Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

STORY: PENZI GUMU EPISODE 03

Free Images : man, person, music, woman, male, love, africa ...

Tulifika nyumbani yani zikko alikua anashangaa kila anacho kiona mh nikawa najiuliza kuna kipya kipi ambacho anashangaa..Nikawa naandaa chakula kwakua mda ulikua umeenda nliona nipike tu ugali na kulikua na samaki kwenye friji kwaiyo nikamua tu nimchemshe fasta fasta nikamkatia katia na nyanya na kitunguu basi tukala na baada ya hapo ni kuoga na kulala..
Nikamwambia "Si ulisema hata chini unalala?" Akasema "Ndio sister" nikamwambia "kwani una miaka mingapi?" Akasema "Kwanini?" Nikamwambia "Unavo niita sister" akasema "Mimi nna miaka 24" nikamwambia "Niite tu Asia" akasema "kwani we una miaka mingapi?" Nikamwambia "mm nna 25" akasema "Sawa" nikachukua khanga na nguo zangu zangu za kulalia nikaenda kuoga na kubadilisha nguo huko huko..

Nikarudi nika mwelekeza zikko bafuni akaenda kuoga alivo rudi nikampa mashuka mawili na mto chini kulikua na carpet na mimi nikapanda kitandani nikalala..

Maisha yalienda hivo na hakukua na tabu yoyote yani tulielewana sana mimi na zikko na tukawa kma ndugu sasa..ila majirani hawaamin kama hakuna chochote kati yetu wanadhani labda tuna mahusiano.. kazi yangu nilikua nafanya vizuri huku dukani nako kunaendelea vzr kwa ufupi mambo yalienda vzr mno..

Baada ya muda kupita alitokea kaka mmoja na kuonesha nia ya kutaka kunioa na kuishi pamoja sikuwa na kipingamizi maana hata ivyo nilikua tayari kwa ajili ya ndoa na umri wangu pia ulikua una ruhusu kwaiyo sikuona shida yoyote.. Nilikua bado naishi na zikko kama kaka na dada kwakweli niliona kama nimepata familia tulielewana mno na tulisaidiana sana kiasi kwamba nilikua nafikiria kupanga nyumba kubwa ili tuishi vizuri kwa amani ile hali ya kulala chumba kimoja yeye chini mie kitandani siku ipenda na pia ile hali ya majirani kuona kwamba naishi na mwanaume kana kwamba ni mpenzi wangu siku ipenda pia ila sikua na namna hivyo nilitaka kupanga nyumba kubwa tuishi kama familia.

Baada ya kupata mchumba na kuonyesha nia nilimwambia zikko iyo siku jion baada ya kuwa tumetoka kwenye shughuli zetu.. "Zikko kuna kitu nataka kukwambia" akasema "Subiri kwanza nikaoge alafu tuje kuongea vzr mie naskia kuwashwa washa tu hapa" nikamwambia "Haya poa" akaenda kuoga na mimi nikawa naandaa chakula..
Baada ya pale sasa wakati wa kula akasema "Enhee ni nini ulitaka kusema?" Nikawa natabasamu akasema "Sura yako inafuraha inaonyesha ni kitu kizuri..Umepandishwa cheo nini?" Nikacheka nikamwambia "Unaumwa wewe kwaiyo kupandishwa cheo ndo kitu pekee kinachoweza kunifanya niwe na furaha?"akasema "Haya kama kuna kingine niambie" nikamwambia "Nimepata mchumba" akasema "Mchumbaa??" Kwa mshangao nikamwambia "Ndio mchumba na yuko tayari kufata taratibu zote tufunge ndoa" sura yake haikua na furaha sana ila akasema "Sawa" nikamwambia "Hee yani hivo tu?" Akasema "Ndio sa nisemeje mchumba si wako au?" Nikamwambia "Yani mie nlivo kuwa na furaha nikajua nikikwambia utafurahi lakini naona sio nlivo tarajia" akasema "ulitarajia nini? Niruke ruke nishangilie? Kwan naolewa mimi alafu mie nataka kulala" nikamwambia "Mbona kama hizi habari hazija kupendeza?" Akasema "Una amini katika mapenzi? Tena ya ndoa?" Nikamwambia "Ndio naamini" akasema "Endelea kuamini mimi nalala kesho niwahi dukani"

Nilishangazwa na mapokeo yake ila nikadhani labda ni kwa ajili anahofia nikiolewa labda yeye sitamjali tena au tamfukuza wakati amejifunika pale chini kwenye carpet amelala nikamwambia

"Zikko usijali kama una hofia sitakujali tena unakosea siwezi kukutupa" kwa mala ya kwanza tangu nimjue zikko leo ndo siku ya kwanza aliongea kwa hasira tena kwa kunipandishia sauti.. "Kwani mimi ni omba omba au? Kwanini unanichukulia kama omba omba Asia??!!!" Khaa aliongea mpka nikaogopa.. nikamwambia "Sio hivyo Zikko hujanielewa" akasema "Ukinipa mshahara wa mwezi huu taenda kupanga chumba" kisha akajifunika mpaka usoni..

Nilimsemesha sana lakini sikujibiwa hata moja hivyo niliona bora na mimi nipande kitandani nilale ila sikujua kwanini zikko amechukia kiasi kile..Ila nikajua kama kawaida yake akichukia usiku asubuhi ana amka bila kinyongo..

     Itaendelea..


  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4