Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 31


Here Comes The Movie About Africa's Most Scandalous Love Story ...



"Vizuri sana basi pumzika acha na si tupumzike maana tumechoka sana,"Aliongea Dokta na mama Linna ikabidi alale ingawa usingizi haukuja kabisa sababu alikuwa na mawazo juu ya mmewe kwa aliyomfanyia maana ni makubwa mno na hamna kosa alilomfanyia.
"Mwache kesho naenda bank nahamisha kila kitu sibakizi hata mia na uzuri account yake naijua ina milioni 851,"Aliongea Mama Linna moyoni akiwa mle chumbani amelala huku macho yanaangalia juu ya dari.



Mchungaji alionyeshwa chumba akaingia  kulala pia Dokta na mkewe Sophia nao  wakaenda kulala,huko chumbani wanandoa hawa kwa kua walikumbukana mno basi cha kwanza tu walivyoingia walikula kubwa ya wakubwa.Walipotosheka walioga nakulala maana Dokta alichoka sana.


Mama Linna nae kule chumbani kwake alizidi kuwaza tu,usingizi hakuuruhusu kabisa kiukweli.
Mpaka inafika asubuhi ye alikuwa anawaza tu mpaka aliposhtuliwa na Sophia Mama mwenye nyumba.
"Habari za asubuhi Mama Linna pia pole na uchovu,"Alisalimiwa na Sophia.
"Za asubuhi ni nzuri na uchovu bado nipo nao kiukweli,"Aliongea Mama Linna.
"Ok! Nimekuletea supu upate au unaoga kwanza."
"Asante sana naona nioge kisha nile pia jana Dokta alisema we ni muhasibu utanisaidia kuhusu swala la kuhamisha pesa,"Mama Linna alishukuru kwa supu nakuuliza swali.
"Yah! Mimi ni muhasibu wala usihofu nitakusaidia,account si ipo Nmb au,"Alijibu Sophia swali la Mama Linna nakuuliza.
"Ndio Nmb,"Alijibu Mama Linna.
"Ok! Basi leo we tulia ila kesho tutaenda wote bank,nataka leo ninavyorudi toka kazini nipitie kariakoo ninunue nguo zako pamoja na hijabu ukavae kesho,"Aliongea Sophia.
"Wawoooo asante sana yani ubarikiwe maana hapa sina nguo hata moja ni hizi tu zilizopo mwili ni nazo itabidi nichome tu maana zimeingia kwenye jeneza,"Aliongea Mama Linna kwa furaha kidogo ingawa ilikuwa ya kulazimisha.
"Wala usihofu saizi uoge taulo hili na ukirudi nakupa dira uvae hizo ulizovaa tutachoma."
"Sawa nashukuru sana."
Basi Mama Linna aliingia bafuni akaoga tu mwilini,kichwani na usoni alifuta tu sababu alikuwa na kidonda.
Alipomaliza alijifuta nakurudi chumbani ambapo tayari alikuta Sophia kamuwekea mafuta na dira,alipaka mafuta akavaa nakuanza kula supu ya kuku na chapati.
Akiwa anaendelea kula akasikia hodi,kwa kua sauti aliijua kuwa ni Dokta basi alikaribisha.
Hakuwa Dokta pekeake aliyeingia bali aliongozana na Mchungaji.
"Karibu sana jamani pia poleni na uchovu wa kumuokoa Mama Linna,"Aliongea Mama Linna huku akionyesha tabasamu.
"Si tuko vizuri hofu kwako tu mwenye majanga,"Aliongea Mchungaji.
"Hahaha mi pia kama mnavyoniona nipo kula supu iliyopikwa na Mama Dokta,"Alicheka Mama Linna nakuongea.
"Aah! Tunakuona,aisee kwanza tumshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kuwa na moyo wa kukuokoa pia kwa kutufikisha salama nakuamka salama,"Aliongea Dokta.
"Amen Dokta na Baba Mchungaji nawashukuru sana na muendelee na moyo huo huo,"Alisema Mama Linna.
"Asante Mama Linna itakuwa hivyo,kubwa la si kuongea kwa sasa nikukuaga wenzio tunarudi Mbeya tukaendelee na majukumu pia tukuombe tu uishi hapa hapa na mke wangu wala usihofu kabisa chochote unachotaka mwambie au tuwasiliane,"Aliongea Dokta.
"Asante sana Dokta na Mchungaji,nashukuru kwa kunipa ruhusa kuishi hapa kwa muda wakati mipango mingine inaendelea,"Aliongea Mama Linna akishukuru.
"Wala usihofu hapa kuwa huru tu mke wangu anaishi na mfanyakazi tu watoto wetu watatu wapo shule za bweni hivyo mtakuwa nyie tu."
"Asante sana jamani pia niwaombe tu hili gari mlilokuja nalo mliache nyi nawapa kadi ya bank maana wakati naanguka kule Mbeya nyumbani card niliiweka mfukoni na Bahati nzuri wakati mnaniokoa haikuanguka hivyo hii hapa namba ya siri hii mkachukue pesa milioni 100 mgawane,kila mmoja anunue gari analotaka na mkinunua muwape madereva wa IT wapeleke Mbeya wawaletee nyi mpande ndege muwahi,"Aliongea Mama Linna na muda huo Sophia alikuwa mle mle ndani na alisikia yote,na ndipo akajua Mama Linna kumbe anapesa nyingi si mwenzie licha ya yeye kuwa na pesa lakini hamfikii Mama Linna.
"Jamani asante Mama Linna kwa hio zawadi,tukushukuru sana jamani,"Waliongea Mchungaji na Dokta.
"Wala msihofu haya ndio malipo ya kuwa na wema mzuri,"Aliongea Mama Linna nakuwapa card ile ya bank.
Basi waliongea kidogo kisha wakaenda huko bank wakiongozana na mkewe,walipofika kupitia mkewe Sophia waliangalia account ya Mama Linna wakakuta ina milioni 200 na basi wakahamishia kwao ile 100 waliyoambiwa ambapo kila mmoja ilikuwa ni 50m 50m.
"Kwa hio mme wangu unaenda kununua gari gani,"Mkewe Sophia alimuuliza mmewe Dokta.
"Mke wangu mi na mwenzangu Dokta tumekubaliana tunanunua Ist tu ya bei rahisi na pesa zinazobaki zitafanya mambo mengine au unasemaje,"Dokta alijibu swali la mkewe.
"Kweli kabisa mme mtakuwa mmefanya vizuri,basi muwahi mkanunue ili mkapande ndege ya saa6."
"Sawa mke wangu na kwa kua si nyumbani haturudi basi card hii ukampe Mama pia mshukuru sana,"Aliongea Dokta nakukabidhi card kisha ye na Mchungaji wakaenda sehemu wanayouza magari,wakachagua Ist mbili wakalipia kwa kuhamisha pesa bank kupitia simu pia wakalipia gharama za madereva watakaopeleka Mbeya.Walipomaliza walienda airport,huko walifanya taratibu zote ikiwemo kukata ticket na Bahati nzuri walifanikiwa.
Saa5 na dakika 45 tayari walikuwa ndani ya ndege bombadia,ilipofika saa6 kamili ndege ilipaa nakuanza kukata mawimbi kuelekea Mbeya.


Huku nyuma mke wa Dokta alifanya kazi zake,muda wa kurudi nyumbani ulifika alifunga ofisi yake nakwenda kariakoo.Huko alinunua nguo za Mama Linna za kutosha pamoja na hijabu kumi rangi tofauti,alipomaliza alinunua simu janja pamoja na line (sim card) kisha akarudi nyumbani kwake akiwa na furaha.
Ilimchukua nusu saa tu mpaka kufika na alipofika alipoingia chumbani kwa mama Linna ajabu hakumkuta.
Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4