SEPTEMBER 1 SEHEMU YA NANE.

TULIPOISHIA JANA SEHEMU YA SABA.
"Hakuna shaka ilimradi ulinzi uwepo, jeshi la polisi watahusika katikati ya mabehewa tu kwa kujichanganya na raia. Askari kanzu watawekwa humo, ili usalama wa raia uwepo. Safari hii nahitaji iwe ya kihistoria, iende na kumalizika kwa usalama mkubwa bila ya kukumbwa na lolote"
TIRIRKA NA SEHEMU YA NANE ..
**
Norbert alipokaribia kufika kufika kwenye kiwanda cha kutengeneza magari ya kuchezea watoto, aliegesha gari lake njiani kisha akashuka akiwa na mkoba mdogo. Haraka alitembea na kuingia kwenye vyoo vya ghorofa moja lenye maduka mengi ya nguo. Huko ndani alibadili nguo zake, alipotoka alivaa nguo ya wafanyakazi wa kiwanda yenye rangi ya bluu pamoja na kofia ambayo ina nembo ya mahali anapoenda
Alirejea garini na kuweka mfuko ule aliyotoka nao, ambao ulihifadhi mavazi aliyoyavua. Hatimaye alitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea kiwandani, alipokuwa akikaribia kufika hapo alishtuka akishikwa begani na kujikuta akihama njia upesi. Alipomwona aliyefanya hivyo, alijikuta akishusha pumzi na kumtazama.
"Haya baba vipi siku hizi uandishi umebuma, au umetembea na mke wa kigogo wakakufilisi hadi umekuwa kibarua wa kiwandani", Mwanamke aliyemgusa alimwambia kwa dharau kuu., maneno hayo yalikaribia kumfanya hata akaribie kucheka ila alijizuia na kuvaa sura isiyo na mzaha.
"Jamila shida yako nini kwani? Ulisema unaachana na mimi ukinituhumu kwa umalaya wangu. Haya kuniona nikiwa mfanykazi wa kiwanda wewe kinakuuma nini?"
"He! Heee! Unalo babu weee, siyo wewe uliyekuwa ukijiona unavyowachukua kina dada kwenye kieskudo chako kile. Hivi sasa ndiyo umefikia huku. Ama kweli kuna alfa na umega.", Binti ambaye si mfuatiliaji wa vyombo vya habari alijikuta akiongea hivyo, haswa baada ya kumwona akiingia mahala hapo akiwa namna hiyo ilihali anajulikana umaarufu wake. Akili yake ikawaza ni maarufu asiye na kitu kama wengine wenyee kujulikana wana maisha ya duni, kumbe mwenzake yupo kwa ajili ya kingine.
"Haya ukimaliza uniambie niwahi kazini, niokoe kibarua changu", Kaila alisema
Binti alimwaga maneno yenye shombo kwa Kaila, alipoweka tu kituo wala mzee wa kazi hakuhangaika kumsemesha. Alipiga hatua kuondoka huku akimwacha akiendelea kuangua kicheko, ambacho kwake aliona ni sawa na kumpigia honi kiziwi.
Msichana huyo aliwahi kuwa na uhuasiano naye, ila alikuja kuvurugana naye baada ya kumkuta na mwanamke mwingine. Alijaribu kila aina ya uongo kuweza kumtuliza, ila haukuzaa matunda na hapo ndipo akajikuta akiwa na chuki kwake. Kumwona hapo kwa jinsi anavyopenda kumwona akiwa na hali mbaya, alikumbuka kumcheka na wala hakujua kama bado jina lake lipo palepale. Atamaizi vipi juu ya hilo, wakati kutwa ni kwenye mitandao kuangalia umbea na wala si habari maalum. Ndiyo maana akakosa zote zinazomuhusu hadi akafikia kumcheka hivyo, ilihali mwenzake anamwona ni punguani.
Norbert alipompita alikaza mwendo na hatimaye akafika lilipo lango la kiwanda, mahala hapo alikutana na mlinzi ambaye hakuonesha shaka naye. Alimpita tu na kuingia ndani, hatimaye akaja kufika kwenye eneo la ndani ambalo lina malori mengi yakiwa maegeshoni. Hapo aliishusha vizuri kofia yake kuzuia uso wake usionekane, aliingia ndani kwenye moja ya idara za sehemu hiyo.
Kaila alitokea upande ambap hushughulikia haswa kutengeneza viongozeo vya magari, huko ndiyo alidhamiria kuingia. Chipu ile huwa na mahali huunganishwa, moja kwa moja aliposikia inatoka kiwanda hiko ndiyo akahisi moja kwa moja inaundwa idara hiyo. Kutokana na watu wa humo asilimia kubwa kufanana mavazi hata wa idara tpfauti, aliweza kuingia bila wasiwasi
na akatokea upande ambao kuna wafanykazi wakiwa kazini. Norbert aliwapita wote na akafika eneo ambalo kuna wengine wenye kutumia bisibisi kufunga rimoti za magari. Napo aliwapita na kukuta mlango uliyooandikwa 'authorized only', huu aliuendea wala hakujali waliyomaanishwa kwenye maandishi yale ni kina nani.
Aliusukuma mlango huo uliyoundwa kwa vioo, ukafunguaka akaingie eno lenye korido yenye upana kiasi ikiwa na milango ya kambarau kwenye kila pande. Norbert alipeleka macho kwa umakini kisha akaishusha zaidi kofia kuhakikisha hakuna kiumbe anayeweza kuinasa sura yake, alifanya hivyo kwa kuhofia kamera za CCTV kuweza kuwepo eneo hilo. Alipiga hatua hadi alipofika mwisho wa korido ile, huko alikuta ngazi zenye kushuka chini. Bila ya kukawia alizishusha ambapo alikutana na mlango mwingine, huo uliandikwa maandishi kama ya ule wa kwanza. Isipokuwa tu kulikuwa na mlinzi mwenye kifaa cha kuchunguza vitu vyenye asili ya chuma mwilini, akiwa na kirungu tu na si kitu kingine.
"Hey! Sheria za hapa unazitambua wazi, huruhusiwei kufika huku rudi kwenye idara yako", Mlinzi alimkoromea huku akimsogelea, alipomfikia alimpelekea mkono kifuani akiwa na lengo la kumsukuma amrudishe alipotoka.
Loh! Hakujua kama hilo ni kosa kubwa amelifanya, kitendo cha kumgusa tu Norbert. Kiganja chake kilidakwa kwa wepesi wa hali ya juu kisha Kaila akamvuta kuja upande wake. Mlinzi alijikuta akienda mzimamzima kama ajiletae kumkumbatia mzee wa kazi, alipokaribia kugusana kifua na alimyefanyia kitendo hiko kwa wepesi wa hali ya juu. Alijikuta akipitiliza baada ya Norbert kuyumba pembeni, mlindaji aliapopita usawa wa N001 alipokea pigo moja la kisogoni akalegea viungo vyote na kuanza kuelekea chini.
Norbert alimdaka kwa haraka, aliangalia pande zote na kuona eneo hilo halina kamera. Alimburuza hadi kwenye mlango mmojawapo wa eleveta, hapo alibonyeza kitufe ambapo baada ya sekunde kadhaa ulifunguka. Alimsukuma humo ndani, kisha akaingia na kubonyez anamba ya ghorofa ya mwisho ya jengo lilipo juu yake. Alipofanikisha hilo alitoka upesi na kuiacha ifunge, Kaila akawa amemaliza vikwazo vyote sasa akaingia kuelekea ndani.
Mlango wa pili aliufungua akajikuta yupo kwenye chumba kidogo chenye mlango mwingine kwa mbele. Huku pembeni yake kukiwa na kibanda chenye vioo, mzee wa kazi alitupa macho pande zote na hatimaye akajitosa kwenye kibanda kilichopo pembezni ya hapo. Ndani alikuta kukiwa na tarakilishi ambayo inaonesha korido kadha ambazo hakuzipita, alpotazama pembeni alikuta mavazi ya mlinzi ambayo aliyanyakua upesi.
Eneo kilipo kiwanda cha kufufua simu zilizokufa Mbagala charambe kwa Mbiku, mahali ambapo kuna lango la kuingilia kiwandani hapo. Majira hayo bado gari za kampuni ya ulinzi ambayo ipo chini ya umiliki wa Watson ziliingia mfululizo, vijana wenye silaha za moto walishuka kwa wingi na kwenda kujipanga sehemu tofauti. Ujio huo wa watu hao uliwashangaza wafanyakazi wengi, ila hawakuwa na uwezo wa kuhoji waliendelea na kazi zao kama kawaida.
Muda mchache baadaye Huze aliwasili hapo akiwa na Watson, ulinzi imara waliyoukuta hapo baada ya kukagua waliona ungeweza kutosha kummaliza jasusi aliyewatia hasara kubwa ndani ya siku mbili tu. Hakuona kitu cha kuweza kuwafanya wamhofie tena, wao waliamini vijana hao wangemtia nguvuni. Hakujua tayari wamechezewa mchezo mbovu, laiti kama wangelimaizi hilo wasingeliweka nguvu kubwa hapo na kuimarisha kule kwenye mradi wao mwingine.
"Vipi hapa Huze unafikiri huyo jasusi anaweza kutoka kweli kwa ulinzi huu?", Watson aliuliza. "Hawezi kutoka katu, vijana hawa shughuli yao naifahamu fika si ya mchezo", Huze alijibu, muda huo wapo sehemu ya juu wakiangalia jinsi ulinzi ulivyo mkali.
"Unajua hawa vijana serikali inajua ni walinzi wa kawaida tu, ila ni hatari zaidi ya jeshi. Ukumbuke tumewapa mafunzo ya kijeshi na utumiaji silaha, huku wachache miongoni mwao wakiwa ni makomandoo"
"Ndiyo maana sina shaka nao, namsubiri huyo mshenzi mwenye kujifanya anajua kutumia silaha afike hapa. Ndiyo atajua kwanini tulipewa cheo na Alpha cha kuweza kuongoza kikosi hiki"
"Yaani hawa hata huyo N001 wanayeamini ni hatari, akiingia anga zao hawezi kutoka"
"Ok tuingie ndani kutazama mfumo wa ulinzi ulivyo haswa kwenye kamera za ulinzi", Huze alisema huku akigeuka nyuma na kuelekea ulipo mlango wa kurejea ofisini.
**
Eneo kilipo kiwanda cha kufufua simu zilizokufa Mbagala charambe kwa Mbiku, mahali ambapo kuna lango la kuingilia kiwandani hapo. Majira hayo bado gari za kampuni ya ulinzi ambayo ipo chini ya umiliki wa Watson ziliingia mfululizo, vijana wenye silaha za moto walishuka kwa wingi na kwenda kujipanga sehemu tofauti. Ujio huo wa watu hao uliwashangaza wafanyakazi wengi, ila hawakuwa na uwezo wa kuhoji waliendelea na kazi zao kama kawaida.
Muda mchache baadaye Huze aliwasili hapo akiwa na Watson, ulinzi imara waliyoukuta hapo baada ya kukagua waliona ungeweza kutosha kummaliza jasusi aliyewatia hasara kubwa ndani ya siku mbili tu. Hakuona kitu cha kuweza kuwafanya wamhofie tena, wao waliamini vijana hao wangemtia nguvuni. Hakujua tayari wamechezewa mchezo mbovu, laiti kama wangelimaizi hilo wasingeliweka nguvu kubwa hapo na kuimarisha kule kwenye mradi wao mwingine.
"Vipi hapa Huze unafikiri huyo jasusi anaweza kutoka kweli kwa ulinzi huu?", Watson aliuliza.
"Hawezi kutoka katu, vijana hawa shughuli yao naifahamu fika si ya mchezo", Huze alijibu, muda huo wapo sehemu ya juu wakiangalia jinsi ulinzi ulivyo mkali.
"Unajua hawa vijana serikali inajua ni walinzi wa kawaida tu, ila ni hatari zaidi ya jeshi. Ukumbuke tumewapa mafunzo ya kijeshi na utumiaji silaha, huku wachache miongoni mwao wakiwa ni makomandoo"
"Ndiyo maana sina shaka nao, namsubiri huyo mshenzi mwenye kujifanya anajua kutumia silaha afike hapa. Ndiyo atajua kwanini tulipewa cheo na Alpha cha kuweza kuongoza kikosi hiki"
"Yaani hawa hata huyo N001 wanayeamini ni hatari, akiingia anga zao hawezi kutoka"
"Ok tuingie ndani kutazama mfumo wa ulinzi ulivyo haswa kwenye kamera za ulinzi", Huze alisema huku akigeuka nyuma na kuelekea ulipo mlango wa kurejea ofisini.
**
"Bosi kuna faili hili muhimu inabidi lisainiwe upesi sana kabla hujandoka", Msichana mmoja alikuwa akitembea na kijana aliyevaa nguo nadhifu akiwa na mkoba mkononi. Binti huyu alishika faili pamoja na kalamau akimwonesha.
"Aaah! Eliza mbona unalileta sasa hivi nikiwa natoka kuwahi kikao cha bodi ya wakurugenzi. Muda wote ulikuwa wapi?"
"Bosi ndiyo limewasili sasa hivi, linahitajika kurejeshwa idara ya waajiri ni muhimu sana"
Kijana huyo alichukua kalamu akiwa amesimama usawa wa mlango wa kamabrau, alisaini huku akimwambia binti abonyeze kitufe cha kushuka cha lift hiyo. Alipofanya hivyo kengele maalum ililia, naye alimpatia faili baada ya milango ya lifiti kufunguka.
"Jesus!", Kijana alijiseme kwa nguvu huku akiangusha mkoba wake kwenye mlango wa kambarau, ndani alimshuhudia mlinzi akiwa amelala chini hajitambui. Binti aliyepokea faili ndiyo kabisa lilimwanguka na akapiga kelele.
Walinzi waliyopo eneo la karibu, walikuja haraka na kujionea hali halisi ilivyo. Kwa haraka kengele ya hatari ilibonyezwa huku wachache wakikimbilia eneo ambalo wana silaha. Wengine walimtoa mwenzao kwenye lifti, wakiwa mbele ya huyo bosi ambaye hakuelewa kumetokea nini hadi akawa hivyo.
"Nasema hivi, milango yote ifungwekwa kila idara. Walinzi wa geti kuu nao wafanye kazi yao. Vijana nahitaji wenzenu wapekue humu ndani ya jengo zima, hata idara nyingine tujue kuna nini", Bosi alisema.
"Bosi!", Amri ilipokelewa na kwa haraka mlinzi aliongea kwa simu ya upepo, aliwapa taarifa wenzake waliyopo nje juu ya maagizo hayo huku wengine wakimpa huduma ya kwanza mwenzao yule hadi alipoamka.
Mlinzi alizinduka baada ya kuchomwa sindano kwa haraka aliponekana asingerejewa na fahamu muda ndani ya mfupi, alijikuta akitazama hapo kwa sekunde kadhaa ndipo akajua yupo ghorofa ya juu mbali na ofisi yake ya kazi, jambo hilo lilimshngaza ambapo alichukua dakika kadhaa ndipo alipoweza kukumbuka kile kilichotokea.
"Bosi tumevamiwa, kuna mtu amevaa ovaroli za vibarua alifika na kunifanyia haya eneo langu la lindo", Alisema hata bila ya kuulizwa, maelezo yake yalifanya msako mkali uanze. Ikatolewa amri wafnayakazi wa idara ya rimoti za magari ya watoto wahojiwe juu ya hilo, wakifanya hayo hawakujua mtu wanayemtafuta yupo eneo gani.
ITAENDELEA
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment