STORY: PENZI GUMU EPISODE 15 FINAL EPISODE
Nika panic sana yaani hasira ilinijaa sio kawaida nikatoka nikaenda zangu kunywa mpka nilipo choka nikarudi nyumbani zikko anajitahidi kunisemesha lakini mimi sina habari nae.. Asubui niliamka mapema kabla yake nika omba ruhusa kazini kwamba leo nna dharula sitafika..
Nikaenda moja kwa moja dukani nikafungua nika kaa mimi hapo nimenunua kufuli lingine nikawa nimetulia wateja wanakuja kama kawaida nawahudumia badae mida ya mchana akaja mdada akamuulizia zikko nikamwambia hayupo ampigie simu..
Zikko akaja mida ya mchana akakuta duka liko wazi akatahamaki.. "Ni leo tu ndo nmechelewa my love nlikua najiskia vibaya sana" nikamjibu "Oky poa" akasema "Imekuaje leo umekuja huku?" Nikamwambia "si ni dukani kwangu?" Akasema "Sawa" amekaa pale nikapata plan yani huyu namuacha kwa majuto mimi nimempa mapenzi yangu yote alafu yeye ananifanyia mambo meusi hajanijua vizuri..
Nikaingia online nikatafuta chumba nikapata chumba na sebule.. Nikamwambia zikko "natoka kidogo" akasema "sawa" nikaenda kupa angalia nikapapenda nikalipia nikatafta gari nikagamisha kila kinacho nihusu nikapeleka nyumba mpya alafu nikarudi dukani.. kimya kimya yaani ki professional najifosi kumchekea ila moyoni naumia sana.
Akaniuliza "baby ulienda wapi umechelewa" nikamwambia "Sorry babe.. nlienda kuomba ruhusa kazini" akasema "sawa" nikamwambia "tutoke twende tukale hotelini babe" akasema "Sawa my love" tayari ilikua jioni yani naongea tu ila natamani hata sijui nimfanyeje tuu maana ukiangalia mimi ndo namlea kitu chochote pesa yoyote atake nampa kwanini anifanyie ushenzi mimi? Moyo unauma mno ila najikaza tu maaana niliamua kumuacha kisomi..
Nikamwambia "tangulia kwenye gari" mimi nikabadilisha kufuli kisha nikamwambia mlinzi "kwanzia leo mimi peke yangu ndo mhusika wa hapa na unanitambua kufuli nimebadirisha na yule bwana hajui ila nitamwambia ila akija kwa fujo deal nae hata polisi muitie" akasema "na yule mdogo wako je?" Nikamuuliza "Mdogo wangu gani?" Akasema "Kuna binti huwa anakuja kushinda nae hapa pia alisema ni mdogo wako" nikasema "Sina ndugu hapa mjini" akasema "sasa yule nani?" Nikamwambia "labda malaya wake" hakujibu kitu mimi nika amua kuondoka zangu.
Nikaingia kwenye gari nikawasha gari tukafika hotelini tuka agiza chakula kwa mawazo yake mie ndo nimemtoa "Dinner Date" dinner date my foot kwa ushuzi wote alonifanyia hata hamu sina.. Nika agiza vyakula vya gharama mwambia "Babe agiza chochote leo niko na mood nzuri sana" wine za gharama vyakula vya gharama fanya kama unaona😋😋
Ye anakula huku anachati najua tu anachati na wanawake zake nikamaliza nikamwambia "Nakuja mala moja" akasema "Sawa" kwakua alikua busy sana na simu nikaenda mpka pale reception nikamwambia yule dada "Bill yote atalipa boss pale" akasema "No prob" nikaondoka zangu nikawasha gari yuleee nikaenda kwangu nyumba mpya.
Amekaa wee baada ya masaa kama mawili akanitumia msg "Uko wapi?" Nikamwambia "Nyumbani" akasema "poa nakuja" baada ya dakika tano kapiga simu "wee mwanamke umeondokaje hapa hujalipa?" Nikamwambia "We ndo unatakiwa kulipa na kwa taarifa nkwambie tu tumeachana" nikakata simu..
Katuma msg sijibu kapiga simu mpka kachoka nikamblock.. alinitafta mpka akachoka mwenyewe nikaendelea na mambo yangu aliporudi nyumbani sijui alirudije mwenyewe alituma msg za malalamiko na misamaha kibao "Nisamehe mke wangu umeenda wapi mbona chumba kipo kitupu" nikamtumia msg moja na ya mwisho "it's over between us" akaendelea kutuma msg zake misikumjibu tena.
Kesho nimeenda kazini namkuta boss wangu nje "Nikamwambia leo umewahi sana" akasema "Nimewahi kudai pesa yangu" nikampita nikamwambia "Goodluck" akasema "Come-on Asia nakudai laki na 25" nikacheka kiutani tu huku naenda ofisini nikamwambia "Haha okay" akanifata akanambia "Jana nimemlipia boyfriend alikua anadhalilika hotelini akasema nitamalizana na wewe" nikamwambia "Ooooh hiyo ni biashara yenu mimi sikuwepo" akasema "kwaiyo nimetapeliwa?" Nikamwambia "Naah kadai hela yako"
Mimi nikaenda ndani nika anza kazi zangu..maisha yalikuwa hivyo ilikua ngumu ila zikko nilimtoa kabisa moyoni. Na kuanza maisha mengine Mungu akimleta wa kwangu basi nitampokea wakati wa Mungu ni wakati sahihi.
........ THE END......
FUNZO..
kuna tofauti kati ya uvumilivu na upumbavu Kuna vitu vya kuvumilia ambavyo ni vya kawaida pesa..Mali..watoto hivyo ni vitu ambavyo vinavumilika..
Lakini heshima na mapenzi wala si vya kutafuta kma upo na mtu sahihi basi utavipata bila kuhangaika ila ukimpata mtu ambaye hujapangiwa hakuna rangi utaacha ona!!
Kuna mapenzi kweli lakini sio kumlea mwanaume na kumchukulia majukumu yake mnatakiwa kusaidana and as the matter of fact mwanaume ndo anatakiwa kukulea lakini ukimuendekeza we ndo utakuw kitega uchumi chake na atatafta pahala pa kuzitumia pesa zake au unazo mpa...
Mwanaume akikupenda atakupa kila unachostahili iwe mapenzi..matunzo..heshima na kila kitu same goes to mwanamke.. yaaani mapenzi ya kweli hayajifichi..
Kuna muda mtu anakuwa kwenye mahusiano na mtu kwa ajili ya kitu fulani tofauti na mapenzi ya dhati wengine hufikia katika ndoa kabisa..mwisho wa siku mbivu na mbichi hujitengaa.
Bro.. mwanamke ulie nae anakupenda kweli au kisa unamlipia kodiiii?????..
Auntie.. Uyo niggah ulonae anakupenda kweli au kisa umeumbika basi akiongozana na wewe roho yake kwatuuuuu????
Mapenzi ya kweli hayanunuliki kwa gharama yoyote..
Love you..
Next story soon..
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment