Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 6


Review: 'Tyler Perry's Temptation' is very Perry, indeed - Los ...


"Mama ninayosema ni kweli kama huniamini basi ipo siku utajua tu kwa kuona we mwenyewe,"Linna alimjibu mamake.


"Mme wangu inamaana Linna ni muongo,"Mama Linna alimuuliza mmewe.
"Ndio Linna ni muongo tu,"Baba Linna alijibu.

"Mh! Wifi yaishe mtoto amekosea tumsamehe,"Mama Linna alimwambia Joyce asijue wenzie wanamchora tu.

"Sawa wifi ila asirudie tena,"Joyce aliongea.

"Huyu mtoto mnoko sana inabidi ale fimbo,"Baba Linna aliongea kwa ukali.

"Baba nisamehe usinipige,"Linna aliomba msamaha huku anaanza kulia maana alitegemea mamake atakuwa upande wake lakini kamgeuka.
"We lazima uchapwe huna adabu."

"Mme wangu mpige tu,"Mama Linna nae alikazia.

"Baba usinipige mi ni mwanao,"Aliongea Linna huku akilia.

"Ah! Lazima uchapwe,kwanza kalete fimbo we mwenyewe."
Linna hakuwa na jinsi zaidi ya kwenda nje kutafuta fimbo nakurudi nayo ndani kisha akampa babake.

"Baba unanipiga huku kosa umefanya wewe sawa baba nipige tu,"Aliongea Linna baada ya kumpa Babake fimbo.

"Linna sitaki tubishane lala chini."
Linna alilala chini na babake akaanza kumchapa.

Alimchapa fimbo saba,mamake nae alipokea fimbo akaanza kumchapa
fimbo zisizo na idadi huku akisema mwanae hana  adabu,lichonganishi,linaongea uongo kwa wakubwa.
Alivyoona ametosheka alimuacha.
"Haya inuka nenda nje kalilie huko."

Linna aliinuka huku analia nakutoka nje,alizunguka nyuma ya nyumba akaanza kulia,alipochoka alinyamaza nakurudi ndani.Huko alimkuta mamake na Aunt kwa mjibu wa babake wamekaa wanaangalia tv huku wanacheka wanagonga na mikono.



Linna alikaa pembeni ya mamake na muda huo huo simu ya mamake iliita,Mamake
alipokea akaongea na mpigaji kama dakika mbili kisha akakata.
Alivyokata alimwambia Joyce kuwa anatoka mara moja atarudi baadae kidogo.

"Haya wifi uwahi kurudi."

"Nawahi ila jiko lile pale."

"Aya wifi nitapika usihofu."
Mama Linna aliinuka akaenda chumbani akajiandaa akatoka.





Sebuleni walibaki Linna,babake na Aunt.
"Linna!!,"Ant yake alimuita.

"Abee!"Linna aliitika.

"Kwanini unatabia mbaya,"Aliulizwa?.

Linna alikaa kimya?.

"Nakuuliza kwanini unatabia mbaya."
Kwa mara ya pili Linna hakujibu swali badala yake aliinuka nakwenda stoo,huko alichukua machungwa akamenya nakuanza kula.Hakujibu maswali toka kwa Aunt yake sababu aliogopa majibu yake yangemuudhi.

Aunt au Joyce alipoona Linna kaondoka pale sebuleni aliamua kumfata Baba Linna sehemu aliyokuwa.

Linna nae kule alitoka na machungwa yake,alipofika sebuleni  alikuta Aunt yake  hayupo.
Haraka alifunua pazia la dirishani
akachungulia akaona  Babake anachezea chakula cha watoto kwa Aunt yake.


"Mh! Lazima nifanye kitu,"Aliongea Linna huku akiachia pazia ambalo alifunua.
Baada ya kuachia lile pazia haraka alienda chumbani kwa Aunt yake,akaanza kupekua nguo.
Shida yake ilikuwa ni chupi na sidiria na kweli alizikuta,haraka alichukua nakwenda kuweka chumbani kwa mamake juu ya kitanda.
Lengo la haya yote mamake akirudi aone mwenyewe,maana kashindwa kumuamini mwanae.
Alipotoka chumbani kwa mamake alirudi pale sebuleni alifunua pazia kwa mara ya pili nakuchungulia akakuta Aunt yupo uchi afu anamvua nguo babake.


Haraka Linna alirudishia pazia akatoka nje nakwenda mpaka pale walipo huku lengo babake asimsaliti mamake.


"Babaaa!!!!!,"Linna alimuita Babake baada ya kufika pale.
Kwanza walishtuka sana kusikia sauti ya Linna hawakutegemea kama atafika pale kwenye bustani.

"We Linna unataka nini huku,"Joyce alimuuliza Linna akiwa anajiziba sehemu za siri.
Kabla Linna hajajibu Babake nae aliuliza.

"Linna nini huku,hivi upoje we mtoto."

"Baba njaa inauma nataka chakula,"Linna alimjibu Babake.

"Dah! Yani we Linna unaninyima raha sana,"Baba Linna aliongea kwa masikitiko.

"Baba nakunyima raha ninavyotaka chakula,"Linna alimuuliza na Babake alikaa kimya?.


"Baba nakuuliza nakunyima raha mi mwanao,"Linna alimuuliza tena.

"Mh! Mwanangu nenda ndani nakuja,"Aliambiwa Linna.

"Sawa Baba,"Linna aliondoka pale nakurudi ndani?.


Huku nyuma baba Linna alimwambia Joyce kuwa waache kwanza kula burudani maana Linna  anamachale hivyo watafute sehemu ingine.


"Ah! Baby mwenzio nina hamu,mtoto asikusumbue au twende ndani,"Joyce aliongea.

"Powa twende ndani baby,"Baba Linna aliunga mkono hoja.

Walivaa nguo zao wakaingia ndani,wakamkuta Linna amekaa tu sebuleni.

"Baby ebu mpikie mtoto,"Baba Linna alimwambia Joyce.


"Jamani twende kwanza ukanipe tamu,"Aliongea Joyce huku akideka.


"Hapana mtoto ana njaa ebu kampikie hata mayai."

"Sawa baby ila mwenzio ninahamu sana au hunipendi."

"Nakupenda sana basi twende chumbani."
Muda huo wanaongea Linna alikuwa anawachora tu.
Walishikana mikono wakaanza kuelekea chumbani.



"Babaaa!!!!"Linna alimuita Babake ajabu safari hii alikaa kimya tu hakuitika lakini ghafla mama Linna aliingia akakuta wameshikana mikono na karibu  wanaingia chumbani.

Linna akabaki kimya hakutaka kutia neno maana mamake mwenyewe kaona.

"Safi leo kajionea mwenyewe kwa macho yake,"Aliwaza Linna akitegemea mamake atamfukuza Joyce lakini cha ajabu mama Linna akasema.
"Wawoo mtu na kakake mmependeza sana jamani."

Joyce na Baba Linna walishtuka sana halafu wakajibu aah!! Umeonaeee mtu na dadake kwa raha zetu.


Linna ndio alibaki hoi maana alitegemea mamake atakinukisha lakini hamna eti anawachekea tu.


"Nawaona aisee mtu na Dadake,"Aliongea Mama Linna nakukaa  kwenye sofa.

Joyce alimuachia Baba Linna akaja akakaa karibu na mama Linna na lengo Linna asimwambie mamake juu ya alichoona kule nje na maneno aliyosikia.


Baba Linna ye alienda stoo kuzuga zuga.
"Wifi umewahi kurudi,"Joyce aliongea.

"Ah! Nilikuwa napeleka funguo tu."

"Mh! Sawa halafu hata chai sijapika,"Joyce aliongea.

"Wifi hata usiwaze kwa nipike mi mwenyewe,"

"Haya wifi."
Mama Linna aliinuka na Linna  akamuita mamake.

"Mwanangu unasemaje,"Mama Linna aliitika.

"Mama, Baba na Aunt walikuwa chumbani kwako na sasahivi walitaka waingie mara ya pili,"Linna aliamua kusema hivyo lengo kuu hasa ni mamake asanuke kuwa huyu sio Aunt ni mchepuko.
Joyce alishtuka kusikia Linna ameongea hivyo?.

"Linna unasemaje,"Joyce aliuliza kwa mshangao huku Mama Linna mapigo ya moyo yakianza kubadilika.


"Nasema ulikuwa chumbani kwa Mama,"Linna aliongea kwa kujiamini sababu zile chupi na sidiria aliziweka kule chumbani kwa mamake na Babake.

"Wifi ni habari za kweli,"Mama Linna alivyomjinga badala akinukishe ye aliuliza kwa upole.

"Mwanao muongo sana"Joyce alijibu.

"Mama mi sio muongo kama huamini kaangalie chumbani,"Linna aliongea.


Mara baba Lina akaja pale sebuleni. "Nyi mnabishana nini?."

"Mme wangu chumbani kwangu mlikuwa mnafanya nini?."Baba Linna hakujibiwa swali ila akaulizwa.

"Ah! Yale yale kwani vipi mke wangu."

"Jibu swali baba Linna,"Mama Linna aliongea kiukali.

"Haya najibu sikuingia chumbani mimi na Joyce,"Baba Linna alijibu.

"Mama we ingia chumbani,"Linna alimwambia mamake.

Baba Linna na Aunt wakabaki wameduwaa kwa maneno ya Linna.

Mama Linna  aliingia chumbani akakuta juu ya kitanda kuna chupi na sidiria.

Inaendeleaa



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4