MAMA WA KAMBO 41

Lakini cha ajabu na cha kushangaza Baba Linna alivyosikia vile alicheka sana nakusema.
"Linna muongo na mnafiki yani unamuonea Joyce sana pia una roho mbaya mno ona ulivyomfanya shemeji yani we litoto sijui upoje subiri mke wangu Joyce aje nimwambie ujinga uliofanya,"Hivyo ndivyo Baba Linna aliongea,hakika alionyesha udhaifu mno mbele ya mwanae.
"Mpaka hapa nilipofikia ni ukweli usiopingika kuwa sina Baba,kweli tenda wema nenda zako usingoje shukrani.Nimemuokoa lakini bado haniamini Mungu mimi kwa nafasi yangu kama mtoto nimejitahidi kila njia ya kumwambia lakini hanielewi basi sina jinsi sina namna zaidi ya kumwaacha hivyo hivyo kama watamuua wamuue mi nitafanyaje sasa,saizi ningoje tu adhabu,"Aliongea Linna kwa uchungu baada ya kumweleza Babake na kila kitu alichofanya na Baba kutomuelewa nakusema anamwambia Joyce.
"Tena uondoke hapa mbwa wewe sitaki uongee na leo iwe mwanzo na mwisho kunishobokea,ukiona sehemu nipotezee tu kama unashida kaburi la mamako unalijua nenda huko nyau wewe,"Alisema Baba Linna kwa dharau dhidi ya mwanae,Linna kusikia hivyo hakusema chochote.Alikaa kimya tu maana hata angeongea angeonekana mnafiki tu,aliinuka sofani nakutoka nje huku mawazo yakiwa yamemzonga mno hakujua nini hatima yake maana game alilolicheza Baba Linna la kuwa na mchepuko Joyce kumleta nyumbani akimfanya mdogo hapo ndipo lilipofikia supu imeingia nzi shilingi imepinduka Linna haamini kabisa anachoona nakusikia kuwa yule ndie Babake kipenzi.
"Mungu narudia tena,mi si chochote mbele ya Baba na Joyce,tizama mateso,manyanyaso na changamoto ninazopitia.Mungu sina uwezo wa kupambana nao na ndio maana najikabidhi kwako upambane nao mwenyewe pia umpumzishe mama huko kaburini alale kwa amani nampenda sana,ninaomba nakushukuru huku nikirudisha sifa na utukufu kwako Baba yetu wa Mbinguni (Amen),"Alisali Linna akiongea na Mungu wake akiwa nje anamwagilia maua.
Thanga nae mzee wa plan bado alikuwa anapiga kelele,na muda huo alikuwa amekaa chini anagalagala.
Baba Linna maneno aliyoambiwa na Linna alianza kumwambia Thanga a 2 z,hakika akili yake ilikuwa haina akili kabisa.
Thanga nae kusikia vile alianza kumlaumu Linna kwa aliyoyafanya.
"Shemeji mwanao alichofanya sio kabisa ona sasa bora ungekuwa wewe kipofu,sasa mimi itakuaje maana mganga alisema dawa ya kuponya haipo,"Thanga alimwambia Baba Linna huku akilia taratibu.
"Ndio hivyo shemeji bora mngefanyaga kwa uhakika sasa nyi mnamwachia Linna ona amekufanya kipofu,nafuu angeacha Joyce anifanyie mimi tu kuliko wewe maana mimi tunapendana sana na uzuri nilimwambiaga mganga aliyeenda kuniroga nimpende kama yupo aende akaongeze,"Kubwa jinga Baba Linna aliongea kikubwa akimlaumu Linna,alitaka apewe yeye na si Thanga.
"Ndio hivyo shem mwanao kavuruga mipango kwa mkeo aje umwambie kila kitu ikiwezekana apate adhabu kali,"Alisema Thanga.
"Shemeji we usihofu kabisa kwa arudi utaona tu,naapia kidole changu cha kushoto lazima damu ya Linna imwagike,"Aliongea Baba Linna akionyesha kidole chake.
Joyce a.k.a Mama Plan alifika bank kuhamisha pesa milioni 10,alimdanganya Baba Linna kuwa shangazi yake anaumwa kumbe uongo tu ni janja yake ya kumfilisi Baba Linna na kubwa zaidi kujua pesa zipo au hazipo maana awali alienda alikuta kuna 30k tu.
Alipofika wakati anafanya prose's za kuhamisha ndio alipigiwa simu na Thanga kuhusu dawa,ye alijua ni utani tu mpenzi wake anamtania.Hakujua kuwa ni kweli Linna kawavalisha jezi na mchezo hawajauelewa kipa ameenda mbele,beki zipo kushoto streka karudi beki Linna kamaliza mchezo Thanga haoni.
Hilo hakujua na ndio maana alikata simu akijua ni Baba Linna ndio haoni,basi aliendelea na taratibu za kuhamisha pesa na Bahati nzuri akafanikiwa kuhamisha ndipo akajua kumbe zile 750m bado zipo na sasa zimebaki 737 au 38 hivi,hakujua ilikuwa 50m na sasa zimebaki kwenye account 35m au 36m hilo mama plan hakujua sababu hakuangalia.
Basi baada ya kuhamisha alifurahi mno,alitoka nakupitia kwenye zile hotel nakutaka pesa na akawambia ye boss Baba Linna ni mmewe.
Wale wahudumu wanaohusika kusimamia kwa kuwa walimjua na walitambulishwa basi hawakua na noma kabisa,walimpa pesa zaidi ya milioni 5 akaanza kurudi nyumbani akiwa na furaha.
"Huyu mwanaume hii wiki hamalizi na pesa zipo hivyo lazima nifanye juu chini afe kabisa nikamtupe na marafiki zake wakiuliza nawambia sijui,maana nikisema nisubiri sijui akonde sijui ni kupoteza muda tu mi nataka nianze kujichana na mme wangu Thanga tuinjoy maisha,"Aliongea Joyce mama plan akiwa njiani kuelekea nyumbani.
"Yani sitojali ameteguka mguu sijui kavunjika mkono mi naua tena kwa mkono wangu sitaki kukodi watu,"Alizidi kuongea Mama plan na tayari alikuwa amefika nyumbani,ajabu alipofika alishangaa kuona Thanga amekaa chini anagalagala nakulia huku Baba Linna akijitahidi kumtuliza.
"Nyi vipi mbona siwaelewi kulikoni,"Joyce aliuliza na ndipo Baba Linna kubwa jinga mwanaume aliyeovadoz limbwata akaanza kumwambia kila kitu aliachoambiwa na Linna na akahitimisha kwa kusema anaomba Linna apewe adhabu kali ambayo itakua kumbukumbu kwenye maisha yake.
"Dah! Linna huyu kafanya na kakwambia hayo yote,"Aliulizwa Baba Linna.
"Ndio mke wangu,ndiye aliyevuruga mipango,"Ajibu Baba Linna.
"Sawa sawa subiri nitakachomfanyia hatokuja kunisahau mpaka siku anaingia kaburini,hapa alipogusa amegusa pabaya ni kheri achezee transformer kuliko kuichezea furaha yangu,nasema ataona,"Aliongea Joyce kwa ukali huku akipiga pushapu.
Alipiga pushapu tatu akainuka nakumufuata Linna kule nje alikokuwa anamwagilia maua.
Alipomfikia alimchota mtama Linna akaanguka chini puu!!.
Kosa la kupigwa Linna alilijua kabisa hivyo hakuuliza.
"Inuka inuka nifate sebuleni mbwa wewe,"Aliambiwa Linna.
Linna aliinuka huku machozi yakimlengalenga nakuanza kumfata Joyce.
Walipofika sebuleni Joyce alimshika Thanga akampeleka chumbani nakumwambia atulie maji yamemwagika hayazoleki awe mpole kisha akarudi sebuleni ambapo yupo Linna na Babake.
"Linna sitaki nikupige maana umekuwa sugu,sasa nataka uchague adhabu moja kati ya hizi tatu,moja nikutoboe macho,mbili nikukate pua na tatu nikate vidole vyote haya chagua haraka,"Joyce alimwambia Linna achague huku ye ameshika kisu mkononi.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment