BEFORE I DIE SEHEMU YA 7
“Grace wazo lako ni zuri sana.lakini ukumbuke kuwa nilikwisha kuahidi kukusaidia kuyajenga maisha yako upya wewe na sabrina.Sijaisahau ahadi yangu.Hata nikiwatafutia kazi ya kufanya kwa sasa itakuwa ni kazi ambayo haitakuwa na maslahi yoyote kutokana na elimu yenu ndogo.Kwa maana hiyo lengo langu ni kwanza kuwapeleka shule mkaendelee na masomo halafu baada ya kusoma ndipo niwatafutie kazi.Nataka muanze elimu ya sekondari haraka iwezekanavyo mara tu shule zitakapofunguliwa.kwa sasa niko katika mchakato wa kutafuta shule na pindi nitakapoipata shule nzuri itakayoniridhis
ha nitakutaarifuni.Tafadhali msiwe na papara na haya maisha.Bado hamjachelewa.Umri wenu una ruhusu kabisa kuyatengeneza upya maisha yenu.Naahidi kuwasaidia kwa kila hali ili muweze kufanikisha malengo yenuo na kuwa na maisha mazuri siku za usoni.” Innocent akasema na kumfanya Grace atabasamu kwa furaha huku sura yake nzuri ikizungukwa na nuru ya matumaini ya maisha mapya.
ENDELEA………………………………
Asubuhi na mapema siku iliyofuata,kabla hajaanza kazi Joshua akaenda katika ofisi ya bosi wake kama alivyokuwa ameelekezwa siku iliyotangulia.Usiku mzima alikesha akiwaza kitendo cha bosi wake kutaka kufahamu mahala anakoishi na zaidi ya yote akamuachia shilingi elfu arobaini pesa ambayo hakuwa ameota kama angeipata kwa usiku ule.Kilichomuumiza kichwa ni kwamba jana alikutwa amelewa kiasi cha kushindwa kufanya kazi na meneja mwajiri alikwisha kusudia kumfukuza kazi.Hakuwa na uhakika kama bosi wake angeweza kumsamehe kwa kosa hilo.Asubuhi hii alikuwa mnyonge sana akijua lolote linaweza kutokea.Aidha kufukuzwa kazi au kupewa karipio kali. Saa moja na nusu juu ya alama Innocent akawasili na kuelekea moja kwa moja ofisini kwake.Katika sehemu wanayokaa wageni wanaosubiri kuonana naye alimkuta Joshua tayari amekwisha fika akimsubiri.Akamsalimu na kumkaribisha ndani.
“Ndiyo bwana Joshua habari za toka jana? Innocent akauliza huku akikoroga kikombe cha kahawa na kumpatia Joshua “Habari za toka jana nzuri bosi.” Joshua akajibu kwa sauti iliyojaa uoga.
‘Mama na watoto hawajambo? “Hawajambo bosi” Innocent akaweka vitu vyake mezani sawa sawa halafu akamtazama Joshua kwa sekunde kadhaa. “Joshua nimekuita asubuhi hii kuna mambo ambayo nataka tuyajadili mimi na wewe.Jana nililetewa barua ya kusaini kukufukuza kazi kwa kosa la kulewa kazini na kushindwa kufanya kazi.Kwa mujibu wa meneja maslahi, si mara ya kwanza kwa wewe kufanya kosa la namna hii.Wamekwisha kupa maonyo kadhaa lakini bado umeendelea na tabia hii ya ulevi kazini.Mimi nilikataa kusaini na nikamuomba meneja mwajiri anipe nafasi ya kukaa na kuongea na wewe ili nijue tatizo lako ni nini hadi unafikia hatua hii.Jana niliamua kwa makusudi kwenda kufahamu mahala unakoishi na jinsi gani unavyoyaendesha maisha yako.Kusema ukweli Joshua sijapendezwa na aina ya maisha unayoyaishi .Baada ya kujionea mimi mwenyewe maisha yako nimeguswa na niko hapa kwa ajili ya kukusaidia lakini kwa sharti moja tu kwamba unaniahidi utaachana kabisa na pombe.Joshua una watoto watatu kama ulivyonieleza na wote hao wanahitaji matunzo bora,elimu bora ambayo itawajengea msingi bora wa maisha yao.Watoto na familia yako wanahitaji kukaa katika nyumba nzuri na si ile unayoishi sasa.Yote haya yanaweza kufanyika iwapo utaachana na pombe.Kwa hiyo naomba uniahidi kama utaachana na pombe ili nione ni jinsi gani ya kuweza kukusaidia kwanza kupata nyumba bora na baadae kukuinua kiuchumi.” Joshua alishindwa kujizuia kutokwa na machozi kwa kauli ile ya Inocent kwamba anahitaji kumsaidia.Akapiga magoti na kukiri kwamba toka siku ile ameachana kabisa na ulevi wa kupindukia.Innocent akamruhusu kwenda kuendelea na kazi na kuahidi kumsaidia muda si mrefu ili maisha yake yaweze kuboreka.
MIAKA MIWILI BAADAE
Miaka miwili sasa imekatika toka Innocent akabidhiwe kampuni hii ya kutengeneza maji ya kunywa.Kwa muda huu mfupi kampuni ilikuwa imerudia hali yake ya kawaida .Uzalishaji uliongezeka na hivyo kuifanya kampuni kuwa na fedha za kutosha na kama alivyowaahidi wafanyakazi Innocent hakuchelewa kuanza kuongeza mishahara ya watumishi wake.Pamoja na kuongeza mishahara yao aliweza kuwawezesha pia kwa usafiri wa kuja kazini na kurudi majumbani kwao kwa kununua mabasi ya kampuni maalum kwa ajili ya wafanyakazi tu.Vile vile ilianzishwa shule ya chekechea kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi Kingine alichokuwa akitazamia kukifanya ni kuanza zoezi la kutoa mikopo ya nyumba kwa wafanyakazi wake ambao hawakuwa bado na nyumba za kuishi.Hali za maisha ya wafanyakazi wa kiwanda hiki zilianza kuboreka na kila mmoja alijisikia furaha kufanya kazi hapa.Kila mfanyakazi alikuwa akijituma kwa namna alivyoweza.ili kuweza kuogeza uzalishaji.Hii ikampa faraja sana Innocent ambaye kwa muda huu mfupi alitokea kupendwa na wafanyakazi kupita kiasi. Grace na Sabrina wote kwa pamoja walikwisha maliza masomo ya sekondari.Walisoma masomo ya sekondari katika ule mpango wa elimu ya sekondari kwa miaka miwili.Walikuwa na uhakika mkubwa wa kufaulu mitihani yao kwa sababu walikuwa na waalimu wazuri waliokuwa wakilipwa vizuri na Innocent ili kuhakikisha kwamba wasichana hawa wawili wanafaulu mitihani yao ya kidato cha nne. Ilikuwa ni siku ya jumamosi ,siku ya mapumziko ya wiki .Siku hii innocent aliamua kuitumia kwa kulala nyumbani .hakutaka kwenda kazini au sehemu yoyote ile.Mchana wakati akipumzika dada yake Sarah akaja na kumweleza kwamba alikuwa akihitaji kwenda katika klabu ya usiku ili kupoteza mawazo baada ya kazi nyingi za wiki nzima.Alikuwa akitaka kuongozana na Innocent kwa sababu hakuruhusiwa kutoka yeye mwenyewe kwenda sehemu za starehe nyakati za usiku.Innocent hakutaka kumyima raha dada yake akakubali kuongozana naye kwa usiku huo kuelekea Club peninsula moja kati ya klabu mpya na inayolitikisa jiji la Dar. Saa moja za jioni wakaanza safari ya kuelekea Klabu Peninsula.
“Inno kuna mahali tutapitia kwa ajili ya kuwachukua marafiki zangu wawili .Si unajua tunatakiwa tuwe na kampani ya kutosha.Tena nimekumbuka Lulu atakufaa kwa kampani ya usiku huu.” Sarah akasema huku akitabasamu “Sarah kila siku umekuwa ukinipigia kelele kuhusu huyo rafikiyo Lulu.Ni msichana wa namna gani huyo? “ Innocent akauliza.
“Inno,Lulu ni msichana ambaye nina uhakika anaweza akakufaa.Ni msomi,ni mrembo na ni hivi majuzi ametoka Urusi alikokuwa akichukua shahada yake ya udaktari.Nilimuahidi kukukutanisha nawe lakini naona leo ndiyo siku muafaka” Sarah akasema na kumfanya Inno acheke kwa nguvu. “Usinifurahishe sarah.Mwanamke wa ndoto zangu nitampata tu lakini si huyo Lulu wako unayempa sifa kama malaika.”
“Unasema hivyo kwa sababu bado hujaonana na Lulu.Nakuapia Inno ukimuona wewe mwenyewe utamkubali.Inakubidi kwa sasa utafute mchumba Innocent .wewe ni mtu mkubwa sasa hivi.” “nakubaliana nawe Sarah,mchumba nitatafuta lakini si kwa kutafutiwa.Bado nina muda mzuri na wakutosha wa kutafuta mtu nimtakaye.”
* * * *
Saa tatu kasoro wakawasili klabu Peninsula.Ilikuwa ni sehemu yenye pilika pilika nyingi kwa usiku huu.Sarah ambaye ndiye aliyekuwa dereva akawasha endiketa ya kushoto kuashiria kwamba alikuwa akielekea hapo klabuni.Wakati gari yao imesimama wakisubiri gari mbili zilizokuwa mbele ziingie ndani ghafla Innocent akaona wasichana wanne wamesimama chini ya nguzo ya umeme.Mavazi yao yalionyesha wazi kwamba walikuwa ni wasichana wanaofanya biashara ya ukahaba.Katikati yao alikuwepo msichana mmoja mwenye umbo dogo ambaye kwa msaada wa mwanga wa taa Innocent aliweza kulisoma vyema umbo lake.Alikuwa ni binti mdogo kuliko wote waliokuwa wamesimama pale.Alikuwa amevaa sketi fupi sana iliyoacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi.Alikuwa ameegemea nguzo ya umeme huku akipuliza moshi wa sigara.Sijui kwa nini Innocent alikuwa akimuangalia msichana yule namna ile. Wakati bado amekodoa macho kuwaangalia wasichana wale ,Sarah akakanyaga mafuta na gari yao ikaingia ndani .Bila kuchelewa wakakata tiketi na kuingia ukumbini.Innocent alikuwa mkimya sana na alionekana kutotulia ,kila mara alikuwa akiangalia saa yake.
“sarah naomba funguo za gari lako nakwenda kuwachukua rafiki zangu wawili nao waje ili tuwe na kampani ya kutosha kwa sababu naona hapa mwanaume niko peke yangu.” Innocent akasema na kuinuka akitoka nje ha kuwaacha Sarah na rafiki zake wakiangua kicheko kikubwa. Baada ya kutoka nje ya ukumbi moja kwa moja inno akaelekea mahala alikokuwa amewaona wale akina dada.Kwa sasa walikuwa wamebakia wawili pale chini ya nguzo.Akapumua baada ya kumuona yule msichana mdogo bado yupo.Taratibu akarudi na kupanda gari ,akaliwasha na kutoka nje ya geti.Akashusha kioo cha mbele halafu akaita “Psiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii…” wasichana kama sita hivi wakatimka na kulizingira gari lake.Kijasho kilikuwa kikimtoka kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuzingirwa na kundi la akina dada wanaouza miili yao.Aliogopa sana iwapo angeonekana na mtu yeyote anayemfahamu.Kwa haraka haraka akaangaza na kumuona yule binti aliyekuwa akimtaka bado ameegemea nguzo ya umeme . “Namtaka yule binti pale kwenye nguzo ya umeme.”Innocent akawaambia wale akina dada..
“Ouh kumbe hana meno huyu anataka kifaranga chenye nyama laini….” Mmoja wao akasema huku akiondoka.
“Uncle achana na kale katoto kameshalewa bangi halafu hakajui chochote kale.Cheki huu mzigo unavyolipa” Akasema mmoja wao huku akijizungusha na kumuonyesha Inno sehemu zake za makalio.Innocent hakutaka kuendelea kukaa pale kwa muda mrefu akatoa noti moja ya shilingi elfu kumi na kumpa mmoja wao. “kamata hii,niitie yule binti mdogo pale chini ya nguzo.” Mwanamke yule haraka haraka akaenda na kumleta binti yule,Innocent akafungua mlango akaingia na kuliondoa gari bila kuongea chochote.Innocent alikuwa akitokwa na jasho jingi.Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusimama na kuzingirwa na kundi la akina dada wanaouza miili yao.Katika maisha yake hakuwahi kuota kama iko siku atakuja kufanya kitendo kama kile.
“Hivi ni mimi kweli ndiye nimefanya kitu hiki? Siamini bado kama nimeweza kufanya kitendo kama hiki.Nashukuru Mungu sijaonwa na mtu yeyote anayenifahamu .Ni kitendo cha aibu kubwa.Sielewi kimenitokea kitu gani mpaka nikaamua kufanya kitu cha ajabu namna hii.Lakini sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya hii.Nisingeweza kumpata kirahisi binti huyu bila kujifanya ni mteja ninayehitaji huduma ya kimwili.Masikini binti mrembo kama huyu ni kwa nini aingie katika biashara ya kuuza mwili? Amekosa nini binti huyu mzuri hadi afikie hatua ya kuutoa sadaka mwili wake? Siwezi kuacha binti mrembo kama huyu apotee.I must do something.I must help her.” Innocent akawaza huku akimtazama binti yule aliyekuwa amekaa pembeni ambaye kwa sasa alikuwa akisinzia pale kitini.
“masikini anaonekana kama vile tayari amekwisha lewa.Inavyoonekana tayari atakuwa amefundishwa kutumia vilevi.Anatia huruma sana binti huyu.Hapana siwezi kukubali nitafanya lolote linalowezekana ili kumsaidia.Ni lazima nimtoe katika maisha haya anayoyaishi kwa gharama yoyote ile.” Innocent akawaza tena huku akimtazama binti yule mdogo mwenye uzuri wa asili uliofichika kutokana na aina ya maisha anayoyaishi.Haikuhitaji akili ya ziada kutambua kwamba binti yule alikuwa na uzuri wa kipekee kabisa lakini kutokana na maisha anayoyaishi uzuri wake tayari ulianza kufifia.
“Usiku huu nitaenda naye wapi? Nahitaji sehemu tulivu sana ambayo ninaweza kuwa na binti huyu kwa usiku huu .Ngoja niende naye 104 lodge.Ile ni moja kati ya sehemu tulivu sana.” Innocent akawaza huku akikanyaga pedeli ya mafuta na kulifanya gari liongeze mwendo.
TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment