Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 01


Review: 'Tyler Perry's Temptation' is very Perry, indeed - Los ...

Limbwata ni uchawi wa mapenzi unao tumika sana katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki. Lengo la uchawi huu ni kumpumbaza mwanaume na kumfanya asiseme chochote kwa mwanamke aliye mfanyia uchawi huu nakuisahau familia yake kabisa.Kwa mujibu wa maelezo ya Sangoma mmoja mkazi wa Mkata, Handeni, Tanga. Nguvu ya uchawi wa limbwata ni kubwa mara mia ya nguvu ya uchawi mwingine wa mapenzi uitwao SHUNTAMA ( Ukaege ) unaotumiwa na Bukobian women (Wahaya).
Katika uchawi huu, mwanamke huchukua kipande cha nyama ya n'gombe, mbuzi,kuku au bata na kukiweka kwenye tupu yake ya mbele kwa muda wa siku saba.
Baada ya siku saba kukamilika, mwanamke huyo atakitoa kipande hicho cha nyama na kuchanganya na nyama nyingine ya kawaida pamoja na dawa maalumu ya kichawi na kupika kitoweo hicho kisha kumpa mwanaume ale.Mwanaume akisha kula chakula hicho, tayari anakuwa amesha shikwa na uchawi huo.Mwanaume huyu atampenda mwanamke huyo katika siku zote za maisha yake na atafanya kitu chochote kile ambacho mwanamke huyo atamtaka kukifanya.Na Bahati mbaya dawa ya kumponya mtu aliyelishwa limbwata aina hii wataalamu ni wachache mno hivyo mara nyingi unakuta mhanga anakufa nalo.
 Wanaume wengi wameharibu maisha ya familia zao kwa sababu ya uchawi huu wa limbwata.




"Nilitaka kujua kwanini NYAMA HUWEKWA KWENYE PAPUCHI na sio sehemu nyingine yoyote ya mwili,"Lilikuwa ni swali la mwanadada Joyce akimuuliza rafiki yake kipenzi ambaye alimshauri amlishe limbwata aina hio mchepuko wake ili apate mali.
"Shogangu walatini wana msemo wao mmoja unasema, QUICI QUIDI VAGINA, SOLOSOLO CEDIT, wakimaanisha WHATEVER IS ATTACHED TO THE VAGINA, IT BECOMES A PART OF IT,Ama  CHOCHOTE KINACHOUNGANISH
WA NA PAPUCHI KINAKUWA SEHEMU YA PAPUCHI kwa maana nyingine kinakuwa  PAPUCHI KABISA,"Shogake Joyce alimjibu rafiki yake.

"MH! Nini maana ya kuwa PAPUCHI,"Joyce aliuliza tena.
"Kuwa papuchi maana yake ni kuwa mtu usiye julikana upo upande gani,unajua papuchi haijulikani iko upande gani.Kwa sababu mwanamke akisimama,inakaa mbele, akiinama inaelekea nyuma na akichuchumaa inarudi chini,na anaye weza kuamua papuchi ikae upande gani ni mwanamke mwenyewe,akitaka ikae mbele atasimama, akitaka irudi nyuma atainama na akitaka iende chini atachuchumaa.
So mwanaume aliye lishwa limbwata anakuwa amefanyika kuwa papuchi ya mwanamke aliye mlisha.Kwa maana nyingine basi huyu mwanamke ndie atakaye amua ni kitu gani huyu mwanaume anatakiwa kukifanya,kwa namna gani na kwa wakati gani
Hii ndio mantinki ya limbwata kupitishiwa kwenye papuchi ya mwanamke na ndio maana nakushauri umlishe mchepuko wako ili uisahau familia yake,"Shogake Joyce alimaliza kumjibu.
"Mh! Jamani kumbe zuri sana hilo limbwata yani nipeleke sasa hivi kwa huyo mganga akanipe nataka huyo mwanaume nimuendeshe nikombe kila kitu,"Aliongea Joyce.
"Hayo ndio maneno Shogake twende sasahivi kwa mtaalamu Razaki ukapate hio limbwata."
Hivyo ndivyo wanawake hao walivyoshauriana kwenda kwa mganga na wakaenda kweli,huko walipata dawa na mhusika ambaye ni Joyce akaja kumlisha mchepuko wake kama alivyoelekezwa na mtaalamu na kuanzia siku hio yule mwanaume akawa haongei kitu kwa Joyce ye kila kitu ni ndio tu hapana kwake mwiko.





MAMA WA KAMBO:01


Mama wa kambo ni story inayomhusu mtoto Linna,mtoto ambaye amepitia changamoto nyingi akiwa bado mdogo,tuanze mkasa huu mpaka mwisho.



Mamake Linna na Babake walioana mwaka 2009 mkoani Mbeya,Mamake alikuwa mtu wa Tanga na Babake mtu wa Moshi.

Mamake Linna alikuwa manager wa Bank na Babake alikuwa mfanyabiasha mkubwa wa mafuta.Mwaka 2010 walibahatika kupata mtoto mmoja wakike, walifurahi sana na wote kwa pamoja wakakubaliana wampe jina la Linna,jina ambalo lilikuwa la bibi yake Linna Mama wa babake ambaye ni marehemu kwa sasa.

Kila mmoja alionyesha upendo mkubwa kwa mtoto wao.
Walimpa huduma zote anazostahili mtoto ukizingatia pesa walikuwa nazo za kutosha.

Kadiri siku zilivyokuwa zinaenda na mtoto Linna alizidi kuwa mkubwa,baada ya miaka miwili aliacha kunyonya.Siku zilivyozidi kukatika mtoto Linna akawa anaweza kuongea japo kwa shida,maneno kama tata,Mwamwa,papa,Joli,hayakumpiga chenga mtoto Linna.

Wazazi wake furaha kwao iliongezeka,walimfungulia account bank wakamwekea milioni sitini mtoto wao kama zawadi.


Siku zilizidi kusogea mbele Linna akawa mkubwa,akawa anaweza kuongea vizuri,kula peke yake,wazazi wake walimtafutia mwalimu awe anamfundisha kusoma pale pale nyumbani,hawakutaka kumpeleka shule.Walitaka wawe karibu nae muda wote kama si Baba basi Mama,kwa upendo huo mtoto Linna alikuwa anadeka tu kwa wazazi wake.



Baada ya miezi tisa Linna alikuwa anajua kusoma na kuandika japo sio sana.
Alivyojua kusoma na kuandika wazazi wake walimpeleka shule moja jina Xx iliyopo Dar Es Salaam jiji la biashara.
Huko alianza kusoma kwa bidii sana mpaka kingereza akawa anajua kuongea nakuandika.

Wazazi wake walivyosikia anajua kuongea kingereza nakuandika walifurahi sana,wakamuahidi kumpeleka shule nzuri zaidi nje ya nchi masomo yake yote akasomee huko.

Ahadi hio mtoto Linna aliipenda sana nae aliwambia wazazi wake wampeleke huko walikoahidi mapema kabla mwaka haujaisha.
Walimjibu asihofu watafanya hivyo?.



Basi Linna aliendelea kusoma jijini Dar Es s Salaam huku akisubiri ahadi ya wazazi wake kwa hamu kubwa.
Muda wa likizo ulipofika baba ake alienda kumchukua akarudi nae jijini Mbeya.
"Baba,Mama yuko wapi?"Mtoto Linna alimuuliza babake baada ya kufika nyumbani kwao.
"Bado hajarudi toka kazini"Alijibu babake.

"Sawa ila Baba njaa inauma sana."

"Mwanangu nikupikie mayai au."

"Mayai sitaki."Alisema Linna.

"Mwanangu unataka nini sasa, ebu niambie sema unachotaka."

"Nataka kuku na chipsi."

"Sawa mwanangu naenda kukununulia."

"Sawa baba uwahi kurudi."

"Sasa hivi narudi." Alizungumza Baba Linna nakuondoka akimuacha mwanae peke yake.
Huku nyuma Linna aliwasha tv akaanza kuangalia.
Dakika kumi hazikuisha tangu babake aondoke mlango ulifunguliwa akaingia mamake Linna.
Linna aliinuka akamkimbilia nakumkumbatia.
"Wawooo mama shikamoo."

"Marahaba mwanangu za shuleni."

"Shuleni safi mis u mama jamani hata kuja kuniona mwanao,"Alideka Linna.

"Jamani mwanangu nisamehe nilikuwa busy kazini,"Alijitetea mama Linna.

"Mh! Mama kwahiyo hunipendi si ndio."

"Mwanangu nakupenda sana?"

"Kama unanipenda kwanini? Ulikuwa huji kuniona,"Linna alizidi kuuliza?.

"Nisamehe mwanangu,"Aliongea Mama Linna akionekana kusikitishwa na maneno aliyoongea mwanae kipenzi.

"Sawa Mama zawadi yangu ulisema."

"Mwanangu hata husahau."

"Mama mi siwezi kusahau siuliniambia nikukumbushe."

"Twende chumbani nikakupe."
Mama Linna alimbeba mwanae mpaka  chumbani nakumkalisha kwenye sofa.
"Mwanangu zawadi ninayokupa ni hii bahasha itunze sana ipo siku itakusaidia nikiwa sipo duniani na usimuonyeshe mtu yeyote,"Aliongea Mama Linna.

"Mama mimi nilijua unanipa nguo sasa unanipa bahasha mi yanini,"Alisema mtoto Linna asijue mamake ameweka nini mle ndani?.Lakini licha tu ya kutojua kwa umri wake alikuwa sahihi kabisa kwa alichoongea.

"Mwanangu we bado mdogo,yawezekana usione umhimu wa zawadi hii ila ukiwa mkubwa utajua na huko mbele itakuja kukusaidia,nakuwekea juu ya dari usimwambie mtu yeyote hata Baba usimwambie umesikia mwanangu,"
Aliongea Mama Linna.

"Mh! Sawa weka ila mi nataka nguo na chips mambo ya bahasha mi staki,"Alisema Linna akionekana kuchukia.

"Nguo nakupa wala usiwe na wasi wasi ila zingatia hii bahasha,"
Aliongea Mama Linna akimsisitiza mwanae juu ya ile Bahasha ambayo bado hatujui ndani kuna nini?.

Baada ya hapo Mama Linna alifungua kabati alitoa gauni zuri nakumpa mwanae.
Linna alifurahi sana.
"Asante sana Mama ndio maana nakupenda mwaaa."

"Mia pia mwanangu nakupenda sana."

"Aya mama mi naenda sebuleni kusubiri chips kuku toka kwa Baba."

"Nenda na mi nakuja."
Linna alitoka mle chumbani nakwenda chumbani kwake kuhifadhi gauni lake alilopewa na mamake.Alipoliweka alienda sebuleni kusubiri chips zake.

Baada ya muda  babake akarudi na chips kuku.

"Mwanangu nimenunua hizi hapa,"Alizungumza.

"Baba nilishe tena fanya upesi maana umechelewa sana,"Aliongea Linna kwa sauti ya kudeka maana walimzoesha hivyo?.

"Mwanangu we kula tu mi kuna sehemu naenda."

"Kama hutaki kunilisha mi siri machips yako."

"Atakulisha mamako mi nina haraka sana."

"Baba sitaki anilishe mama nataka wewe ndio unilishe,we si ndo umenunua."

"Mh! We mtoto uwage unasikia nimekwambia nina haraka."

"Baba we ndio husikii hutaki kunilisha mi mwanao."
Baba na mtoto wakawa wanabishana,Linna alikuwa sahihi kwa anachosema sababu tangu akiwa mdogo wazazi wake walimtengenezea mazingira ya kudeka na walipenda.

"Mama Linna ebu njoo umlishe mtoto,"
Baba Linna alimuita mkewe baada ya kuona Linna anataka amlishe wakati yeye kuna sehemu anaenda.


"Simtaki mama nataka wewe Baba,"Aliongea Linna.


"We baba Linna nini na mwanao,"Mama Linna alimuuliza mmewe.

Linna anataka nimlishe,ebu mlishe mi naenda ofisini mara moja,"Alijibiwa mama Linna.

"Aka mi sitaki mtoto anataka umlishe wewe babake,kwanza naenda jikoni kupika "Mama Linna alimwambia mmewe kisha akaenda zake jikoni.

"Baba kwahiyo hutaki,"Linna aliuliza?.

"Mwanangu nakulisha,"Baba Linna alinawa mikono nakuanza kumlisha mwanae.
Akiwa anamlisha mlinzi wa gheti alikuja.
"Bosi kuna mgeni,"Mlinzi alimwambia baba Linna.

"Mruhusu aingie."

Mlinzi alitoka nje punde mlango ulifunguliwa aliingia mdada umri kama wa Irene Uwoya ila ye alikuwa mzuri sana kama Jackiline Wolper.
Alivyoingia tu ajabu alimkumbatia Baba Linna na Linna akiwepo.
"Wawoo baby,jamani mbona umechelewa kuja kunipokea na vipi mkeo yupo,"Yule Dada aliongea haraka haraka na kuuliza?.

"Ndio yupo Dah! Inabidi tuwe makini sana,"Alijibu Baba Linna.


"Mh! Basi mwambie mi dadako,"Huyu dada alimwambia baba Linna na muda wote huo Linna alikuwa anawachora tu.Ukweli huyu Dada alikuwa ni mchepuko wa Baba Linna(Joyce)wa muda mrefu na kwa hatua hii walivuka mipaka kwani Baba Linna alimleta nyumbani kwake anapoishi na mkewe akidanganya kuwa ni Dada yake huku ukweli ukibaki pale pale kuwa sio Dadake bali ni mchepuko.

"Sawa baby namwambia hivyo usihofu,"Aliongea Baba Linna.


Uvumilivu ulimshinda Linna akaamua kumuuliza huyu dada kuwa kwanini? Hasalimii pia kwanini anamuita Babake baby.

"We kitoto tena ukae kim........ HUU NI MWANZO WA SIMULIZI HII AMBAYO



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4