤Unajua sana, hebu nitolee umbeya huko!
Hii inawahusu sana wale wanawake ambao wanatabia ya kuamkia kwenye majungu ya vitumbua, maandazi ukiuliza eti ni biashara. Hivi mwanaume akitoka nje ya ndoa kwenda kutafuta kuamshwa utaweza kufanya biashara zako na zikaenda kweli? ❤❤❤
Mwingine anadai anafanya usafi wa nyumba. Acha mambo hayo wewe. Jitulize hapohapo kitandani, mvutie baba watoto kwa mambo matamu, baada ya hapo hakikisha unampa kiamshio ili aamke.
❤❤❤Unaposhindwa kumuamsha mumeo asubuhi, unamwacha kwenye bahari yenye kina kirefu na unampa nafasi ya kuwa mzito katika kila jambo. Kwa nini usimsaidie mwezako? Unataka huduma hiyo apewe na nani? ❤❤❤
Mwingine anaamka amechoka ati! Hebu acha mambo yako, kilichokuchosha nini. Aliyekwambia nani kama kiamshio cha asubuhi kinaongeza uchovu? ❤❤❤MWANAUME ANAAMSHWAJE?
Ikifika alfajiri mwanamke kuwa wa kwanza kuamka kitandani, baada ya hapo fanya uchokozi wako kwa kumwamsha taratibu. Tena huo ndiyo muda wako wa kutumia utaalamu wako wote kuhakikisha anakuwa tayari kwa kupokea kiamshio kutoka kwako. ❤❤❤
Endapo atapata kiamshio na umempa inavyotakiwa, utakuwa umefanikiwa kumfanya aamke akiwa amechangamka sawia na mawazo yake yote yatakuwa kwenye kazi.
Baada ya hapo, mpeleke bafuni akaoge, akitoka huko akute umeshamwandalia kifungua kinywa kizuri. Hakikisha kina mvuto ambacho anakipenda. Huo ni ushindi shoga. ❤❤Atakapotoka kwenda kazini, mawazo yake yote hujikita nyumbani. Aende nje kutafuta nini ikiwa raha zote anakutana nazo nyumbani? Shoga yangu, wengi wanasalitiwa kwa sababu ya kujisahau.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment