STORY: PENZI GUMU EPISODE 14
Basi nililia mpaka nikachoka nika amua tu kuendelea na mambo mengine huku najiuliza nini cha kufanya wakati moyoni najua kabisa kwa zikko ujanja sina na kumuacha siwezi. Badae zikko alirudi nikamwambia "vipi tulipanga uende nyimbani kujitambulisha" akasema "Mbona una haraka sana mke wangu tutaenda tuu" basi mie kuniita vile tu moyo wangu unafarijika mambo yakaisha kama hakijatokea kitu na wala sikutaka kufatilia tena maana sikutaka kuumia moyo kwakweli niliona yanini nijiumize na mtu nipo nae ndani kila siku? Hao michepuko tuu mama mjengo nimetulia hapa najiambia maneno hayo wakati hata ile ahadi ya nitakuoa sina achilia mbali pete ya uchumba lakini mie tena nimezama nimedumbukia kwenye penzi la zikko huniambii wala unishauri yani hakuna habari utanambia kuhusu zikko nikakuelewa basi nikajichanga changa nikanunua gari yani ikumbukwe hapo mie ndo mume maana zikko ninamlisha nina mvisha sijui pesa ya kunyoa na takataka zote nampa mimi kwaiyo iyo jeuri hapo mjini anaitoa kwangu.
Nilinunua gari na kiwanja kwa pesa nilizo kuwa nadunduiza dunduiza zikko alifurahi sana na akanipongeza sana ila kuhusu kiwanja hakua amejua basi akanishauri tufanye party ya kusherekea mafanikio tumepiga hatua sijui nini na nini haya tukafanya party tu tukachoma nyama vinywaji vikanunuliwa na tuka alika watu wetu wa karibu inshort ilikua party flani ya kishua kuja kwa code😊 basi mimi nilialika wafanyakazi wenzangu pamoja na boss wangu maana kiukweli tofauti na kazini sikuwa na marafiki mimi ni yule mtu wa kushinda ndani tuu.. zikko nae alialika alio wajua na nyama choma party ikawa nzuri tuu.. hakukua na mc ila kulikua na mziki wa chini chini wafanyakazi wenzangu walika na couples zao walio kuwa single walikuja na rafiki zao party ilifanyika nyumbani.
Katikati ya party nlikiona kibinti kimoja yani bado hakija jielewa vizuri hata mavazi yake yanaonesha tu kwamba huyu bado ana safari ndefu tu katikati ukuaji na kujielewa ila sikumfatilia sana muda ule wakati namwangalia huyo binti alikuja boss wangu akasema "Don't tell me ulikua hivyo few years back" nikacheka nikamwambia "Hell no.. i was better than that" tukacheka nageuka kumwangalia tena sijamuona baadae namuona akiwa pamoja na zikko wanazungumza nikamsogelea nikamsalimia zikko akasema "Huyu ni girlfriend wa Martin ila martin katoka kidogo huyu anaoneka ana waswas kwaiyo ndo niko nae hapa" nikamwambia "Sawa" wakati najichanganya namuona Martin yupo kwenye kona ana mkiss mwanamke nikajisemea duh huyu anajiamini nn kuja na wanawake wawili kwenye party moja na sijui wanampendea nn sura Hana mwili mbovu na pesa ndo kabisa eh jaman wanawake sisi kweli tuna huruma akaja tena boss wangu akasema "you know what you look gorgeous tonight I'd like to date you" nikamwambia kiutani "Just because of tonight? Is it the dress.. shoes or make up?" Akasema "Girl your perfect tonight" nikatabasumu nikamwambia "I'm sorry but I'm taken" pale pale akaja zikko akanishika kiuno akamsalimia boss wangu akasema "mimi ni boyfriend wa asia" boss akasema "ouch! Boyfriend not married yet so there's a big chance i can turn them tables" nikamwambia "Nah you don't stand a chance" akacheka sana huku anaondoka akasema "In case you changed your mind you know where to find me" zikko akasema "Mnaongelea nini?" Nikamwambia "usijali baby nika mkiss" ghafla si ndo kile kibinti kinaibuka..
Kwanini una mkiss bwana angu.. Eeh what? Yani nilijikua mwenyewe nashangaa zikko akasema "Ren hebu usiwe hivo" yule binti kaanza kutukana yani pale ndo nikajua kabisa huyu hata miaka 20 hajafika watu wakasogea pale "nini tatizo?" Yule mtoto nadhani hakua anajua kama ye ndo mwizi akaanza kuropoka "Si huyu Malaya analeta leta mazoea kwa wanaume za watu" yani kwakweli ilikua ni aibu kweli maana watu wote walio kua pale ni watu ambao nawaheshimu kwa kweli nikawa tu natoka eneo lile maana nilikua na hasira na nime aibika mtu ninae jisifu kuwa ndo mpenzi wangu anafanya mambo ya kunidhalilisha kwakweli nilijiskia vibaya sana.. Yule mtoto alitukana sana akatokea dada mmoja anaitwa maggie akamshika yule mtoto kumtoa nje yule mtoto akamsukuma akamwambia "Niache na wewe" yule dada akamkata kofi moja yule mtoto aka kaa kimya akamvuta akamtoa nje huku anaita "Zikko.. zikko.. Unaona zikko.. sikubali kudadeki" kakatolewa nje alafu yule dada akamfata zikko akamwambia "Ukimtaka utamfata" zikko akanisogelea sikutaka mambo yawe mengi nikasimama nikasema "Ladies and Gents samahanini kwa kilicho tokea ila anyways nadhani party imeisha mtaendelea ku enjoy drinks na nyama hizo ukiona muda wa kuondoka umefika your allowed.. I'm very tired I'll go inside now thank you for coming" nikaondoka hakuna alisema chochote nliingia ndani nikapokea msg kutoka kwa boss wangu "In case you change your mind" nikazima simu..
Nikavua nguo nikaenda bafuni kuoga watu nje walikua wanaendelea kunywa na kula nyama choma nilivo maliza kuoga nilipanda kitandani nikalala badae mida ya saa nane naskia mtu ananisukuma sukuma "Mke wangu umelala?" Nikageukia upande mwingine akasema "mke wangu party imeisha" nikasema "Ok" nikavuta shuka nikajifunika "Mke wangu amka tuongee basi" niliongea kwa sauti kubwa na ya ukali "Tuongee kuhusu nini? Hebu niache bwana alaaaah" akasema "sasa kwanini unapaza sauti?" Nikamwambia "Wewe si umenikuta nimelala hebu usinipe tabu sijui unaniskia niache tu nilale kwa amani" akaendelea kuongea ongea nikaona ananitia hasira tuu maana sikuwa na mood ya kuongea nae kama ananikera tu nikanyanyuka pale nikachukua shuka nikaenda sebuleni na nikafunga mlango wa sebuleni kwaiyo ye akabaki chumbani mimi nikalala chumbani..
Asubuhi nikajiandaa niende kazini ye hakuwepo chumbani mimi nimemaliza kuvaa natoka kwenda kazini gari hamna kaondoka nalo nilichukia sana ila nika amua tu niende kazini..
Badae nimetoka kazini narudi nyumbani nikakuta gari lipo nikajua zikko karudi.. sikuwa na habari nae nikafanya mambo yangu tu nikapika chakula nikamkaribisha akaja kula ananisemesha mimi sina habari nae.. Badae nikawa nataka kutoka akasema "nitatumia gari natoka" nikamwambia "Nunua lako baba utumie mie pia nataka kutumia gari" akanyamaza kimya nikaoga nikavaa suruali yangu na tishert na sendos nikaingia kwenye gari nikawasha kuelekea bar napenda tu zile kelele za bar watu wanakunywa na nini basi ndo naenjoy
Wakati niko njiani nilikia zebra crossing nafunga break ili watu wavuke kikandoka ki wallet cha kike ila sikujali sana nikaendelea na safari yangu nafika nikashuka nimefika counter nikakumbuka nimesahau simu narudi kwenye gari tafuta simu huku na huku katika harakati hizo mbona kama kuna kitu nimeshika nyuma ya siti yaani kutoa mkono natoka na condom.. Tena imetumika
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment