Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

STORY:PENZI GUMU EPISODE 02

Free Images : man, person, music, woman, male, love, africa ...

Basi sikuwa na namna na sikutaka kufunga duka langu maana ndo lilikua limeanza kuchangamka kwaiyo nilimtafuta yule kijana nikamuomba aje dukani tuongee..
Alikuja nikamwambia "Nnaombe ukae hapa dukani maana mimi nitaanza kufanya kazi siku si nyingi" akasema "Sawa sister mimi niko tayari lakini sasa ulisema mpka nijipange mimi sijajipanga bado nifanyeje?" Nikamwambia "Unajua mimi nimepanga chumba  kimoja" akasema "Sister mimi ntalala hata chini au kma vipi basi nitalala hata dukani" nikamuuliza "Utaweza kulala dukani kweli?" Akasema "Ndio sister mimi sijali" nikasema "sawa kama kuna vitu utahitaji kwenda kuchukua kachukue uanze kazi rasmi" akasema "Amna chochote nitaanza leo" nikasema poa..

Tukawa tumekubaliana na malipo mimi nikatoka na kumuacha pale dukani maana kila kitu nlikua nimesha muelekeza.. Nilienda kumnunulia baadhi ya viti muhimu mswaki dawa ya meno na sabuni kisha nikanunua na chakula nikamuachia pale mimi nikaenda zangu nyumbani nikamwambia tarudi baadae..

Nilienda nyumbani nikampuzika kidogo na baadae usiku mda wa kufunga nikarudi dukani kuangalia mambo yanaendaje.. Nikamkuta Zikko bado hajafunga nilikua nimempelekea chakula alifurahi kuniona akasema "Sister mbona umekuja hapa saiv?" Nikamwambia "Na wewe mbona hajafunga mpaka saiv sa nne?" Akasema "Bado kulikua na wateja" nikamwambia "Utachoka sana ikifika tu sa nne ufunge pesa hazitoshagi" akasema "Sawa" nikawa namwelekeza jinsi ya jinsi ya kufunga tukafunga nikampa chakula akawa anakula.

Ila sasa yaani kila nikiangalia mazingira ya humu dukani sioni angle ambayo atalala yani naona kumebana bana ila sikuwa na namna hata nikisema nimnunulie godoro hakuna pa kuliweka yaan ndani humu kumebana bana sana ila sikuwa na namna yoyote ya kufanya baada ya pale nilimwambia afungue duka sa tatu na nusu mimi nitakuja asubuhi kisha nikaondoka zangu..

Asbuhi wakati najiandaa kwenda kule dukani nilipigiwa simu kwenda kule ambako ndo nimepangiwa kwenda kufanya kazi kwaiyo nilimpigia simu zikko nikamwambia aendelee tu na shughuli za dukani mimi nitachelewa akasema sawa.. Nikaelekea kule na nilipo fika nikaambiwa nianze kazi immediately yani kesho nikienda niende kwa ajili ya kuanza kazi maana alie kuwa kwenye nafasi ile hayupo tena kwaiyo nafasi haiwezi kubaki wazi kwa mda mrefu sikuwa na pingamizi maana hakuna chochote ambacho kingeweza kunifanya nichelewe kuanza kazi na hata hivyo nlikua excited kuanza kazi muda wowote maana tangu nimemaliza chuo sikuwa nimefanya kazi ambayo nilikua naipenda.. kwaiyo niliondoka ili kujiandaa na kuanza kazi kesho yake..

Nilipita dukani na kumwambia Zikko kuhusiana na hali halisi kwiayo itabidi tu yeye aendelee.. Zikko nilitokea kumuamini katika mda mfupi sana kwanza ni mtu mwenye utii na ni mnyenyekevu ni kijana wa rika langu lakini jinsi alivyo kua ana nitii na kuninyenyekea basi nilivutiwa nae na kumuamini zaid..
Nilianza kazi na kweli nilikua busy sana na muda wa kwenda kule dukani sikua nao kabisa ila zikko nilikua tu nawasialiana nae kupitia simu na kama kuna kitu alitaka kujua nilikua nampa maelekezo kupitia simu..

Baada kama ya wiki nilienda dukani nilipo pata muda kuangalia mambo yanaendaje na kwakwel mambo yalikua yanaenda vizuri tu ila tatizo lilikua kwa zikko yani ana vipele vya mbu kwanzia usoni na mikononi nilimhurumia na alikua ana jituma sana kiasi kwamba nilimhurumia.. ilipo fika jioni nikamwambia "funga" akasema "Sawa sister ukitoka nitafunga" nikamwambia "Funga kwa nje tunatoka wote" akasema "Sawa" akafunga alipo maliza  tukaondoka akasema "Sister mimi naenda wapi?" Nikamwambia "Kwangu"  akasema "kwanini kuna kitu nimekosea sister" nikamwambia "Zikko unako lala kuna mbu sana eeh na pia kanafasi kale yani siwezi hata ku imagine unalalaje" akanyamaza nikamwambia "Kwanzia leo utakua unakaa kwangu sawa?" Akasema "Nashukuru sana sister"

Stoory ndo ina anzaaaa sasaaa..
Mimi na zikko nyumba moja? Eti wahenga walisema hakuna urafiki wa mwanamke na mwanaume? Ni kweli?  Je urafiki wa boss na mfanyakazi wake nao haupo?


  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4