KOCHA SIMBA ATAJA SABABU YA KUTOELEWANA NA BENCHI LAKE LA UFUNDI
SVEN Vandernbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema haikuwa rahisi kufanya kazi na benchi la ufundi kutokana na kutozeana.
Sven alipoanza kazi ililipotiwa kuwa hakuwa na maelewano mazuri na Kocha Msaidizi, Seleman Matola jambo ambalo liliamuliwa na uongozi ili kumaliza tofauti zao.
Kocha huyo amesema kuwa ilikuwa ngumu kufanya kazi na benchi la ufundi mwanzoni ila kwa sasa tayari wamezoeana na maisha yanaendelea.
" Haikuwa kazi rahisi kufanya nao kazi pale mwanzo lakini ukiliangalia sasa utaona tunashirikiana sana na kila kitu kinakwenda vizuri," amesema.
Previous article
Leave Comments
Post a Comment