MAMA WA KAMBO 40

Maneno yale aliyasikia vizuri kabisa na hakika yalimuumiza mno kuliko kitu chochote ukiacha kifo cha mamake,alikaa chini mtoto Linna nakuanza kulia huku akimtaja mwenyezi Mungu.
"Mungu wangu lipi baya nimefanya hapa duniani na kwanini uliruhusu nizaliwe ee Mungu ulijua haya yatatokea,ungeweza kutoruhusu nizaliwe Mungu maneno aliyosema Baba yanaumiza mno iiii iii kwanini mimi lakini Mungu inamaana na watoto wengine Baba zao wanawafanyia hivi hiij😢😢😢nionee huruma sina mama,umemchukua.Baba nae ndio hivyo namsaidia lakini natukanwa naambiwa mnoko,Mungu ulisema watoto wadogo acheni waje kwangu,maanake utatulinda nakutuongoza tutende yaliyo mema na si mabaya mpaka pale tutakapotimiza ndoto zetu.Mungu mimi bado mdogo,nionee huruma na kwakua ulijua nitazaliwa nitapitia haya na Baba leo ananiona mbwa takataka nisiyefaa,basi Mungu huna budi kunilinda,kuniongoza vyema chini ya jua nikitambua sina Baba duniani bali Mungu wa Mbinguni uliyetuumba kwa maksudi maalamu,ni imani yangu Mungu utanilinda kama ulivyowalinda na kuwaokoa wana Israel katika mikono ya farao,"Mtoto Linna alimaliza kumwambia shida zake Mungu,licha ya awali kuanza kumlaumu Mungu kuwa kwanini aliruhusu azaliwe lakini mwisho Mungu anabaki kuwa Mungu na ndio maana Linna mwisho alimuomba amlinde.
Baada ya hapo mtoto Linna aliinua mikono juu ikimaanisha anamwambia Mungu kuwa amejikabidhi kwake.
Aliinuka nakwenda kumwagilia maua huku moyoni akiwaza adhabu toka kwa Joyce maana aliambiwa asiwe anamwambia chochote Babake kama ana jambo amwambie yeye,sasa leo kajikoroga kamwambia maswala ya shule wakati alionywa nakukatazwa.
"Basi tu sasa nitafanyaje Mungu wangu wa haki atanilinda,"Aliongea mtoto Linna akianza kumwagilia maua hasa ile sehemu ambayo alifukia hati.
Thanga nae kule bafuni alikokuwa anaoga alimaliza na sasa alikuwa ameanza kujipaka mafuta yale yale yenye dawa.
Alianzia kichwani,akaja usoni.Wakati anaanza mwilini ndipo akagundua yale mafuta yamechanganywa na dawa tena ile ile maana aliiona kabisa wakati Joyce anachanganya kwenye mafuta ya kumpa Baba Linna.
Kwanza alishtuka Thanga wawatu,haraka alimpigia simu Joyce nakumuulizia vipi dawa kwenye mafuta yake imefikaje.
"We nae vipi nipo bank bhana dawa si iliyobaki si ipo hapo hapo nyingine ndio ile tumempa yule,"Aliongea Joyce simuni nakukata simu akijua ni utani wa Thanga kumbe mwenzie yupo siriazi.
"Halafu huyu anamambo ya kijinga,hii si dawa hii tena ile ile inamaana ameniwekea na mimi ili niwe kipofu ,uwiiiii iiii nimeisha Thanga nitaambia nini watu,nitawaonaje mimi ,kitumbua nitaonaje uwiiiii iiii,"Aliongea Thanga nakuanza kulia sababu alijua supu imeingia nzi shilingi imepinduka Joyce kamfanyia umafia ,hakujua kuwa ni Linna ndio kafanya huo mchezo amewavalisha jezi na mchezo hawajauelewa beki ameenda mbele no9 amerudi beki na kipa kaenda forward goal limebaki tupu Linna kamaliza wamebaki hawaamini wanachokiona Thanga ameisha.
Thanga alilia sana sababu alijua upofu ukianza hata Joyce atamkimbia maana alivyo na tamaa ya wanaume anaweza mpiga chini muda wowote.
"Uwiiiii Mama madhambi niliyofanya nimelipwa tayari na Mungu ,uwiiiii uwiiii Mungu nisaidie naona ukungu,sioni sioni uwiiiii uwiiii,"Thanga aliongeza kilio baada ya kuona ameanza kuona ukungu,vyovyote vile moyoni alijua tayari ukipofu ndio umeanza.
Haraka alitoka mbio mle chumbani nakwenda sebuleni huku akijigonga gonga kwenye vitu.
"Shemu makelele pia unajigonga,huoni au unaigiza maana pia uko uchi,"Baba Linna alimuuliza Thanga na muda huo Linna alikuwa ndio anaingia hivyo swali lake kwenda kwa Thanga alilisikia.
"Uwiiiii jamani sioni sioni sioni sioni sioni uwiiiii jamani sioni msaada wajameni uwiiii,"Thanga hakujibu swali badala yake aliendelea kuruka ruka nakupiga kelele.
"Hahahaha huoni vipi sasa,si jana ulikuwa vizuri tu au marelia imepanda kichwani ,"Alisema Baba Linna huku akicheka.
Thanga hat hakuongea zaidi alizidi kulia nakuruka.
"Baba nikwambie kitu,"Linna alimuuliza Babake.
"Niambie ila usiwe umbeya,"Alisema Baba Linna.
"Lakini usimwambie Aunt Joyce,"Alisema Lina.
"Kama kizuri simwambii ila kama kibaya namwambia."
"Baba ni kizuri kwangu na kwako."
"Haya ongea nakuskiliza,"Aliongea Baba Linna na ndipo akaanza kumweleza Babake kila kitu tangu Joyce anaongea kuhusu kwenda kwa mganga na kurudi na dawa kisha kuchanganya ili ampe yeye Baba Linna na akihitimisha namna alivyomuokoa kwa ujanja alioufanya na mwisho Thanga upofu kumkuta.Linna alisema yote hayo akijua Babake atachukua hatua kali za kuwatimua wote wawili kisha abaki ye na Babake na upendo wa Baba na mwana uwe kama zamani licha ya Mama Linna kutokuwepo.
Lakini cha ajabu na cha kushangaza Baba Linna alivyosikia vile alicheka sana nakusema.
"Linna muongo na mnafiki yani unamuonea Joyce sana pia una roho mbaya mno ona ulivyomfanya shemeji yani we litoto sijui upoje subiri mke wangu Joyce aje nimwambie ujinga uliofanya,"Hivyo ndivyo Baba Linna aliongea,hakika alionyesha udhaifu mno mbele ya mwanae.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment