MAMA WA KAMBO:02
Mwandishi Aneth
"We kitoto ebu kaa kimya? Muone kule masikio kama kenge mjane,"Aliongea yule Dada kwa ukali akimkaripia Linna.
"Baba eti mi kitoto nina masikio kama kenge,"Linna alimuuliza babake.
"Hapana mwanangu we mtoto mzuri sio kitoto alikuwa anakutania tu,"Alijibu Baba Linna.
"Aya baba na huyu ni nani?"
"Huyu ni Aunt yako anaitwa Baby ni mdogo wangu,"Baba Linna alimdanganya mwanae.
"Naenda kumwambia mama,kuwa huyu unamwita baby,"Alisema akiinuka sofani.
"Linna nitakupa na zawadi usimwambie mama sawa."
"Sitaki zawadi naenda kumwambia na chips zako siri kula mwenyewe na baby wako,"Linna alijitoa mikononi mwa babake akaenda jikoni ili amwambie mamake,alipofika jikoni na babake akawa amefika.
Ile nataka kuongea babake akamshika mkono.
"Mwanangu Linna ebu njo uku acha umbeya wako,"Aliambiwa Linna na Babake ili asiseme.
"Baba mi masikio kama kenge kweli,"Linna alimuuliza babake.
"Hapana mwanangu we msomi sio kenge,"Alijibu Babake akipotezea.
"Mme wangu kwanini unasema mtoto m,mbeya,"Baba Linna aliulizwa na mama Linna.
"Mke wangu we tulia mi na mwanangu tunajuana,halafu kuna mgeni njo mara moja nikutambulishe "
"Haya mme wangu nakuja sasa hivi ila hukuniambia mh!"Aliongea mama Linna.
Baba Linna alimshika mkono mwanae wakarudi sebuleni,walipofika walikaa Linna akaanza kulishwa kama awali.
"Baby huyo mtoto mbona anadeka sana,"Dada aliyetambulishwa kuwa ni mdogo mtu alimuuliza Baba Linna.
"Nampenda sana,anavyodeka najiskia furaha kwa sababu mi ndo babake,"Alijibu Baba Linna.
"Baby mi sijapenda unalidekeza mno ipo siku litajuta."
"Huyu kujuta hawezi labda niwe nimekufa."
"Baby usiseme hivyo hii ni dunia tunapita tu."
Wakati Baba Linna na huyu Dada wanaongea,Linna alikuwa anawasikiliza tu huku moyoni akisema lazima amwambie mamake.
"Mke wangu akifika nitamwambia we ni dadangu sawa."
"Sawa na jina uniite Joyce."
"Powa Joyce."
"Baba mi nimeshiba nipe juis"Aliongea Linna.
"Sawa mwanangu nakupa,"Aliinuka
nakuangalia kwa Linna,alipoona kama haoni akamkiss huyu dada.Kumbe Linna nae aliona ila alijifanya hajaona.
Alivyomkiss alienda kwenye friji alichukua juis akamimina kwenye glass nakumpa mwanae.
Baada ya nusu saa
mama Linna alikuja pale sebuleni alimsalimia huyu Dada mgeni.
"Habari ya saizi."
"Safi za hapa."
"Hapa nzuri karibu sana?"
"Asante wifi nimekaribia,"Alivyomsalimia mama Linna alikaa sofa alilokaa mwanae ili apate utambulisho toka kwa mmewe.
Baba Linna alianza kuongea huku akiona ona aibu.
"Mke wangu huyu anaitwa Joyce ni Mdogo wangu mtoto wa marehemu babamkubwa,kaja kutusalimia ataishi hapa kwa mda kisha anarudi chuo maana anasoma,"Mama Linna alidanganywa na mmewe kuwa mdogo wake wakati ni mchepuko na alifika hapo kwa lengo la kumdhuru Mama Linna ili aolewe yeye.
"Karibu wifi hapa ndo nyumbani na huyu ni Mwanetu anaitwa Linna,"Mama Linna aliongea asijue anamkaribisha shetani kwenye nyumba yake huku mwanae yupo kimya?.
"Asante wifi nimekaribia pia asante kwa kutuzalia mtoto mzur,i"Aliongea Joyce huku akimkonyeza Baba Linna kumaanisha dili limetiki.
"Jamani Asante sema Baba Linna hakuniambia ujio wako,"Aliongea mama Linna.
"Hilo halina shida mke wangu mambo mengi kikubwa amefika salama,"Alisema Baba Linna huku moyoni akifurahia mpango kwenda vizuri.
"Sawa basi niwaache kidogo kwa niandae chakula."
"Aya wifi yangu mi nipo na kaka na Aunt yangu Linna."
Mama Linna aliinuka ile anaanza kutembea mwanae akamuita.
"mamaaa!!"
"Unasemaje Linna."
"Mama huyu si wi...hata kabla hajatamka neno wifi Babake alimfinya bila mamake kugundua.Mtoto Linna alitaka amwambie mamake kuwa huyo aliyetambulishwa sio wifi ni mtu na baby wake lakini ndio hivyo tena akafinywa atulie.
"Mama,Baba ananifinya,"Linna alimwita Mamake ili amwambie kuwa Baba anamfinya lakini mamake akamwambiwa atulie asiwe msumbufu sana.Laiti angemsikiliza mwanae basi angejua ukweli lakini ndio alipuuzia nakwenda zake jikoni.
Sebuleni walibaki Linna,Baba na huyu dada.
"Linna nimekwambia acha umbeya,"Aliambiwa mtoto Linna na babake.
Linna alikaa kimya?.
"Halafu baby hili litoto silipendi yani lina mdomo sana,"Aliongea Joyce,Baba Linna akakaa kimya vijana wa kisasa wanasema no coment ndicho alichofanya Baba Linna.
"Baba namwambia mama kuwa huyu kasema hanipendi pia nina mdomo,"Alisema Linna.
"Mwanangu usimwambie nitakupa na zawadi hakusemi wewe,"Baba Linna alimtuliza mwanae,Linna alitulia lakini swala la kumwambia mamake lilikuwa pale pale.
Waliendelea kuongea vitu wanavyo vijua wao na moja ya mambo waliyokuwa wanaongea eti wamemisiana sana usiku wajitahidi waonane na baba Lina akamwahidi Joyce usiku ataenda ndani kwake.
Wakati wanaongea hayo na mengine mengi Linna alikuwa anawasikiliza tu,wao walijua yupo bize na game kumbe hapana masikio yametega wanachoongea.
"Umefeli Baba lazima nikufungie usitoke ndani mwa mama,"Aliongea Linna moyoni.
Baada ya saa moja mama Linna alikuja pale sebuleni nakuwakaribisha chakula.
"Aya wifi tunakuja,"Aliongea Joyce.
Mama Linna alitangulia sehemu ya kulia chakula.
Baba Linna na Joyce waliinuka nakwenda pahala pa kulia chakula.
Linna ye hakuinuka kwani muda huo alikuwa bize na game.
"Linna ebu njo kula."
"Mama niletee huku nakula kidogo tu,"Aliongea Linna.
"Huko sileti ebu njo hapa mezani fanya haraka,"Mamake aliongea kwa ukali mpaka Linna aliogopa?.
Basi aliacha kucheza game nakwenda,alikaa kwenye kiti mamake alimpakulia chakula akaanza kula.
"Lione kule hata husali,"Mama Linna alimsema mwanae akionekana kukerwa na kitendo cha mwanae kutosali.
Waliendelea kula,Mama Linna alitazamana na mwanae,
Baba nae alitazamana na Joyce.
Wakati wanaendelea kula Linna aliona babake anamkonyeza huyu dada,aliye mtambulisha kama dadake kumbe hapana?.
Linna aliangusha kijiko maksudi ili ainame aone wanafanya nini?.
"We unakulaje embu okota hicho kijiko,"Alisemwa Linna na mamake asijue mwanae yupo kwenye uchunguzi,Linna aliinama kuokota kijiko na kule kule chini akaona mkono wa babake umeshika miguu ya huyu dada.
Linna alibaki amekodoa macho tu,sauti ya mamake ndio iliyomshtua.
"We mtoto ebu inuka ule chakula kinapoa"
Linna aliinuka mamake akampa kijiko kingine akaendelea kula, hapo tayari tukio aliloliona akawa amejiahidi kumwambia mamake.
Na wakati wanaendelea kula Linna akawa anaona miguu ya babake(vidole vinachezea miguu ya huyu Joyce.
Kiukweli mama Linna angeona hichi kitendo nadhani huyu dada anae mwita wifi angemtimua muda muda huo huo kwa matendo aliyokuwa anafanya?.
Kwa mara nyingine tena Linna akaona huyu dada anamkonyeza babake.
"Mh! Mi namwambia mama,"Aliwaza Linna.
"Mama!"Linna alimuita mamake lakini alikatishwa.
"Ebu kula wewe nilikataza kuongea wakati unakula."
"Mama mi nakula ila baba na Aunt
wana..... Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment