Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

YANGA YAPIGA HESABU ZA KIMATAIFA KUBORESHA KIKOSI CHAO

YANGA YAPIGA HESABU ZA KIMATAIFA KUBORESHA KIKOSI CHAO
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unahitaji kusuka kikosi upya kitakacholeta ushindani kitaifa na kimataifa kwa kushusha nyota wengi wakali na wenye ujuzi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema kuwa mpango mkubwa kwa Yanga ni kuona inakuwa na kikosi cha kipekee msimu ujao.

"Malengo makubwa ni kuona kikosi cha Yanga msimu ujao kinakuwa ni cha kipekee na chenye nguvu kubwa ya kuleta ushindani.

"Yote yanawezekana kwa kuwa tayari tumetengeneza mazingira bora ambayo yatatupa nafasi ya kufanya vile ambavyo tunafikiria na inawezekana kufikia huko mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4