MAMA WA KAMBO 39

Walipofika ghetini ajabu waliona Masai anasinzia na pembeni yake kuna jiwe na limefanana aliloshika Thanga.
"Yani we fala umerusha jiwe halafu unajifanya unasinzia kenge wewe,"Thanga alimtukana Masai huku akimtingisha kwa nguvu.
"Amka wewe nani amerusha jiwe dirishani,"Masai aliulizwa na Joyce.
"Mimi amerusha kwani anaulisa nini?,"Kutokana na wenge la usingizi Masai akawa amejichanganya kujibu kwanza swali hakulielewa vizuri ukizingatia alikuwa usingizini na huko usingizi alikuwa anaota ndoto tamu mkewe Lembua anamuuliza amerusha pesa ya matumizi,wakati sasa anataka ajibu ndio akawa anatingishwa na Thanga na alipozinduka akajibu swali la ndotoni kuwa amerusha na hapo ndipo Linna akawa amechukua point tatu mhimu juu ya plan yake na sasa kesi akawa nayo Masai.
"We mpuuzi kweli yani umerusha jiwe ili iweje,"Joyce alimuuliza.
"Anaulisa nini tena mi aiwalewi mi ililala apa,"Aliongea Masai.
"Mwehu wewe nasema huna akili kabisa,umepasua kioo kile,"Thanga alimtukana Masai nakumuonyesha dirisha.
"Sio mimi amepasua,mimi ililala,"Alisema Masai.
"Nyoo situmekuuliza apa umesema ni wewe,nasema huna akili na utaona mshahara wako mwezi huu utanunua kioo muone kule jitu zima ovyoo.Baby twende chumbani tukamalize kazi,"Aliongea Joyce kwa ukali nakumtukana Masai kisha akamshika mkono Thanga wakaingia ndani?.
Plan ya Linna ikawa imekamilika kwa staili hio huku yakibaki matokeo ya Plani.
Masai pale ghetini alibaki ameduwaa tu huku akitema tema mate kumaanisha amechukia sana kutukanwa.
Joyce na Thanga baada ya kuingia ndani hawakushtuka kabisa kuwa Linna amefanya yake,walivua nguo zote wakala moja 18+,walipomaliza Thanga aliingia bafuni kuoga na Joyce alivaa taulo akachukua yale mafuta ambayo aliweka dawa.Asijue Linna yenye dawa kamwaga kaweka mengine,alienda chumbani kwa Baba Linna akafungua mlango nakuingia.
"Vipi baby mbona unalia,nini tatizo,"Joyce alimuuliza Baba Linna baada ya kuona amekaa kitandani huku analia.
"We umenifungia mlango naita huitiki,halafu hujalala humu ndani sijui ulikuwa wapi na hujui njaa inauma na hapa inabidi niende hospital,"Alijibu Baba Linna huku akilia.
"Sasa baby usiwe kama mtoto mi mwenzio nilikuwa hospital,usiku ule nilipigiwa simu shangazi anaumwa hivyo nikaenda na asubuhi hii ndio nimerudi,"Aliongea Joyce uongo huku akimshikashika kidevuni Baba Linna,ukweli hakuwa huko hospital bali alikuwa na Thanga mpenzi wake wanakula burudani na mambo ya kwa mganga.
"Ooh! Kumbe pole sana baby na Shangazi anaendeleaje,"Aliuliza kwa upole akionekana kuumia kuumwa kwa shangazi yake Joyce wakati hamna cha shangazi wala babu yake shangazi.
"Asante sana baby pia anaendelea vizuri ingawa inatakiwa pesa milioni 10 akatibiwe Nchini Kenya,"Joyce aliongea tena uongo ,lengo lake nikumpima aone anasemaje.
"Jamani sasa kama pesa ndio tatizo nenda bank kachukue hio milioni wape ili tuokoe maisha ya shangazi,"Alisema Baba Linna.
"Wawoooo baby ndio maana nakupenda sana,basi naomba niende sasa hivi we oga nikirudi nikupeleke hospital,"Aliongea Joyce huku moyoni akisema anaenda bank kutoa kumi anaweka kwenye account yake huku zile m700 na zaidi akisubiri mpaka amuue Baba Linna,asijue Mama Linna alishafanya yake na mle mpaka sasa imebaki 48m na pointi.
"Sawa baby nenda chai umepika au ili nikioga ninywe,"Aliuliza Baba Linna.
"Ndio ukioga tu utaikuta mezani pia mafuta ya kupaka haya,"Ajibu Joyce nakumpa mafuta,lengo anavyorudi toka bank akute tayari Baba Linna haoni.Hakujua Linna amechana mkeka nakubet kwa Thanga au kwake mwenyewe maana mafuta yale ya Thanga ndio yenye dawa na mmoja kati yao akipaka tu biashara imeisha ndio basi tena kawasalimie.
Baba Linna alipokea yale mafuta akaweka nakuingia bafuni,Joyce nae alivaa nguo nzuri akajipulizia pyafumu nzuri akatoka mle chumbani nakwenda chumba ambacho yupo Thanga na ndicho ambacho walilala.
"Baby natoka mara moja,baada ya saa moja narudi,"Aliagwa Thanga na Joyce.
"Powa powa mi nipo namalizia kuoga,"Alisema Thanga,basi Joyce alitoka mpaka sebuleni akamkuta Linna anafuta futa TV.
"Hapo safi sio unakaa tu na ukimaliza toka nje kumwagilia maua mi natoka nitarudi baadae,"Aliongea Joyce alikimwambia Linna.
"Sawa boss naenda kwa nimalize,"Alisema Lina huku moyoni akiombea ile dawa impate mmoja kati yao ili wajue malipo ni hapa hapa duniani.
Joyce alitoka nje akawasha gari nakwenda bank huku akiwa na furaha.
Huku nyuma Baba Linna alioga,alipomaliza alipaka yale mafuta vizuri akavaa nguo huku akijitahidi asitoneshe mkono wake aliovunjika.
Baada ya kuvaa alitoka nakwenda sebuleni kupata chai nzito,akiwa sebuleni alimuona Linna anatokea chumbani kwake akafika mpaka pale alipo Babake.
"Baba shikamoo,"Linna alisalimia.
"Marahaba sema shida yako,sitaki uniangalie ninavyokunywa chai,"Baba Linna aliitika salamu nakuongea kwa ukali.
"Baba mpaka hapa tulipofikia kiukweli kabisa siwezi kusema shida yangu ukanisikiliza,labda niombe tu unipeleke shule maana wenzangu watakuwa wameanza masomo,"Linna alimwambia Babake huku machozi yakimlengalenga.
"Kuhusu shule mpaka aamue Joyce mke wangu,kama atakubali utaenda akikataa basi utakuwa house girl humu ndani,"Aliongea Baba Linna maneno hayo yalimuumiza mno mtoto Linna maana alijua shule ndio basi tena sababu alishamwambia mambo ya shule asahau.
"Baba nashukuru sana pia asante kwa kunileta duniani kunitesa,"Aliongea Linna nakutoka nje kumwagilia maua.
"Mlaumu mamako kwa kukuzaa mbuzi wewe,kabla hajafa ungemuuliza alishindwa nini kuniambia nivae condom mpaka akakuleta kitoto kimbeya kinoko kinafki tena kibaya sura na kwa taarifa yako ukiona hapa unateswa nenda kaburini ukakae na mamako,"Aliongea Baba Linna kwa dharau na kejeli kwa mwanae asijue huyo ndio amemuokoa asiwe kipofu.
Maneno yale aliyasikia vizuri kabisa na hakika yalimuumiza mno kuliko kitu chochote,alikaa chini mtoto Linna nakuanza kulia huku akimtaja mwenyezi Mungu.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment