MAMA WA KAMBO 32

Huku nyuma mke wa Dokta alifanya kazi zake,muda wa kurudi nyumbani ulifika alifunga ofisi yake nakwenda kariakoo.Huko alinunua nguo za Mama Linna za kutosha pamoja na hijabu kumi rangi tofauti,alipomaliza alinunua simu janja pamoja na line (sim card) kisha akarudi nyumbani kwake akiwa na furaha.
Ilimchukua nusu saa tu mpaka kufika na alipofika alipoingia chumbani kwa mama Linna ajabu hakumkuta.
"Jamani ameenda wapi huyu,"Alijiuliza Sophia akiweka mfuko wa nguo pale kitandani,ile anatoka Mama Linna nae akatokea.
"Jamani za saizi nikajua umetoka,"Aliongea Sophia huku akirudi chumbani.
"Nitoke niende wapi,siwezi jamani nilikuwa nachoma zile nguo huko nyuma,"Alisema Mama Linna akikaa kitandani.
"Ooh! Sawa basi vizuri,nguo hizi hapa nimenunua pamoja na simu pia card hii na wao wameshaenda na wameshukuru sana,"Aliongea Sophia akimpa ule mfuko wa nguo,simu na card.
"Wawoooo jamani asante sana jamani Mungu akubariki sana,"Alishukuru Mama Linna nakumkumbatia Sophia.
"Amen."
"Yani asante jamani,sijui umenunua ngapi nikurudishie,"Aliuliza Mama Linna akianza kujaribu zile nguo.
"Kuwa na amani tu mi nimekununulia,"Alisema Sophia.
Basi waliongea mengi mle chumbani na baada ya muda wakaenda sebuleni kupata vinywaji laini(soft drink).
"Kesho tutaenda wote bank ukahamishe pesa zote maana yule mwanamke wamesema mi hatari anaweza tuwahi,"Aliongea Sophia akimwambia Mama Linna pale sebuleni.
"Haswaa tena nimepata wazo,inabidi zile pesa niwe kama nimetoa ionekane mwenye account alitoa maana tukisema tuhamishe siku akiangalia atajua account iliyohamishwa,hivyo tutoe kisha niingize kwenye account yangu hapo kujua itakua ngumu,"Aliongea Mama Linna.
"Aisee umeongea point sana,hilo mi sikufikiria kabisa hivi ulikuwa unafanya kazi gani?."Aliulizwa Mama Linna.
"Mimi nilikuwa manager wa bank,"Alijibu Mama Linna.
"Mh! Ndio maana umeongea hili wazo."
"Jamani kawaida tu."
"Upo vizuri basi kwa kua mi ndio mhasibu kesho tutamaliza mchezo halafu unatulia,"Aliongea Sophia akimhakikishia Mama Linna kuwa watafanikiwa,waliendelea kunywa vinywaji muda wa chakula ulipofika walikula wakakesha kidogo kisha wakaenda kulala.
Dokta na Mchungaji nao walifika jijini Mbeya salama kabisa,walipofika kila mmoja alienda kwake maana walikuwa wamechoka mno.
Mchungaji ye alipofika kwake alikaa kidogo kisha akaenda nyumbani kwa Baba Linna kujua nini kinaendelea maana haikuwa mbali toka kwake.
Ilimchukua robo saa mpaka kufika,ajabu alipofika alikuta watu hamna kabisa wapo tu wenyeji yani Linna,Babake,Mlinzi Masai na Joyce Mama mpya mwenye nyumba.
"Jamani watu wameondoka wote wamewaacha pekeenu,"Aliuliza Dokta baada salamu kupita.
"Msiba siumeisha wakae hapa kufanyaje?,"Aliongea Joyce kwa dharau akimjibu Mchungaji.
"Ni kweli umeisha lakini ni mapema mno marafiki na majirani kuwaacha pekeenu hivi,"Alisema Mchungaji kwa sauti ya upole.
"Baba Mchungaji naona nawewe huna kazi ya kufanya ebu nawewe rudi nyumbani ukafue hata nguo za mkeo maana unatutia kinyaa tu,"Aliongea Joyce kwa dharau,kwa kua Mchungaji alishajua tabia ya huyu mwanamke basi kwa maneno yake wala hata hayakumpa tabu.
"Baba Linna unaruhusu ndugu yako anitukane mbele yako,"Aliulizwa Baba Linna.
"Lakini Baba Mchungaji msiba siumeisha we jikatae tu rudi nyumbani,"Alijibu Baba Linna akimsanifu Mchungaji.
"Ok! Narudi nyumbani samahani kama nimewakosea,Linna uwe unakuja kusali sawa mwanangu,"Aliongea Mchungaji akisimama nakuanza kutoka nje.
"Sawa Mchungaji nitakuwa nakuja pia ni....Hata kabla hajamaliza kuongea mtoto Linna alikatishwa na Joyce kwa sauti ya ukali.
"Kimya wewe tuondolee upumbavu hapa,unamjua wewe huyo.Huyo ni mchawi sana."
Maneno ya Joyce akimfokea Linna Mchungaji aliyasikia vizuri kabisa na hakutaka kujibu kabisa zaidi tu alisema moyoni kuwa abarikiwe.
Mchungaji alitoka nje kabisa akampigia Dokta nakumwambia kila kitu alichoona,kusikia na kuambiwa na mwisho akahitimisha kwa kusema yule mwanamke ni hatari jamaa haongei kabisa.
"Mi nilijua tu yule mwanamke ni shetani kabisa dah,sema powa tutaongea kesho acha mi nilale maana nimechoka sana,"Aliongea Dokta simuni baada ya kupewa story kuhusu nyumbani kwa Baba Linna.
"Sawa ndugu yangu basi kesho,"Aliongea Mchungaji nakukata simu.
Huku nyuma nyumbani kwa Baba Linna baada ya Mchungaji kuondoka Baba Linna na Joyce walianza kumpiga mtoto Linna na kosa lake eti hana adabu mbele yao.
Linna alipigwa sana huku akiwaomba wamsamehe lakini wapi walizidi kumpiga mpaka walipohakikisha amezimia ndio wakamuacha.
Baba Linna kweli limbwata likuwa on maana sasa alikuwa kama zezeta kila anachoambiwa ye ndio tu na si hapana.
"Mme wangu twende tukalale bhana,halafu kesho mdogo wangu anakuja tuishi nae hapa sawa baby,"Aliongea Joyce akimdekea Baba Linna,na ukweli hakua mdogo bali ni mpenzi wake asali wa moyo wake Mr Thanga ambaye wamepanga kumdhuru Baba Linna na wao kubaki na mali.
"Sawa mke wangu aje tu tuishi nae."
Baba Linna alikubali asijue anamkaribisha fisi buchani ambaye ni hatari.
"Sawa baby ndio maana nakupenda sana,"Aliongea Joyce kisha wakaingia chumbani huku wakimwacha mtoto Linna pale sebuleni akiwa amezimia.
Baada ya kuingia Chumbani Baba Linna alikula burudani moja nakulala fofofo.
Joyce hakulala kwanza aliamka nakumpigia Thanga kuwa aje usiku kuna ishu inabidi wapange asubuhi ikamilishwe.
Thanga kuambiwa hivyo akakubali kufika nyumbani kwa Baba Linna dakika 20 zijazo,kweli zilipofika Thanga akawa amefika mpaka ndani?.
"Vipi baby ishu gani tena halafu hapa nahamia lini jamani,"Thanga alimuuliza Joyce.
"Kuhusu kuja kukaa hapa wala usihofu kwanza hivi tunavyoongea ndio umehamia tayari na ishu niliyokuitia ni hii.Nataka kesho asubuhi ufanye juu chini upate bodaboda umgonge Baba Linna yani hakikisha mguu umevunjika au mkono,"Aliongea Joyce nakumwambia Thanga ishu aliyomuitia.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment