Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 5


Review: 'Tyler Perry's Temptation' is very Perry, indeed - Los ...

"Mwenzio Baba ameingia chumbani kwa Aunt tena alivaa tu taulo,"Lina alimaliza kumwambia mamake.
"Mwanangu Linna we umemwona saa ngap?"Mama Linna alimuuliza mwanae.

"Mama wakati nakuja huku ndio nimemuona Baba."

"Mwanangu sitaki uchonganishi kwa nimuulize babako kama ni kweli."

"Mama we muuli........Hata kabla Linna hajamaliza kuongea mara babake akaja nakukaa kitandani.

Alivyokaa mama Linna akamuuliza mmewe.
"Mme wangu kuna kitu mtoto kaongea."

"Kitu gani hicho mke wangu nambie."

"Linna amesema amekuona unaingia chumbani kwa Aunt yake huku umevaa taulo."

"Dah! Mke wangu kumbe nawe ziro kabisa."

"Mme wangu mi ziro tena kivipi wakati nakuuliza?"

"Nasema ziro kwa sababu unasikiliza mambo ya Linna wakati unamjua Linna ni mnoko,mi sikatai kwamba sjaingia aah nimeingia na nilikuwa nataka nimjulie hali mdogo wangu au ni vibaya mke wangu,"Baba Linna aliongea.

"Mme wangu basi yaishe vipi wifi kaamkaje lakini."

"Ah!  Wifi yako yuko poa kabisa."

"Aya mme wangu kwa nikaangalie taarifa ya habari."

"Sawa mke wangu na mi nakuja ila mwanao mwambie unoko aache."

"Mh! Mme wangu si wote ni wazazi wake we muonye tu."

"Aya namuonya we nenda."

Mama Linna alitoka mle chumbani akaenda sebuleni.
Linna nae  akataka kutoka ila babake alimuita.

"Abee baba,"Aliitika.

"Ebu njo hapa,"Linna alisogea alipo.

"Ebu piga magoti hapa,"Aliambiwa Linna.

"Mh! Baba nimekosa nini,"Linna alimuuliza Babake.

"Kosa lako hulijui ee."

"Ndio Baba silijui."

"Aa!  Kwanza piga magoti,"Linna alipiga magoti akatii amri ya babake.

"Kwanini we mnoko sana,"Linna aliulizwa.

"Baba mi mnoko."

"Ee we kanoko halafu kakuda sana unamwambia mamako mambo yangu ili iweje."

"Baba lakini unachofanya sio kizuri kumbuka mi mwanao nahitaji upendo wa baba na mama ndio maana nafanya hivi."

"Nyoo muone kule upendo gani unautaka,humu ndani chakula huli."

"Nakula."

"Tena matonge unakata makubwa kama mtu mkubwa,halafu ooh nataka upendo,upendo gani unataka usiku mrefu mwanangu kua uyaone mi staki unifatilie,"Alisema Baba Linna.

"Mh! Baba nahitaji upendo wa mama na baba,endapo utakuwa na mke mwingine mi nitapata taabu sana."Aliongea Linna huku akilia baada ya Babake kumuonya asimfatilie.

"Pumbavu kwanza sitaki ubishane na mimi,mi nimekuleta duniani halafu unisumbue nakuonya sjtaki ukuda kwenye hii nyumba sawa."Baba Linna  aliongea kwa ukali.

"Sawa ila mpende mama huyo Aunt umuache,ataivuruga hii familia."Aliongea Linna.

"Linna nimekwambia niache na sitaki unoko sijui kama umenielewa."

"Baba mi nakuelewa sana ila we ndio unashindwa kunielewa mi mwanao,hivi baba ungekuwa huna pesa huyu Aunt angekuja humu ndani,Baba mi nakwambia huyu kaja kaona una pesa."

"Halafu Linna we mbishi sana,unajifanya unajua kushauri eti.We katoto sijui kachawi au kuna mtu anakufundisha,ebu inuka uondoke na ole wako mama ajue utanitambua na saizi nakuonya kwa mara ya mwisho hata ukiniona na Aunt kaa kimya umeelewa."

"Ndio Baba nimekuelewa,"Aliongea Linna kiunyonge.

"Na unoko sitaki sawa."

"Sawa baba."

"Ole wako nisikie nitakata huo mdomo sawa."

"Baba hutasikia tena ila umuachAunt,Aunt atavunja ndoa yenu,"Aliongea mtoto Linna asijue babake kalishwa limbwata hajielewi.

"Pumbavu nimekukataza nini?"

"Samahani baba nisamehe."

"Embu toka hapa kenge wewe na ukiendelea na tabia hii nakupeleka shuleni ukakae huko huko,maana unaninyima raha."
Linna baada ya kufokewa alitoka mle chumbani,alipotoka alianza kulia huku akielekea sebuleni na alipofika alikaa sofa ambalo amekaa mamake.

Lakini akiwa pale amekaa mamake nae  akasema.
"Saizi mwanangu umekuwa kanoko sana hivi kwanini mwanangu."

"Mama mi sio mnoko mambo nayokwambia unayapuuzia ila najua mi ndio nitakaye kuja kuteseka huko mbele."

"Linna tena uishie hapo hapo utakuja kuteseka kwa lipi,Babako ana sheri,ana magari,ana mjumba huu tunaoishi.Mi mamako nina pesa uje uteseke kwa lipi,mwanangu au unapepo."

"Mama hamna aijuae kesho,Mama nakwambia vitu unasema mi mnoko na wakati hivo vitu unauwezo wa kuvitatua mara moja na siku ya kuja kuujua ukweli utakuwa umechelewa na utatamani siku zirudi nyuma uvitatue lakini utakuwa umechelewa.Mama mi ndio nitakae teseka,"Linna alimwambia mamake kwa uchungu lakini mamake hakumuelewa kabisa masikio aliziba.

"Linna usiniletee mambo ya kinoko hapa kwanza kaa kimya paka wewe."

"Mh!  Mama sawa nakaa kimya ila kuna siku utakuja kujua mwanao nini nilikua naongea."

"Toka hapa kwanza kaa kimya sitaki uniongeleshe pumbavu unatutia aibu mbele za wageni."
"Sawa mama."
Linna baada ya kupigwa biti na mamake basi aliamua kukaa kimya?.

Wakiwa pale sebuleni mara Aunt alikuja pale.

"Wifi za asubuhi,"Mama Linna alisalimiwa.

"Nzuri tu wifi yangu pole na uchovu."

"Asante wifi nishapoa hajambo Aunt yangu."

"Huyo apo hajambo kabisa."

"Linna hujambo,"Linna aliambiwa hajambo lakini alikaa kimya tu.

"We Linna Aunt yako anakusalimia hivi husikii au kiburi,"
Mama Linna alimsema Linna.

"Mama huyu siyo Aunt yangu huyu ni baby wa Baba,"Linna alimwambia mamake.

"We mtoto unasemaje,"Mama Linna akauliza kwa ukali.

"Mama kama ulivyosikia huyu na baba wanaitana baby,"Linna alimjibu mamake na muda huo Joyce alikuwa amepaniki.

"Mh! Huyu mtoto ana pepo yani kakangu nimuite baby wifi sasa mwanao ananivunjia heshima kabisa kumbe ndivyo unavyomfundisha mwanao,"Joyce aliongea kwa ukali huku akimshutumu Mama Linna.

"Jamani jamani jamani mi mtoto huyu we Baba Linna ebu njoo huku," Mama Linna alimuita baba Linna.

Baba Linna nae baada ya kuitwa mara moja akafika akitokea chumbani.

 "Nyi kuna nini hapa."

"Mme wangu naomba uniambie ukweli huyu nani yako,"Mama Linna  alimuuliza mmewe.

"Dah! Kweli mke wangu huna kumbukumbu,we jana nimekwambia huyu ni mdogo wangu anaitwa Joyce.Saizi tena unaniuliza."

"Mme wangu mwanao kasema huyu sio mdogo wako na mnaitana baby."

"Mke wangu huko umeenda mbali sana,usifate ya mwanao nisikilize mi mmeo nachokwambia. Huyu mtoto muongo anaropoka tu,"Aliongea Baba Linna huku nafsi yake ikimsuta sababu alikuwa anadanganya.

"Kweli wifi mwanao muongo sana,"Aunt au Joyce aliongea.

"We Linna kwanini unakuwa mchonganishi mwanangu,"Mama Linna alimuuliza mwanae maana tayari alijua Linna ni muongo.

"Mama ninayo.....
Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4